Tanzania 1
Senior Member
- Oct 4, 2007
- 197
- 25
Nimefurahiswa na Rais kutukumbusha/kusisitiza kuwa juice kwa Kiswahili ni sharubati, lkn alinishangaza/alinisikitisha pale aliposema "ng'ombe zangu"!! Hiki si Kiswahili sanifu!
Watanzania wengi tunajivunia kwa kuijua lugha ngeni huku tunaipa mgongo lugha yetu. Wengi wanafanya makosa mfano wa lile alilolifanya Rais. Wanasema, kwa mfano:
Ninaondoka nyumbani kumaanisha ninakwenda nyumbani
Wengi, hasa wale ndugu zetu wa kilima Njaro (Maxence upo?!
), wanatumia "dha dhe dhi dho dhu" kunapopaswa kutumia tha the thi tho thu. Kwa bahati mbaya, hata watangazaji wa vituo vya redio, BBC ikiwemo, wanafanya makosa km haya. Wanasema, kwa mfano:
adhiri badala ya athiri
dhamini badala ya thamini
dhibiti badala ya thibiti
Kadhalika, wengi wanashindwa kutumia "gha ghe ghi gho ghu", na badala yake wanatumia "ga ge gi go gu". Kwa mfano, wanasema:
luga badala ya lugha
gali badala ya ghali
garama badala ya gharama
MAONI: TUIENZI "LUGA" YETU!!