unprejudiced
JF-Expert Member
- Jan 27, 2017
- 3,505
- 2,862
Kwa mawazo yangu naona rais anazindua vitu vidogo vidogo sana kulingana na hadhi na heshima ya urais. Kwanza kwani lazima kinachojengwa kizinduliwe? Kuzindua kunasaidia nini?. Ningeelewa kama rais anafungua reli au mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge lakini kufungua tawi la Benki ya CRDB, Nyumba za familia 12 za polisi, ukuta wa Mererani, barabara ya Bukombe kuifungua tena(ilishafunguliwa na kutumika enzi za Kikwete), Kiwanda cha vinywaji cha Sonoma, prince pharmaceutical, kiwanda cha Alizeti, Singida(Hiki kilifungwa kwa kufanya makosa tangu 2012), nyumba za NHC Iyumbu Dodoma nk siyo muhimu rais afungue.......Kwani kazi za mawaziri au wakuu wa wilaya na mikoa ni nini? Je ni kwa vile huyu rais hasafiri sana nje hivyo anataka kupata per-diem? Au anataka aonekane ni yeye ni jack of all trade, ajenge publicity?
Kitendo cha wananchi kutoka sehemu mbalimbali kukusanywa na daladala kupelekwa airport ili wakamshangilie rais wakati anapokea ndege moja halafu baadaye wanapandishwa ndege kwa level seat ya watu 72 halafu wanashushwa wapandishwe wengine tena washushwe hadi kila mtu awe amepanda naona kama tunajichora na tunaonekana bado tunaishi gizani na kuabudu vitu vidogo vidogo. SASA WATU WANAPANDISHWA KWENYE NDEGE HALAFU WANASHUSHWA ILI WENGINE WAPANDISHWE ILI IWEJE....MBONA SIJAONA WALA KUSIKIA UTARATIBU KAMA HUU SEHEMU NYINGINE DUNIANI?? Sijajua nia yake.
China imenunua ndege 300 kutoka Boeing zimeletwa kwa awamu, sijamuona Xi Jianping akiwa airport akizipokea.....Sisi ATCL ikinunua ndege 25 rais atakwenda uwanjani mara 25? Kwanini rais hawezi ku-delegate kwa mawaziri aliowachagua? Kila kitu hata kiwe kidogo anakimbilia kufanya yeye? Yeye ni rais wa nchi vitu vingine ni vidogo mno kukimbizana kwa level yake, awaachie aliowachagua....akizindua miradi mikubwa mikubwa naweza kumuelewa japo si muhimu.
Kuzindua, kufungua au sijui kuweka jiwe la msingi ni formality tu, ni nchi chache zinafanya hivyo. Ni mawazo yangu, naomba wakereketwa msinitukane nielimishwe tu kama ni muhimu kwa nchi yetu miradi midogo midogo kufunguliwa na rais. Asanteni kwa kunisoma
Kamatia JPM. Inaonekana umepatia panapouma. Minya. Bonyeza. Wape Dawa. Kimya kimya. Hawana mada wala hoja. Wanajitekenya. Wanacheka. Ushauri. Tuambieni Sera zenu jamani. JPM tunajua anafanya nini. Someni ILANI yao. BADALA YA KUONA KUWA ZAMANI ILIKUWA MANENO. SASA MANENO THEN ACTION. WE UNAONA UJINGA WAKO. HAPO TO UKIAMBIWA MJINGA UTASEMA UNAONEWA. UNAONA MBELE YA PUA YAKO TU. Issue hapa ni „YAMETIMIA“ kweli hapa kazi tu. Lakini we umeona Ngoja uaadvertise your stupidity and enviousness.