Rais wetu Magufuli, Watanzania tunakuhitaji sana zingatia afya yako

Wewe ni kama nabii uliyeshushwa kwa Nchi ya Tanzania Baada ya Nyerere kuja kuikomboa Tanzania kiuchumi

Nimekuwa nikifatilia unahutubia kati ya saa moja hadi saa moja na nusu kwenye ziara zako za kukagua maendeleo

Ila kwa uzoefu wangu viongozi wengi kwa sasa wanatumia dkk 30 hadi arobani tu kwenye hotuba hili ni swala la kiafya zaidi Rais wetu ,kusimama saa moja na nusu kwa mtu mzima aliyevuka miaka hamsini sio nzuri kiafya.

Najua unawapenda sana Watanzania Lakini naomba upunguze muda wa kuhutubia mawaziri wakusaidie kusema

Kupitia uzushi wa mitandaoni kuna kikundi cha watu walishagonga glas ya mvinyo kujipongeza kuwa Mwamba umeanguka wanaichukua Nchi

Walishaanza kupanga na safu mpya ya uongozi wao,unaweza kuona jinsi ambavyo hawa Wahaini walivyo

Taarifa ile ilizua taharuki sana, Watanzania tulikuombea sana ibada ya jumamosi kina Mama walijifungia kanisani wakimlilia Mungu akuepushe na kila ovu, naamini Mungu aliwasikia na tilifurahi kwa pamoja tulipokuona

Rafiki wangu wengi walizima simu siku tatu kwa jinsi walivopaniki kupitia uzushi uliokuwa ukienea leo ndio wamewasha simu zao baada ya kukuona kwa Tv, unaweza kuona ni kiasi gani inavyopendwa na Watanzania mzee wetu

Kila binadamu ataonja mauti,kwa mapenzi ya Mungu ila sio ya binadamu

Hivyo tunakuomba pata muda mzuri wa kupumzika,Kwasababu tunajua wewe ni mlevi wa kufanya kazi,

Kuna wapinzani walionyesha kufurahia sana hizi taarfa za uzush,wale waliofurahia wajiandae tu kwa kuwa wameanza wao

Tunakuhitaji sana mzee wetu Magufuli tunakuombea maisha marefu na yenye afya katika kuikomboa Tanzania
Naomba ni nikuu maneno yako *"Kila binadamu ataonja mauti,kwa mapenzi ya Mungu ila sio ya binadamu"* Lissu walitaka kumuondoa lakini kwa mapenzi ya Mungu akapona. Hivyo basi tusimamie injili ya kweli isemayo .....kila ambacho hupendi kutendewa usiwatendee wezanko........
 
Watu wanamwelewa na kumkubali JPM tofauti na maneno ya mitandao.
Nchi inamuhitaji JPM kuliko JPM anavyoihitaji nchi
Watu wenye njaa kama wewe, ndio mnaotuletea shida. Unaweza kutumika kufanya lolote bila hata kutafakari, kwa sababu ya njaa yako tu.
 
Hata mimi na wewe siku ukifa kuna watu watafurahi. Hata Yesu Kristo na mitume wengine walipokufa watu fulani walifurahi. Hakuna jipya.

Queen Esther
Wewe na mimi ni ma raisi? Kwa kiongozi mkubwa wa nchi, ile picha aliyoipata haileti afya.
 
Andika point acha majungu
Naomba ni nikuu maneno yako *"Kila binadamu ataonja mauti,kwa mapenzi ya Mungu ila sio ya binadamu"* Lissu walitaka kumuondoa lakini kwa mapenzi ya Mungu akapona. Hivyo basi tusimamie injili ya kweli isemayo .....kila ambacho hupendi kutendewa usiwatendee wezanko........
 
Iwapo ataendelea kuweka pamba masikioni kwake, akae akijua SIKU YA KIFO CHAKE kuna baadhi ya watanzania watakesha wakila "bia" na nyama choma. Mwambieni Mungu FUNDI.
Robart wewe unakijua kifo chako ni lini atakuongoza tu huu mpk 2025
 
Mpaka sasa sielewi kilichotokea!! Jumapili nilishangazwa na body languange ya wote walokuwamo ndani ya ikulu!! Je ni kweli alipata tatizo kidogo au ulikuwa ni uzushi tu!!????
Natamani nipate hali halisi P hata kwa code shusha nondo!!!
 
Back
Top Bottom