Rais Wangu TCRA imeshindwa Kuionya Mtandao wa Tigo, Nisaidie Baba

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
376
691
Huu mtandao kwa kweli sasa niseme tu basi.
Kosa ukibakisha salio kwenye simu yako, yani utaunganishwa kwenye vihuduma vyao ambavyo hata hujawahi kuvisikia.

Leo nimebakisha salio kubwa tu nashangaa baada ya dakika kumi wakanitumia msg kuwa nimefanikiwa kuunganishwa na huduma ya tigo game.

Kiukweli mimi kwanza sio mpenzi wa Games, na sina game lolote kwenye simu.

Nimewapigia wakaniambia inaweza kuwa kuna app ya game yao au kupitia ads zao. Lkn sijawahi kuclick ads ya tigo.

Simu yangu hajawahi ishika mtu yoyote useme labda yeye ndiye kaniunganisha.

Sio hili tu, mara nyingi unakuta unapewa mkopo bila kuwaomba.

Tumekuwa tukitoa malalamiko TCRA lkn nao wamekuwa bubu kushughulikia matatizo haya. Mnatufanya tuhisi kuna rushwa inawafanya kuwa vipofu na viziwi kushughulikia matatizo haya.

Sasa mimi siiombi TCRA wala Waziri husika, maana wote ni butu katika kushughulikia matatizo yetu.

Mimi nakwenda Moja kwa moja kwa Rais Magufuli mtetezi wa wanyonge.
Nakuomba Rais wangu uweze kuwashughulikia hawa Tigo wairudishe ela yangu shilingi miambili (200/=) walionitapeli hawa tigo.

Nakuomba Rais utambue kuwa hii ufisadi sasa umekithiri katika mitandao ya simu kwa kutuunganisha katika huduma ambazo hatujajiunga.

Tunaomba uondoe Ufisadi huu kama sera yako inavyosema.

Nawasilisha.
wp_ss_20170113_0001.png
 
Kiukweli Tigo wanaboa sana, wamekuwa ni waganga njaa.

Jambo kama hili ingekuwa ni Ulaya au marekani, unafungua kesi na unalipwa faini.

Bora wewe umeweza kuweka malalamiko yako hapa, sijui wale wa vijijini inakuwaje.

Mimi huwa nikiweka salio naweka la kifurushi tu na tena najiunga haraka na kwa hofu isije ikakatwa. Ukiacha salio utashangaa umekatwa na kuambiwa umefanikiwa kjiunga na huduma fulani.

TCRA kule hakuna mtu wa kuinyoosha hii mitandao, wote wamewekwa mifukoni.
 
Hama mtandao faster,tigo si baba yako au mama yako aisee.
Mie voda walianza manyaunyau yao nikahamia airtel,kwa sasa wameanza kujirudi naona.
 
Back
Top Bottom