Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni (official visit) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa Rais kwanza mwanamke.

Kina Queen Elizabeth wametawala dunia miaka na miaka. Majukumu mazito kuliko aliyonayo.
Amepigiwa Uganda na mseven

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wanawake tunajiamini sana, tatizo ni kuwa tuko katika dunia ambayo mwanamke haruhusiwi kujiamini, Mwanamke ukijiamini utaitwa majina, utapewa majina, na inafika muda utaanza kuyaamini majina hayo ndiyo majina yako. Bado tuna changamoto kubwa, na battle letu ni kubwa sana.

Mama hajayasema hayo kwa bahati mbaya, kuna chokochoko kubwa kutoka dunia ya kiume.

Ameshapata nafasi, atafanya vizuri. Ambao hawajaridhika watulie tu.
Ukishasema dunia ya wanaume, binafsi nasema ni makuzi: Alishajiruhusu kuwa chini ya mwanaume, nasikia ni mke wa tatu: Wa tatu! Kwa maana nyingine sehemu kubwa ya maisha yake imekuwa ni mapambano hata na wanawake wenzake.

Kwa ujumla akiendelea kujitaja juu ya haya, anawaaminisha watu kwamba anatambua mapungufu yake na tutaanza kuyatafuta. Yeye asimamie madraka yake kwa vitendo na siyo mipasho kwa wanaomkwaza.
 
Rais kupewa support na mwanamke mwenzake siyo jambo baya maana kumbuka tupo kwenye mission ya Beijing.

Muhimu ni kuprove kuwa anaweza kufanya vizuri zaidi.
Kumbuka kuna hali tofauti kabisa kati yake na m'mke wa US. Wakati huyu anaona ni sawa kuolewa uke-wenza, kwa US hiyo ni kama ukichaa. Hivyo akina Kamala wanapokutumia salamu za pongezi, elewa pia wanakupa rating ya chini.
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa.
Sasa mpaka mwanamke anakua rais wa nchi bado Tena atakua anaendelea kubeba mimba? Kwani mama samia Ana miaka mingapi Hadi aweze kubeba mimba tena
 
Nimesikia leo hii kijana mmoja akilalamikia hizi semi kuwa Rais anahisia za jinsia, duuuu wanawake sijui hata tukoje, itoshe kusema kazi za juuu huku tuwaachie wanaume.
 
Nampenda mama anaongea vizurI ila aache kujidefend sana na kauli za mimi ni mwanamke ninajinsia ya kike kila mtu anajua ni bora awe anasema mimi ni Rais
 
Ukute kuna kidume kimuendesha endesha kwenye maamuzi ya Taifa hivyo anakitangazia hadharani. Hivyo anaona sehemu pekee ya kulalamika ni majukwaani japo imekua too much
UNajionea? Bado hazoei! Ni rais mwanaharakati wa jinsia, ingawa nahisi ni njia ya kuondoa presha ya maisha na ndoa yake.
 
Huyu mama pamoja na yule aliyerithi nafasi yake wote hawakuchaguliwa na wananchi ila walirejeshwa madarakani kwa mtutu wa bunduki hilo liko wazi na ndilo linalomtesa, hayo ya jinsia ni porojo tu.

She doesn't have the lawful mandate, she has a bogus mandate.
 
With this regime, a man is an endangered specie
Very true nikikumbuka siku ya kuapishwa kwa Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa anadai ooh nimeamua kuondoa taboo (miiko) eti wizara hii lazima iongozwe na jitu la miraba minne ...leo nimeteua mwanamke.... yaani it seems wanaume tumemkosea na hatusitahili teuzi?
 
Hata mimi hili jambo jana lilinifikirisha, nikajisemea moyoni inawezekana ndani ya Chama chake au watu walio karibu naye wanazungusha maneno kwamba hataweza kuongoza hii Nchi, nionavyo ndani ya chama kuna kila zana inainuliwa kumponda Mh. Rais, watu wa Jiwe wapo vitani muda wote, hawataki kuamini kwamba sasa keki imevunda wakae kwa kutulia.

Mama akae kwa kujiamini, aunde timu anayoiamini bila shaka yoyote, atoe takataka na chawa wote wa aliyepita, tayari anaye Mabeyo wasiwasi wa nini?
Bila ya Mabeyo wanaume waliomzunguka wangejaribu sana kumnyanyasa. Anawafanya wafunge breki, wawe na heshima.
 
Kuna watu muna uvivu wa kujisomea. Mazoea ya kupewa notisi hadi chuo kikuu. Tafuta hotuba za watu wafuatao walipokuwa ktk nafasi zao za juu:

Specioza Kazibwe wa Uganda
Joyce Banda wa Malawi
Ellen Johnson
Karibu Tanzania.
 
Kuna watu muna uvivu wa kujisomea. Mazoea ya kupewa notisi hadi chuo kikuu. Tafuta hotuba za watu wafuatao walipokuwa ktk nafasi zao za juu:

Specioza Kazibwe wa Uganda
Joyce Banda wa Malawi
Ellen Johnson
Specioza Kazibwe!!?

Hiyo huyu ambaye AU ili- question. ' is Dr. Specioza fit for the top job?!, Na akapigwa chini. JK na yule wa Algeria wakawabwanapigiwa Chapuo, ECoWAS wakajitoa. Mifano mingine kweli inaundermine mlengwa.
 
.... "wengine hatujaumbwa hivyo (kutoa amri)... Mimi natumia kalamu... (kukwambia hufai, kazi imekushinda)...."
 
Back
Top Bottom