Rais wetu anazindua ukuta wa Mirerani, Kazi za mawaziri ni nini? Kwani kuzindua ni lazima?

Kwa mawazo yangu naona rais anazindua vitu vidogo vidogo sana kulingana na hadhi na heshima ya urais. Kwanza kwani lazima kinachojengwa kizinduliwe? Kuzindua kunasaidia nini?.

Ningeelewa kama rais anafungua reli au mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge lakini kufungua tawi la Benki ya CRDB, Nyumba za familia 12 za polisi, ukuta wa Mererani, barabara ya Bukombe kuifungua tena(ilishafunguliwa na kutumika enzi za Kikwete), Kiwanda cha vinywaji cha Sonoma, prince pharmaceutical, kiwanda cha Alizeti, Singida(Hiki kilifungwa kwa kufanya makosa tangu 2012), nyumba za NHC Iyumbu Dodoma nk siyo muhimu rais afungue.

Kwani kazi za mawaziri au wakuu wa wilaya na mikoa ni nini? Je ni kwa vile huyu rais hasafiri sana nje hivyo anataka kupata per-diem? Au anataka aonekane ni yeye ni jack of all trade, ajenge publicity?

Kitendo cha wananchi kutoka sehemu mbalimbali kukusanywa na daladala kupelekwa airport ili wakamshangilie rais wakati anapokea ndege moja halafu baadaye wanapandishwa ndege kwa level seat ya watu 72 halafu wanashushwa wapandishwe wengine tena washushwe hadi kila mtu awe amepanda naona kama tunajichora na tunaonekana bado tunaishi gizani na kuabudu vitu vidogo vidogo.

SASA WATU WANAPANDISHWA KWENYE NDEGE HALAFU WANASHUSHWA ILI WENGINE WAPANDISHWE ILI IWEJE....MBONA SIJAONA WALA KUSIKIA UTARATIBU KAMA HUU SEHEMU NYINGINE DUNIANI??

Sijajua nia yake.
China imenunua ndege 300 kutoka Boeing zimeletwa kwa awamu, sijamuona Xi Jianping akiwa airport akizipokea.

Sisi ATCL ikinunua ndege 25 rais atakwenda uwanjani mara 25? Kwanini rais hawezi ku-delegate kwa mawaziri aliowachagua? Kila kitu hata kiwe kidogo anakimbilia kufanya yeye?

Yeye ni rais wa nchi vitu vingine ni vidogo mno kukimbizana kwa level yake, awaachie aliowachagua akizindua miradi mikubwa mikubwa naweza kumuelewa japo si muhimu.

Kuzindua, kufungua au sijui kuweka jiwe la msingi ni formality tu, ni nchi chache zinafanya hivyo.

Ni mawazo yangu, naomba wakereketwa msinitukane nielimishwe tu kama ni muhimu kwa nchi yetu miradi midogo midogo kufunguliwa na rais.

Asanteni kwa kunisoma

Siku anaagiza ukuta ujengwe mbona hukuja hapa kuuliza mawaziri wako wapi? Watu hamkosi cha kukosoa.
 
Kumbuka mikoa ya kanda ya ziwa ilikuwa imesahaulika kwa miongo mingi,ndio maana wananchi wa kanda hii walimpigia kura kwa wingi.
Kakudanganya nani huko ndiko walikompa kura nyingi. Ungesema huko ndiko alikoiba kura nyingi ungeeleweka zaidi. Pia hakuna mkoa uliosahaulika ila watu wa mikoa hiyo walijisahau.. ww unazani Maendeleo ya kaskazinin yaliletwa na serikali. Watu walijitambua mapema wakachangamkia fursa wakaboresha kwako. na hadi Leo wanaendeleza kwako. Mfano tu: Mchaga hawezi jenga mjini kabla hajajenga kwao. Kwa hyo maendeleo ni tabia ya mtu kama ilivyo usafi. Kama huna tabia hyo hata uletewe nn havitadumu...watu watarudi square one.
 
Unagemjua aliyeagiza kujengwa ukuta huo ili kuzuia utoroshaji wa madini wala usingeuliza.
We mjanjaaa umemtetea Jpm kwa kijanja .aliagiza yy Na mengi Ni yy swali lazima vyote afungue yy wasaidizi wake VP.
Gharama ya yy kwenda Ni kubwa kuliko wasaidizi tena w mikoa husika.
Fanya research
 
Hivi unaamini kabisa hiyo ndiyo njia sahihu kabisa ya kuzuia wizi wa madini? Unamjengea binadamu ukuta, amekuwa ngombe? Atashindwa kuruka huo ukuta? Hata hivyo wizi wa madini haufanyiki hivyo. Wizi unafanyika kwa njia ya collusion.na wagusika mbalimbali. Madini bado yataibwa tena kwa kupitia getini. We' ve got to be serious!
Bado unaota wewe,zinduka dada!
Humo ndani kuna mabenki,Tra,wakala wa jiolojia
Getini kutakua na scanner za hali ya juu,achana na fikra hasi na mawazo mgando kuwa hatuwezi kudhibiti madini yetu
 
mleta uzi hajauliza aliyeagiza ukuta ujengwe! kauliza kama kuna ulazima kwa raisi kwenda kuzindua zindua kila kitu hata kidogo. raisi kujenga ukuta sio jambo geni . trump amefanya wala sio kwamba yye ni .zalendo kuliko wote. ni kwamba anatimiza majukumu yake kama raisi.sasa unataka tujue aliyeagiza ukuta kujengwa huko arusha ili?
Na unafuatilia maisha ya JPM yanakuhusu nini?
Kiherehere muwe mnawapelekea waume zenu
 
Kwa mawazo yangu naona rais anazindua vitu vidogo vidogo sana kulingana na hadhi na heshima ya urais. Kwanza kwani lazima kinachojengwa kizinduliwe? Kuzindua kunasaidia nini?.

Ningeelewa kama rais anafungua reli au mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge lakini kufungua tawi la Benki ya CRDB, Nyumba za familia 12 za polisi, ukuta wa Mererani, barabara ya Bukombe kuifungua tena(ilishafunguliwa na kutumika enzi za Kikwete), Kiwanda cha vinywaji cha Sonoma, prince pharmaceutical, kiwanda cha Alizeti, Singida(Hiki kilifungwa kwa kufanya makosa tangu 2012), nyumba za NHC Iyumbu Dodoma nk siyo muhimu rais afungue.

Kwani kazi za mawaziri au wakuu wa wilaya na mikoa ni nini? Je ni kwa vile huyu rais hasafiri sana nje hivyo anataka kupata per-diem? Au anataka aonekane ni yeye ni jack of all trade, ajenge publicity?

Kitendo cha wananchi kutoka sehemu mbalimbali kukusanywa na daladala kupelekwa airport ili wakamshangilie rais wakati anapokea ndege moja halafu baadaye wanapandishwa ndege kwa level seat ya watu 72 halafu wanashushwa wapandishwe wengine tena washushwe hadi kila mtu awe amepanda naona kama tunajichora na tunaonekana bado tunaishi gizani na kuabudu vitu vidogo vidogo.

SASA WATU WANAPANDISHWA KWENYE NDEGE HALAFU WANASHUSHWA ILI WENGINE WAPANDISHWE ILI IWEJE....MBONA SIJAONA WALA KUSIKIA UTARATIBU KAMA HUU SEHEMU NYINGINE DUNIANI??

Sijajua nia yake.
China imenunua ndege 300 kutoka Boeing zimeletwa kwa awamu, sijamuona Xi Jianping akiwa airport akizipokea.

Sisi ATCL ikinunua ndege 25 rais atakwenda uwanjani mara 25? Kwanini rais hawezi ku-delegate kwa mawaziri aliowachagua? Kila kitu hata kiwe kidogo anakimbilia kufanya yeye?

Yeye ni rais wa nchi vitu vingine ni vidogo mno kukimbizana kwa level yake, awaachie aliowachagua akizindua miradi mikubwa mikubwa naweza kumuelewa japo si muhimu.

Kuzindua, kufungua au sijui kuweka jiwe la msingi ni formality tu, ni nchi chache zinafanya hivyo.

Ni mawazo yangu, naomba wakereketwa msinitukane nielimishwe tu kama ni muhimu kwa nchi yetu miradi midogo midogo kufunguliwa na rais.

Asanteni kwa kunisoma
Kuzindua ni lazima, ndege tunazindua, ukuta tunazindua, ilani tunazindua, everything!!
 
Ameamua kuwa hizo ndo kazi zake lakini hilo sio lengo bali hapa ni yupo kwenye kampeni zake binafsi za Urais na Chama pia....anajihami..
 
Ungeijua thamani ya huo ukuta kwa nchi yako wala usingediliki kuyasema haya ila kwasababu hamna kitu wala hatutakushangaa
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom