Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni (official visit) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa Rais kwanza mwanamke.

Kina Queen Elizabeth wametawala dunia miaka na miaka. Majukumu mazito kuliko aliyonayo.
Au yule Makel (kama sijakosea) wa Ujerumani
 
Anachukua tahadhari juu ya mfumo dume!

PENGINE BAADA YA TAREHE 30/4 TUNAWEZA ONA MABADILIKO BAADA YA KUWA MWENYEKITI. HIVI SASA ANACHUKUA TAHADHARI NDIO MAANA ANAFICHA MAKUCHA!! PIA HUU NI MWEZI WA RAMADHANI KUHUTUBIA MCHANA NA SWAUMU SIO MCHEZO!!!
MAMA SAMIA HUU MWEZI MTUKUFU APUNGUZE KAZI ZENYE SHURUBA WAFANYE WASAIDIZI ZAIDI!
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa.

YAANI WEWE UNAWAZA KUWA Rais Samia NI WA KUTUNGA MIMBA KWA MAKAMO YALE?? HUJUI KUWA BINTI YAKE NI MBUNGE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR? NYIE WATU WENGINE NI WANGA TU!
 
Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Joice Banda wa Malawi
Good! Ellen Johnson shule imepanda kuliko rais wetu, hata hivyo alistahili sifa sana hasa kwa kuwa aliingia ofisini kwa kupigania nafasi. Liberia ikiwa ktk hali hovyo kabisa, hadi akaitoa kwenye shida. Tatizo ni wao waliingiza ushabiki wa mpira na kumchagua George Weah ambaye ni mwanaume na ni bure kabisa!! hawezi hata kutoa hotuba.

Urais siyo muhimu kwa sababu ya mwanaume au mwanamke. Hakuna sababu ya kuendelea kutaja mimi ni mwnamke, mwanamke, mwanamke. Ni rais, FINITO! Labda kama anataka vigelegele vya wale wanaowinda vyeo maana naona kuna akina mama wanahangaika kushangilia. Tujiamini na akiona mwanamke mwenye uwezo amchangue lakini siyo ku-balance gender mechanically na watu wasio na uwezo kama ilivyo bungeni.
 
Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni (official visit) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa Rais kwanza mwanamke.

Kina Queen Elizabeth wametawala dunia miaka na miaka. Majukumu mazito kuliko aliyonayo.
Juzi kati alikwenda Uganda...

Labda kama una maana ya kuwa aende Liberia kwa Ellen Sirlif Johnson au Germany kwa Angela Markel au Finland kwa Susan Marin viongozi wa nchi wenzake wanawake...
 
Nakuunga mkono asilimia mia moja
Wewe ni mwanadamu wa jinsia ya kike. Kila mtu anafahamu juu ya matatizo ya jinsia katika dunia hii na kila nchi inajitahidi kuondoa matatizo hayo. Njia mojawapo ni kuachana na hali ya kulinganisha jinsia hizi ktk kazi, ili tuzifunike tofauti hizo.

Tangu Samia uliposhika nafasi ya urais, kila hotuba yako imekuwa ni kama nafasi ya kujitetea kwamba unaweza nafasi hiyo, na kuwatetea wanawake wenzako. Ombi langu kwako, achana na kujitetea.

Angalia unavyoshangiliwa na wanawake wenzako, wakiona kama ni mafanikio yao kumbe wengine hawawezi kama wanaume wengine wasivyoweza.

Mfano mzuri dunia hii ni Margret Thatcher na sasa ni yule ‘binti’ mdogo anayeiongoza serikali ya Finland, Sanna Marin kama alivyokuwa Thatcher hataki kabisa kukaribisha jambo hilo la kuonesha wanawake wanaweza au hawawezi. Kwake yeye ni kiongozi na siyo kiongozi mwanamke.
 
Good! Ellen Johnson shule imepanda kuliko rais wetu, hata hivyo alistahili sifa sana hasa kwa kuwa aliingia ofisini kwa kupigania nafasi. Liberia ikiwa ktk hali hovyo kabisa, hadi akaitoa kwenye shida. Tatizo ni wao waliingiza ushabiki wa mpira na kumchagua George Weah ambaye ni mwanaume na ni bure kabisa!! hawezi hata kutoa hotuba.

Urais siyo muhimu kwa sababu ya mwanaume au mwanamke. Hakuna sababu ya kuendelea kutaja mimi ni mwnamke, mwanamke, mwanamke. Ni rais, FINITO! Labda kama anataka vigelegele vya wale wanaowinda vyeo maana naona kuna akina mama wanahangaika kushangilia. Tujiamini na akiona mwanamke mwenye uwezo amchangue lakini siyo ku-balance gender mechanically na watu wasio na uwezo kama ilivyo bungeni.
Support - naona kama kuna kukomoa komoa wanaume vile! Kana kwamba maisha yanaishia hapa! Yaani kama michezo wa draft!
 
una point kwa kweli
I think its enough.,

Mama SASHA uko vizuri tunakukubali.,endelea tu na kazi zako bila ishu za jinsia.,
 
Anaweza kuja kuwa bora kuliko wote waliomtangulia. Au anaweza kuwa wa ovyo kuliko wote waliomtangulia. Au anaweza kuwa hapo katikati.

Nafasi ndio hii. Aonyeshe uwezo wake. Aanzie wapi au aendelee vipi kutoka alipo ni suala la kwake

Hawezi kuwa bora akabezwa. Haiwezekani.
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa.
Sasa mama Samia anaenda kujifungua nini tena? Si ni mtu mzima kabisa pale alipo ina maana mumewe hawajazaaga watoto tu?
 
Wewe ni mwanadamu wa jinsia ya kike. Kila mtu anafahamu juu ya matatizo ya jinsia katika dunia hii na kila nchi inajitahidi kuondoa matatizo hayo. Njia mojawapo ni kuachana na hali ya kulinganisha jinsia hizi ktk kazi, ili tuzifunike tofauti hizo.

Tangu Samia uliposhika nafasi ya urais, kila hotuba yako imekuwa ni kama nafasi ya kujitetea kwamba unaweza nafasi hiyo, na kuwatetea wanawake wenzako. Ombi langu kwako, achana na kujitetea.

Angalia unavyoshangiliwa na wanawake wenzako, wakiona kama ni mafanikio yao kumbe wengine hawawezi kama wanaume wengine wasivyoweza.

Mfano mzuri dunia hii ni Margret Thatcher na sasa ni yule ‘binti’ mdogo anayeiongoza serikali ya Finland, Sanna Marin kama alivyokuwa Thatcher hataki kabisa kukaribisha jambo hilo la kuonesha wanawake wanaweza au hawawezi. Kwake yeye ni kiongozi na siyo kiongozi mwanamke.
Sex inferiority complex
 
Nilikuwaa na mheshimiwa flan tunafatilia hotuba aseee mtoa post upo sahihi mheshimiwa alisema hvo hvo HUYU HAJIAMINI BADO na anaonesha ni weak kabsa.... ANYWAY TIME WL TELL
 
Kuna taarifa ambazo hatuja zisibitisha kuwa kuna walio mshaur ajiuzulu kwa kuwa Ke sasa inawezekana anawajibu wao.
Haya ndio aliyakataa kwenye hotuba yake. Na alisema atawatafuta hata kama mnatumia VPN za Mabeberu ili mje mthibitishe hayo mropokayo mitandaoni.
 
Nilifikiri ni mimi mwenyewe niliyekuwa ninasikia hii kauli kama mara tatu sasa. Aachane na hiyo kauli na achape kazi. Pia hakutakiwa kuongelea mambo ya sumu ndiyo alifanya hata ambao tulikuwa hatujasoma hayo mambo ya sumu kwenda kutafuta na kuyasoma. Kama ni washauri wake waliomshauri walimuelekeza vibaya.

Ila mengine yote katika speech yake aliyawasilisha kwa ufasaha na weledi mkubwa...nina imani mabadiliko aliyoahidi kuyafanya kwa wahandisi wa maji yataleta ufanisi na tija katika miradi ya maji. Ninamtakia kila la kheri.
 
Anachotakiwa achape kazi tuone out pits. Tutampima kwa kazi na kwa ujunsia!
 
Sasa mama Samia anaenda kujifungua nini tena? Si ni mtu mzima kabisa pale alipo ina maana mumewe hawajazaaga watoto tu?
Nani alikwambia mama hawezi kushika mimba pale acheni theory mgando., wewe jibu mama akiwa mjamzito nchi itaongozwa na nani lakini pia akienda kujifungua nchi itakuwa na nani na sheria pale inabidi apewe miezi 3 likizo
 
O

Makamu wake si yupo
 
Back
Top Bottom