Rais wangu unaelezwa ukweli na wasaidizi wako? Kikulacho kinguoni mwako

engijape

Senior Member
Nov 8, 2014
178
97
Wanajukwaa!!

Poleni na majukumu ya hapa na pale. Najaribu kutafakari sana huyu Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli na kujikuta nina kigugumizi. Kwanini? Asilimia 100 ya watanzania mwaka 2015, walifurahishwa sana na Mhe Rais kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata mimi nilifurahi sana kwa kweli. Nilipata matumaini mema kwa taifa langu lililokuwa limejawa na kundi dogo lililojaa ufisadi na roho mbaya dhidi ya mali za uma.

Pamoja na furaha mpaka ya wapinzani wake, hali imebadilika ghafla. watu wanaongea tofauti kabisa na matumaini mazuri tuliyokuwa nayo juu ya Rais wetu ambaye alivunja historia ya utendaji uliyotukuka katika nyasifa zote alizowahi kuzishika akiwa waziri. Utendaji wake huo ulimfanya kuwa maarufu mpaka kujulikanan hadi na watoto kwa utendaji wake.

Swali!! Rais anajua kinachoendelea Tanzania? Rais anapataje kujua taarifa mbalimbali za watu wake?

Kwangu mimi hili linanipa shida kwa sababu si kila kitu Rais anaweza kuelewa hasa ukizingatia ana mambo mengi zaidi juu ya taifa letu. Nafahamu pia ana watendaji wake wakubwa aliowaamini, je wanamsaidia Rais taarifa zilizo sahihi? Ni watendaji au wapiga dili, na je uoga walionao kwa Mh Rais ni uoga wa kufanya kazi au kumdanganya na kunyanyasa maskini pamoja na kuendelea kuiba huku wakisema HAPA KAZI TU!!

Mimi ni mtanzania huru katika nchi huru, Rais wangu, watu wako wana nia njema kama wewe? Kama ndio, na kama wanakupatia taarifa sahihi, basi sitaenda mbali sana kuhusiana na hilo. Napenda tu nikukumbushe kuwa wewe Rais uliaminiwa sana na sisi watanzania, ikiwepo mimi niliyekupigia kura kwa ujasiri bila haya. Utukumbuke na kutukumbuka kwako, ni kutujali maskini tunaohitaji matumizi sahihi ya rasilimali za nchi yetu. Watanzania wananyanyaswa sana na watendaji wa chini kwa kigezo cha utendaji uliotukuka. Wasikufanye haujawahi kuwa mtanznia wa chini. Umekuwa tena kutoka familia maskini. CWT ni mfano tu wa watu wanaendelea kunyonya damu za watanzania maskini sana na wenye kipato cha chini. Nikihitaja CWT unawafahamu vilivyo.

Mh Rais, leo hii nikitaka kufungua biashara 1,000,000/= ninashindwa. hii ni kwa sababu mahesabu ya kodi yamekuwa makubwa, hatujui wala hatuna wa kumlilia zaidi ya wewe Rais, tukimbilie wapi??

Mhe Rais, kauli yako ya nchi ya viwanda naikubali na inawezekana , Je, si ni vyema kama nchi tukashikana bila kujali huyu ni chadema, huyu ni cuf na huyu ni TLP? wew kabla ya kuwa Rais ulionanje nchi yetu? kweli tatizo lilikuwa vyama? hapana. Tatizo lilikuwa uwizi wa rasilimali za watanznia na nidhamu makazini. Usichonganishwe na vyama vya upinzani kwa sababu muda umekwisha wa miaka mitano, na karibia uchaguzi mwingine unafika viwanda halisi viko wapi? mbali na zile za watu kusema ukiwa na brenda kumi za kutengeza juice ni kiwanda. Huoni hawa wanaosema hivi hawakusaidii?

Tunahitaji viwanda halisi vinavyoweza kuingizia nchi kipato na kuboresha maisha ya mtanzania mmoja mmoja. Usidanganywe Mh Rais, wakati umekwisha kabisa. waache hawa wanasiasa sasa na upige kazi. ikitokea yupo kweli anayeleta ujinga na ubishi kufikia nchi ya viwanda, huyo ndio tudili naye. Hawa wafanyakzi wako wa chini, wanatafuta kukufurahisha kwa kupambana na wapinzani. Je ni maendeleo?

Hata kama utaongoza miaka 40, bila uhalisia wa uongozi wako, historia haitaacha kukumbuka hivyo ulivyofanya. Mh Rais, CCM inaweza isitoke madarakani kwa miaka ya karibu, lakini utaongoza vizuri zaidi tunapokuwa na umoja wa kitaifa. AMANI! AMANI! AMANI!AMANI!

UBARIKIWE.

 
ata kama utaongoza miaka 40, bila uhalisia wa uongozi wako, historia haitaacha kukumbuka hivyo ulivyofanya. Mh Rais, CCM inaweza isitoke madarakani kwa miaka ya karibu, lakini utaongoza vizuri zaidi tunapokuwa na umoja wa kitaifa. AMANI! AMANI! AMANI!AMANI!
Amaniiiiii!
 
Umeandika vizuri mkuu ila sidhani kama atapitia huu Uzi ingekuwa ni shilawadu kesho kesho ungesikia anakuja na majibu mazuri au mipasho.....kwa Mara ya kwanza Tanzania tumepata Raising wa ajabu kweli kweli.
 
Mimi sikufurahi huyu mtu kuwa Prezdaa, alionekana wazi kupungukiwa sifa za uongozi. Ni ujinga wa Watanzania ndio umefanya awepo mjengoni. Asilimia kubwa ya Watanzania hawajui kuchuja na kujua yupi anafaa kuwa kiongozi, na hata ukiwaelimisha hawakuelewi, wanatanguliza ushabiki wa vyama na kufuata mkumbo. Madhara ni makubwa.
 
vyuma vimekaza °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
 
Back
Top Bottom