Rais wetu anakera, iweje uwalipe uliowaita majambazi fedha zetu za kodi?

Mleta mada ni mtoto mdogo wa juzi juzi huelewi mambo haya yalitokeaje na wala si kosa lao hao unaowaita wenye vyeti feki.

Hebu fikiria mtu ametumikia taifa maisha yake yote leo amekaribia kustaafu ndiyo ulete ngonjera ya vyeti feki ?!. Watu wamebakiza miezi, mwaka au hata miaka miwili, mitano ndiyo adhulumiwe ?! Ni mfumo ulioleteleza hali hii na pia huko fair kwani wana siasa na wanajeshi hajashirikishwa.
Mwizi ni mwizi, kutumikia taifa kwa kwa muda mrefu kwa njia isiyo sahihi haiwezi kuhalalisha kosa.....

Hapo kama wameona siyo kosa lao basi wawaache waendelee na kazi.
 
Wapewe mafao yao sababu walipiga kazi
Hata mwizi ukimkuta amevunja mlango wa nyumba yako ambao uliuacha umeufunga umlipe maana amevuja jasho na kutumia akili kubwa kuuvunja.

Majambazi nao walipwe kwa kazi kubwa wanaoifanya kuteka mabasi na magari njiani maana siyo kazi rahisi
 
Back
Top Bottom