Ili kuteremusha pesa chini kwa mwananchi wa kawaida, taaaisi kama pride zirudi

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,611
20,936
Nionavyo lengo na dhamira kuu la SSH, ni kuurudisha mzunguko wa kifedha kwa haraka ili hatimaye kila mtu aweze kushiriki vyema katika kujiletea maendeleo yake, taasisi kama Pride ilisaidia sana wakinamama na wafanyabiashara ngazi ya chini katika kujiinua, kwani structure yao ya ukopeshaji na ukusanyaji madeni waliimudu kwa 100%,kitu ambacho hata baadhi ya mabenki kinawashinda.

Nashauri mfumo wa pride na utendaji wake uchukuliwe na NMB ikibidi baadhi ya wataalamu wa pride wachukuliwe ili chombo kingine kidigo kiundwe kitakacho tapakaa kila mahali Tanzania nzima ili kiweze kuwainua upya wafanya biashara ambao wengi walianguka,simaanishi nmb pekee benki yoyote yenye uwezo inaweza kuoganize suala,alimradi tu tutengeneze mzunguko wa kifedha kwa Tanzania yetu, hasa kwa wanyonge,Leo mnyonge kunywa BIA moja inakuwa tabu kweli,sasa tbl atapataje faida.
 
Hakuna kitu kinaitwa kuteremsha pesa chini, tuache haya mawazo na matumaini
Maana akishindwa kufanya hivyo utaanza kumtukana
Pesa haiterememshwi chini Wala kupandishwa juu, bali pesa Ina kanuni zake za kuipata.
Hakuna siku pesa ilikuwepo na hakuna siku haikuwepo.
Fuata kanuni, unaweza kuipata pesa
Katika nchi kama hii ni lazima tukubali wapo tabaka la wachache wenye pesa sana na itaendelea kuwa hivyo.
Pia Kuna tabaka la wengi ambao ni maskini wa kutupwa itabaki kuwa hivyo. Kuziba hili gap sio rahisi hasa kidogo.
Tanzania imekuwa Top 10 ya nchi maskini miaka nenda rudi
 
😂 Ahahahaaaa, pesa wapewe vikoba ili zizagae mtaani, ukiingia ofisini kusign mpaka saa 5 una 100kl baada ya hapo unafikilia kutoka ofisini maana tayari una pesa.

Haya ndiyo yalifanyika kwa Rais fulani huko nyuma, watu wakawa na viburi nk.
Mfumo wa maisha ni kupambana ndipo ule siyo kuletewa mdomoni.
 
Back
Top Bottom