Rais wangu sikia kilio chetu, tupatie ajira

ryoba nyamhanga

New Member
Jul 11, 2016
2
1
Ndugu wanajamiiforums,

Mimi napenda kutumia jukwaa hili kumwomba Rais wangu mheshimiwa dr John Joseph Pombe Magufuli ninayemwamini sana atoe ajira kwa vijana tuliohitimu kozi mbalimbali katika taasisi mbalimbali za elimu hapa nchini, wakiwemo walimu wa ngazi ya cheti,diploma na digrii.

Nasema hivi kwa kuwa vijana nikiwemo mimi tuna shida kubwa kuishi bila ajira. Ukipuuza mimi sitakufanya chochote ila shida unazotupatia, Mungu atakutumbua ifikapo 2020.
 
Umeanza vizuri ila ukamaliz kwa hasira... JPM anapita sana hapa JF.. Kwa hio kama una suggestion iwe constructive bila jazba.. Sio wewe tu ambaye huna ajira.. Wengi tupo kitaa hatuna ajira.. Hili suala la vyeti feki labda litatupatia ajira wenye vyeti vya haki.
 
Mawazo ya kifukara hayo, achana na ndoto za Magufuli kuangushwa mwaka 2020, labda kama sio sisi ndio tuliomchagua bali nyie ndo mtafanikiwa, otherwise, Mh. Magufuli for life, kama Mgabe vile.

By the way, kijijini kwenu kuna mashamba kibao na mvua zipo za kutosha, nenda kalime ndugu yangu kama hapa mjini hakuna ajira, pembejeo za kilimo zinagawiwa za kutosha. Mjini tupo karibia milioni tano, hatuwezi kuajiriwa wote, sawa ndugu? uchangamshe ubongo wako, hatuwezi ajiriwa watanzania wote milioni 50, sasa nani atakuwa anapokea huduma zetu?
 
Subiri kijana utaratibu mzur unawekwa, kutokana na walimu wa masomo ya arts kutosha hadi kuwa na ziada ya walimu elfu 79 sasa hivi nahisi ajira zitatolewa kwa mahitaji na hivyo kuzingatia wale wenye ufaulu mzuri kuanzia o level hadi chuo kikuu. Hapa nahisi wale wahitimu wa vyuo binafsi hii komenti itawakwaza
 
Serikali imefulia haina hata pesa ya kuwatunza hawa iliyowaajiri sembuse wapya,,ndugu tafuta tu maarifa mengine..pole mkuu
 
Utapata wapi ajira wakati hadi hotel kubwa kubwa zimegeuka kuwa Hostel za wanafunzi. Subiri viwanda vikijengwa kwa hii bajeti ya bilioni 60.
 
Ndugu wanajamiiforums,

Mimi napenda kutumia jukwaa hili kumwomba Rais wangu mheshimiwa dr John Joseph Pombe Magufuli ninayemwamini sana atoe ajira kwa vijana tuliohitimu kozi mbalimbali katika taasisi mbalimbali za elimu hapa nchini, wakiwemo walimu wa ngazi ya cheti,diploma na digrii.

Nasema hivi kwa kuwa vijana nikiwemo mimi tuna shida kubwa kuishi bila ajira. Ukipuuza mimi sitakufanya chochote ila shida unazotupatia, Mungu atakutumbua ifikapo 2020.
Karibu sana jamvini.!
Ukiwa unasubiri ajira za Magufuli tafuta shughuli ya kufanya kwa sasa maana ajira haijulikani lini zitatolewa.!
 
Jaribu kuwa muelewa chalii angu.. sio kwamba hamtaajiriwa.. kuna mambo yanawekwa sawa then kila kitu kitakua sawa.. kuwa na subra mkuu..
 
Back
Top Bottom