Rais wetu na Kiswahili

Tanzania 1

Senior Member
Oct 4, 2007
197
24
Nimefurahiswa na Rais kutukumbusha/kusisitiza kuwa juice kwa Kiswahili ni sharubati, lkn alinishangaza/alinisikitisha pale aliposema "ng'ombe zangu"!! Hiki si Kiswahili sanifu!

Watanzania wengi tunajivunia kwa kuijua lugha ngeni huku tunaipa mgongo lugha yetu. Wengi wanafanya makosa mfano wa lile alilolifanya Rais. Wanasema, kwa mfano:

Ninaondoka nyumbani kumaanisha ninakwenda nyumbani

Wengi, hasa wale ndugu zetu wa kilima Njaro (Maxence upo?!;)), wanatumia "dha dhe dhi dho dhu" kunapopaswa kutumia tha the thi tho thu. Kwa bahati mbaya, hata watangazaji wa vituo vya redio, BBC ikiwemo, wanafanya makosa km haya. Wanasema, kwa mfano:

adhiri badala ya athiri
dhamini badala ya thamini
dhibiti badala ya thibiti

Kadhalika, wengi wanashindwa kutumia "gha ghe ghi gho ghu", na badala yake wanatumia "ga ge gi go gu". Kwa mfano, wanasema:

luga badala ya lugha
gali badala ya ghali
garama badala ya gharama

MAONI: TUIENZI "LUGA" YETU!!
 
Yes, ni muhimu kukumbushana ili watu waone umuhimu.

Sikuwa nafahamu kwamba kuna neno "thibiti" kwenye lugha ya kiswahili. Hebu tengeneza sentensi ukilitumia hilo neno. (Nimekosa mifano kwenye kamusiproject.org )

Wapi umesikia mtu akisema dhibiti badala ya thibiti? (Note that the word dhibiti exist)

.
 
Kuthibitisha na kudhibiti! Kuthibitisha ni kuhakiki beyond reasonable doubts kuhusu jambo fulani. Kudhibiti ni kama kumiliki(kuchukua kitu/mali) kutoka kwa muhusika mwingine. Sio tu mali pia hata hali(kama kuna machafuko n.k). Kuna tofauti kati ya hayo maneno.

Rais wetu pia alikuwa anasema Salathini badala ya thelathini na alirudia sana.
 
Wakati mwingine ukionyeshwa shina la neno pekee unakuwa mgeni wa lugha, Asante. :)

Hata mimi nilimsikia Kikwete akikosea hapo.

.
 
Last edited:
Yes, ni muhimu kukumbushana ili watu waone umuhimu.

Sikuwa nafahamu kwamba kuna neno "thibiti" kwenye lugha ya kiswahili. Hebu tengeneza sentensi ukilitumia hilo neno. (Nimekosa mifano kwenye kamusiproject.org )

Wapi umesikia mtu akisema dhibiti badala ya thibiti? (Note that the word dhibiti exist)

.

Kudhibiti ni kuweka kitu/kumweka mtu ktk himaya. Kwa mfano, askari walimdhibiti mhalifu
Kuthibiti ni kudhihirisha/kudhihirika jambo, km alivyosema Mkuu Mkimbizi hapo juu. Nomino itokanayo na kitenzi hiki (yaani, thibiti) ni thabiti - imara; -enye uhakika/ukweli. Mfano, imethibitika kuwa mafisadi wengi ni viongozi ktk serikali.
Unaweza kunithibitishiaje kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu amefariki?

Nilipotaja thibiti na dhibiti sikuwa nikimzungumzia Rais. Tafadhali rejea maelezo yangu hapo juu.
 
Hao watu wa BBC wanaoharibu sana kiswahili ni wale wasio na asili ya uswahilini. Kuna wengine wameathirika na lafudhi za lugha zao za asili. Lakini cha ajabu ni kuwa hata wale wenye asili nzuri ya kiswahili, huiga makosa hayo ya matamshi!
 
Tunachanganywa wakati mwingine. Mfano, shule tuliambiwa hakuna wingi wa saa. Naanza kuamini kwamba masaa ni kiswahili fasaha.

Kikwete alisema "bati tano"; waalimu kazi mnayo!

.
 
Dah wajamani lugha ni yetu lakini tata mno... Kama kuna mtu ana kamusi ya kiswahili fashaa online ntashukuru akinisogezea kwenye mtandao.
 
Kuthibitisha na kudhibiti! Kuthibitisha ni kuhakiki beyond reasonable doubts kuhusu jambo fulani. Kudhibiti ni kama kumiliki(kuchukua kitu/mali) kutoka kwa muhusika mwingine. Sio tu mali pia hata hali(kama kuna machafuko n.k). Kuna tofauti kati ya hayo maneno.

Rais wetu pia alikuwa anasema Salathini badala ya thelathini na alirudia sana.

Kudhibiti ni ku control.
 
Back
Top Bottom