Rais wetu anakera, iweje uwalipe uliowaita majambazi fedha zetu za kodi?

Rais alisema watu wenye vyeti feki ni sawa na majambazi wanaiibia serikali.
Kwanza wamefoji vyeti, pili wamezuia ajira kwa wenye vyeti halali, tatu wameiba fedha zetu wananchi(kodi)

Ulijipambanua kutumbua majipu na wezi wa Mali ya umma.

Umewapa msamaha majambazi wa fedha zetu waondoke ifikapo 15/5 iweje uwalipe mafao wezi.

Haiwezekani, haiwezekani, haiwezakani.

Rais zuia fedha zetu[/cilor] kulipa wezi na majambazi.

Tunakekera tena sana.

Waziri aliyesema anawaandalia mafao mtumbue mapema akapumzike.


Wewe toa hizo zako kama hutaki.
 
Huyo mwenyecheti feki ndiye aliye kufundisha nasasa hivi we we ni daktari halafu unaleta ufukunyuku! Mimi mwalimu wangu ameondolewa lakini ndiye aliyenisaidia sasa hivi Nina phd lakini alinisaidia sana secondary

Mnawakumbuka Waalimu wa UPE(Universal Primary Education)?Waliokuja kuwa Waalimu maarufu kwa jina la(Ualimu Pasipo Elimu~UPE)?
Walijiendeleza kutoka elimu yao ya Misingi kwa evening classes wakafikia mpaka ngazi ya degrees!
Ni ujinga sana kufikiri kwamba kama huna cheti ya O na A level basi we hustahili kufanya kazi!!!
 
Unapoambiwa lete vyeti vyako halali ukileta feki ujue unafanya makosa. Haijalishi itachukua mud a gani ila utakapogundulika lazima ulipe gharama.

JAYJAY,
Na wewe unayekagua vyeti unatakiwa uhakikishe kuwa unayemwajiri ana vyeti HALALI kama utashindwa kung'amua kuwa ni FEKI basi na wewe kama Afisa Utumishi au Menejimenti pia ni FEKI!
Lazima tuangalia panda zote 2 aliyeleta vyeti vya kughushi na huyu aliyekubali kupokea vyeti vya kughushi!!!Shilingi ina pande 2 bro!
 
Ukweli ni kwamba hawa tunaowaona ni wezi ndo wametufundisha kusoma na kuandika mpaka leo tunaheshimika kwenye jamii, hawa hawa ndo wamewasaidia watoto wetu na wazazi wetu na hata sisi kutuchoma sindano wakati tunaumwa tuko hoi na kutufanya kujisikia haueni. Alafu mtu unataka wadhulumiwe. Kama serikali iliwaajiri ilihali ikijua wana vyeti feki nayo ilichemka. Mimi nampongeza sana raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kuwalipa stahiki zao. Mungu ambariki sana.
 
siku zote halisimamii neno lake. ukitaka kuamini angalia hapa
c90ad6211bb5aac960fa03e7e7b90e01.jpg
 
DAIMOND AMEIMBA, KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI.
KAMA SERIKANI ILIAJIRI WATUMISHI WENYE VYETI VYA KUGUSHI NI AIBU KWA SERIKALI, IMECHAPWA.
INATAKIWA KUMALIZANA NA WAAJIRIWA KIMIYA KIMIYA.
KIMSINGI, KATI YA MWAJIRIWA NA MWAJIRI MWENYE TUHUMA KUBWA NI MWAJIRI. HUYU TUMUULIZE ALIPEWA NINI MPAKA AKAAJIRI MTU MWENYE CHETI CHA KUGUSHI. SASA MTUHUMIWA NAMBA MOJA AMBAYE NI SERIKALI INATOA ADHABU KWENYE KOSA AMBALO YENYEWE ILISHIRIKI.
SERIKALI IWALIPE WATUMISHI WOTE WENYE VYETI VYA KUGUSHI NA IACHANE NAO KWA USALAMA.
 
Huyu hajielewi kabisa tena hawa waliofoji ndo wenye uwezo kuzidi wenye vyeti halali..
Kweli, wanastahili kupewa stahiki za jasho lao. Kuna waliokuwa wamebakiza muda mchache kustafu wapewe tu.

Take note. Hao waliotolewa kwenye system wengi wao walikuwa wanafanya kazi vizuri pengine kuliko hata walio na vyetu halali.
 
Rais alisema watu wenye vyeti feki ni sawa na majambazi wanaiibia serikali.
Kwanza wamefoji vyeti, pili wamezuia ajira kwa wenye vyeti halali, tatu wameiba fedha zetu wananchi(kodi)

Ulijipambanua kutumbua majipu na wezi wa Mali ya umma.

Umewapa msamaha majambazi wa fedha zetu waondoke ifikapo 15/5 iweje uwalipe mafao wezi.

Haiwezekani, haiwezekani, haiwezakani.

Rais zuia fedha zetu kulipa wezi na majambazi.

Tunakekera tena sana.

Waziri aliyesema anawaandalia mafao mtumbue mapema akapumzike.
Hta km ni wezi c walikua wanatumikia taifa lao, mfano walimu c ndo hao walio kufundisha ww ukapata cheti original, dactari c ndo alokutibu ww ukaeza kupata nguvu na km kwa miaka yote walkua wanatmikia Taifa n kwa nn wacpewe mafao? RUDI KAFIKIRIE TENA NDIPO UJE TNA
 
swali jepesi ni hili:
kwa mujibu wa rais Magufuli wenye vyeti feki ni majambazi. JE,JAMBAZI ANALIPWA MAFAO?
 
Binafsi nimemuheshimu sana muheshimiwa.. Ametambua kuwa pamoja na mapungufu mengine walitumikia nchi pia.. Na pengine walifanya kazi kwa juhudi kuogopa kupoteza kazi.. So binafsi sijaona kisa kama ni hela inatafutwa na inapatikana ubinadamu kwanza.
 
Muuleweni mtoa mada,anasema huko nyuma hawakuonekana kama watumikia umma bali walikuwa wezi,wakiuibia umma kwa maana ya kuchukua mshahara wasio sitahili kwa sababu wana vyeti feki,sasa huo utumishi wao umeanza lini? Na kama tunakiri ni watumishi halali wanaostahili malipo halali why waondolewe kazini?
Ipo hivi? Kwanza mtoa mada yaweza kuwa na umri under 30. Haelewi mambo mengi ya huko nyuma.
Miaka ya 70 baada ya mahitaji ya elimu na idadi ya wahitaji kuongezeka, waliajiriwa waalimu wa U P E wenye elimu ya kiwango cha chini ya ufaulu wa std7, ambao walifeli kuendelea na elimu ya sekondari.
Pia ilipigwa marufuku kurudia darasa la7.
Usipochaguliwa, hauruhusiwi kukariri darasa, ndiyo inakuwa umeishafika mwisho wako kielimu.
Hapo ndiyo figisu za kutumia majina ya watu wengine kurudia masomo zilipoanzia.
Watu walitumia majina ya watoro kujiendelezea, hilo linafahamika sana. Ni mfumo ndiyo uliolitengeneza janga hilo.
Hakuna mtu anayependa kulikana jina lake kwa sababu nyepesi.
Mambo hayo yameendelezwa nadhani hadi leo, sidhani kama mtoto wa shule ya msingi anaruhusiwa kukariri afelipo mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Akitaka kurudia hadi abadili utambulisho.
Haya ninayoyasema yametumiwa na watu wengi sana hapa nchini na katika zoezi hili wengi hawakuguswa kwa sababu hayo majina waliyahuisha kutokea "chini". Dhambi hii ni ya kitaifa.
Udhaifu huo ulifanya hata wasiosoma kabisa wachonge vyeti.
Lakini kuanzia kama sikosei 2013, wizara ya elimu wameanza uthabiti wa kuweka picha kwenye vyeti vya elimu ya sekondari. Pia kuna sensa imefanyika shule za msingi kuhakiki majina ya wanafunzi na kuyaingiza kwenye "system", huo ni mwanzo mzuri.
Sasa tukija kwenye suala zima la hawa watumishi wa umma waliokumbwa na kadhia hii ni kwamba, siyo wezi kwa sababu waligushi majina. Kughushi nyaraka ni kosa jingine na kutumikia ajira ni ishu nyingine.
Sasa wamestaafishwa, wamefukuzwa ama aina yoyote ya tafsiri ya namna walivyoachishwa, lakini wanastahili mafao yao, ambayo ni tangia kuajiriwa hadi siku wanasimamishwa kazi.
Kumfukuza mfanyakazi, hakumpatii mwajiri haki za kumpora mfanyakazi mafao yake.
Kosa halilipwi kwa kosa, bali kosa hulipwa kwa adhabu.
Kunyang'anywa mafao ni sawa na adhabu tuisikiayo ya jicho kwa jicho. Haifai kwa dunia ya wastaarabu na wapenda haki.
Kwa muktadha huu, mnyororo wa kadhia hii ya wafanyakazi ni mrefu, ikiwemo serikali yenyewe. Kwa sababu, kabla ya uajiri kuna uhakiki. Ilikuwaje wakaajiriwa kwa nyaraka ghushi?
Sheria ni msumeno ikate kotekote.
Mambo haya yanatakiwa yamalizwe kwa hekima kama wengine wanavyosema, kwa sababu jambo hili ni la kitaifa, si la hao wachache tu walioguswa na kufanywa kondoo wa kafara.
 
mkuu wakilipwa ni kosa.

km yupo kiongozi hakuwatambua ashitakiwe.

mbn waliojenga lembeni ya reli miaka mingi ilopita hawajalipwa cos reli ilishapima wao wakaamua,miaka mingi reli hawakua Na hela sasa wamept hela mbn wanabomoa bila fidia cos waliovamia HT km imepita 30yrs.

wao walipaswa kushtakiwa Na viongozi wote walioruhusu kuendelea kuiba
After all cheti cha form four kina tija gani?
Unamfukuza Dr amesoma Russia 7yrs kisa tu katumia cheti cha form four kwenda form five Minaki. Kapiga two safi PCB .Kaaply chuo, kachaguliwa. Kasoma kafaulu.
Leo unasema kihiyo .Cheti cha form four. Aibu Tz
 
Rais alisema watu wenye vyeti feki ni sawa na majambazi wanaiibia serikali.
Kwanza wamefoji vyeti, pili wamezuia ajira kwa wenye vyeti halali, tatu wameiba fedha zetu wananchi(kodi)

Ulijipambanua kutumbua majipu na wezi wa Mali ya umma.

Umewapa msamaha majambazi wa fedha zetu waondoke ifikapo 15/5 iweje uwalipe mafao wezi.

Haiwezekani, haiwezekani, haiwezakani.

Rais zuia fedha zetu kulipa wezi na majambazi.

Tunakekera tena sana.

Waziri aliyesema anawaandalia mafao mtumbue mapema akapumzike.
Wewe MTOTO wa jana Tu huijui hii NGOMA....tuma application upate KAZI...
 
kuna watu wamekosa ajira kwavmda mrefu ilihali MTU kaiba cheti kajipachika.
wewe unaona jambazi ni Yule anaekuibia simu au hela zako tu
si alikuwa anafanya kazi, ww nafikiri hao wenye vyeti feki wasingekuwepo watu wote wangepata ajira ?
 
Back
Top Bottom