Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nashangaa sana nguvu ya kijeshi ambayo Tanzania inataka kutumia dhidi ya wananchi wasio na silaha katika kuzima kile ambacho ukitafakari sana, ni suala dogo tu la watu kueleza hisia zao juu ya mambo ambayo yanawakera kuhusu haki zao.
Kwa nini Rais awe mkali kiasi hiki, kutishia watu hadi kuonyesha nguvu kubwa za kijeshi? Rais anaogopa nini hasa? Kuna ubaya gani kuacha watu waandamane wakaeleza hisia zao na ukawajibu kistaaarbu tu kwamba malalamiko yako utajaribu kadiri uwezavyo kuyatekeleza?
Nakubali kwamba wakati fulani maandamano ya wananchi hutumiwa na watu wachache katika kufanya uhalifu. Basi ingekuwa busara sana kutumia hao wanajeshi wanaofanya mazoezi kwa ajili ya kuona kuwa maandamano yanafanyika kwa amani pasipo wachache kutumia nafasi hiyo kufanya uhalifu.
Lakini kitendo cha kutishia wananchi wa Tanzania ambao siku zote unasema wewe ni kiongozi wao, na kuwaonyesha nguvu kubwa za kijeshi ili wasieleze malalamiko yao ni ukosefu mkubwa wa busara ya kiuongozi. Ukifanya hivyo siku zote utafanya tatizo liwe kubwa hata zaidi. Ndivyo ilivyokuwa Misri, na hatimaye huko Misri hayo majeshi na bunduki zao zilishindwa dhidi ya nguvu ya wananchi, kwa kuwa walichofanya ni kuwachochea wananchi kwa hasira hata zaidi.
Hainingii akilini kwamba tumefikia mahali ambapo Raisi wa Tanzania anabariki mpambano wa wanajeshi wa JWTZ wenye silaha dhidi ya raia wa Tanzania wasio na silaha! Hivi ukifikia hatua hiyo kweli bado unastahili kuitwa kiongozi wa wananchi, waliokuchagua na wasiokuchagua?
Kiongozi wa nchi yeyote duniani anayetumia majeshi yenye silaha dhidi ya umati wa wananchi wake wasio na silaha, ambao wanachotaka tu ni kujieleza madai yao kwa njia ya amani, basi anakuwa amejiondolea uhalali na ustahiki wa kuitwa kiongozi wa wananchi.
Na pia, kwa jeshi lolote duniani litakalobeba silaha dhidi ya wananchi wa nchi yao wenyewe wasio na silaha, kwa kuwa tu wananchi hao waliamua kueleza dukuduku zao za kimaisha kwa njia ya amani, basi wanajeshi wake wanapaswa wajiulize tena na tena iwapo kiapo chao kilikuwa ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi au viongozi wachache wanajiona mabwana dhidi ya wananchi wanaodai kuwa viongozi wao. Na hususa, siku Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, wakichukua silaha dhidi ya Wananchi wa Tanzania wasio na silaha mikononi mwao, basi likome kuitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na litafute jina jingine ili wananchi wa Tanzania waelewe wazi kwamba jeshi hilo sio kwa ajili yao tena. Kulikuwa na sababu kwa nini jeshi hili tuliliita JWTZ, na sababu hizo bado ni za msingi.