Rais, Waziri, Mbunge na Diwani. Nlipewa Rushwa nikakataa.

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,266
2,870
Huu utaratibu mpya wa mtu kupewa Rushwa akakataa na hataki kumtaja au kuwataja waliompa Rushwa ni wa ajabu sana. Naona unaanza kuota mizizi hapa nchini. Week iliyopita kuna waziri naye alisema aliwah kupewa Rushwa akakataa. Mbaya zaidi hakutaja waliotaka kumpa rushwa washughulikiwe. Cha kusikitisha zaidi vyombo vya Dola havikutaka kwenda kumhoji juu ya jambo hilo. Likaishia kuandikwa magazetini na waziri huyo kupongezwa sana. Lakini najiuliza huu utaratibu mbona umeota mizizi sana hapa nchini. Kuna Rais alishawah kuwa na majina ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi/mafisadi akakaa nayo tu mfukon. Kuna Rais ashawah pewa majina ya Majangiri, wauza unga akakaa nayo tu nyumbani kwake.Kuna siku Tanzania Rais atasema kuna mtu aliwah kumpa Rushwa akakataa au akachukua kidogo nyingne akamrudishia. Haya mambo tutegemee siku moja. Sheria inasema anayetoa au kupokea Rushwa anatenda kosa. Sasa wewe unayeletewa Rushwa ukaishia kukataa tu pasipo kumwadabisha mhusika unadhan ni jambo la kutangaza? Si ni bora ungenyamaza tu? Waswas wangu huu ni mkakati wa watu kadhaa pia kujijenga kisiasa ingawa kwa walio na akili wanakuwa na maswali mengi zaidi kuhusu jambo hili. Kwa nini hawa watoa Rushwa hawakamatwi? Ni afrika au Tanzania wauza madawa,majangiri,watoa rushwa na mafisadi wana nguvu kuliko Serikali au wananch. Je inawezekana kabisa mzazi akamsikia mtoto wake alisema ilikuwa kidogo abakwe akaponea chupuchupu bila kuuliza nani alitaka kukubaka na wapi? Please msisahau kuwa sisi ni watu wazima acheni ku tutreat kama watoto.
 
Back
Top Bottom