Rais wetu anashauriwa na akina nani?

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Ukweli Rais Magufuli Watanzania wengi walikuwa na imani nae awali ukiacha watumishi wa serikali kama Mimi.Niliposikia kwenye Vyombo vya habari kuwa CCM kimempitisha Magufuli kupeperusha bendera ili niuma sana.

Sio kwamba sikupenda CHAMA hapana MTU mwenyewe, Magufuli ni mtendaji mzuri ila tatizo lake hapimi kwanza kauli zake na maamuzi yake kabla hajachukua maamuzi. Sijui washauri wake wanamuogopa kumumbia au hashauriki.

1.USAWA WA DINI
Mimi ni mkristo tena naitwa Thomas, lakini teuzi nyingi zimeegemea upande mmoja wa dini ambao ni wakristo, angalieni majina japo majina si kigezo kizuri lakini kuna uhusiano wa jina la MTU na dini yake anzeni na Mawaziri, Manaibu, Wakuu wa Mikoa, Ma katibu tawala wa Mikoa, Wilaya, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa taasisi na mashirika ya umma aliyoteua vyote vina mlengo huo.

2. Kuteu mkuu wa Wilaya hewa
Yeye ndie kioo cha jamii, kitendo cha kuteua mkuu wa Wilaya ki makosa akaingie hadi Ikulu kinadharirisha taasisi ya urais, Pia kuna WAZIRI wake mmoja anaehusika na Bunge, wazee na walemavu aliteua CEO hewa,ambapo alikuja kuonekana sio RAIA wa Tanzania akatenguliwa.

3.Wanafunzi wa Diploma Maalumu wa UDOM
Haijarishi walipelekwa kusoma shahada wala Sta Shahada, busara zingetumika hawa kujichagua, serikali ilipaswa kueasomesha kisha baadae wakapangiwa kufundisha SHULE za msingi na wote wakapewa ngazi ya staa shahada sio kuwafukuza chuo.

4.Uteuzi wa Makatibu tawala wa Wilaya na Mikoa

Rais amepotoshwa au amejipotosha mwenyewe, hawa ni watalaamu hatutafuti kamati ya kampeni za uchaguzi. Kuwa weka wafurukutwa wa vyama, walioshindwa chaguzi kupitia CCM kuwa na DAS siyo sahihi mheshimiwa, Hata kwenye chaguzi kuna wasimamizi wa akiba, ungewaweka akiba kama nafasi wa kisiasa zilikuishia, ili akiboronga MTU kwenye U DC au U RC unamuweka kada pale.

Ninamengi ya kukueleza ila kwa Leo naomba niishie hapa, najua katiba inakupa fursa ya kuchagua washauri MPE MTU unae muamini akuchagulie washauri makini hawa ulio nao kama unafanyia kazi ushauri wao wanakupotosha. Nisamehe Rais wangu na watanzania wenzangu kwa ujumla kama kusema ya moyoni nimemkwaza mtu
 
Kiongozi kuwa na 'washauri'
kiongozi kuwa na 'washauri sahihi'
kiongozi kuwasikiliza 'washauri wake'

Vitu hivyo vitatu ni tofauti saana
 
Yuko Baraza la Idd, mpigie simu
 
Magufuli akae chini afikirie jinsi anavyorun serkali yake
Bado ana muda wakujirekebisha

Udicteta si mahali pake Tanzania
 
Kiongozi kuwa na 'washauri'
kiongozi kuwa na 'washauri sahihi'
kiongozi kuwasikiliza 'washauri wake'

Vitu hivyo vitatu ni tofauti saana

Kuna Washauri ambao bosi akicheka na wao wanacheka.

Kuna Washauri ambao bosi akinuna na wao wananuna zaidi ya bosi.

Nahisi hawa ndio waliomzunguka.
 
Mwisho wa siku kiongozi ndiye anayelaumiwa au kupongezwa kwa mwisho wa uongozi wake. Napenda style yake whether anashauriwa au la. Yeye ndiye atatoa hesabu hivyo aendelee anayoona inafaaa.
 
Hoja zako zina mashiko lakini hiyo namba moja ibabidi uifafanue kiundani zaidi ili na yenyewe niione ina mashiko pia!!
 
Hapo namba 3 wale wa udom naona wametajwa tena hapa kwenye hii siredi. Chuo kudahili wanafuzi karibia 8000 kwa kozi moja. Kwa raslimali hizi za kuungaunga, hapa kuna namna.
 
alipoteua mawaziri wote tulishuhudia njinsi walivyokuwa wanakimbizana kwa kurupuka, wengine kufunga mageti, wengine kukagua makaravati, wengine kubeba mabox muhimbili, wengine kumfungia Dr Mwaka nk, kuna watu rais akiteleza akaanguka nao watafuatisha, yaani ni full kumuogopa. inshort, rais ndo anawashauri washauri wake
 
Back
Top Bottom