Rais wangu Samia Suluhu, tusiguse Hifadhi

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Watanzania na walimwengu wamemsikiliza vema Rais Mama Samia hii leo. Amezungumza mengi yenye tija kwa nchi na wananchi wa Tanzania. Mwanzo wake ni mzuri. Hatuna budi kumuunga mkono.

Pamoja na utamu wote wa hotuba, naomba kwa taadhima kubwa nimpe hadhari kwenye msimamo wake wa kuchimba madini katika Hifadhi za Taifa. Hili hatuna budi kuwa makini nalo. Kumega maeneo ya hifadhi ( za wanyamapori) ili kuchimba madini kutaua ikolojia na hivyo kutaathiri wanyamapori. Suala hapa si ukubwa wa eneo, bali ikolojia. Ukubwa wa maeneo ya hifadhi unatokana na ikolojia.

Mfano, leo Masai Mara ikiuawa kama ilivyokuwa kwenye ujenzi wa hoteli, Serenmgeti nayo itakufa tu! Wanyama huhama kufuata malisho. na ukiwalazimisha wabaki sehemu moja watakosa chakula, na watakufa. Mfano, ukimega eneo la Tarangire, ujue kuna wanyamapori hawatakuvuka kwenda Ziwa Manyara.

Madhara yake ni makubwa. Watazaliana wenyewe kwa wenyewe na mwishowe tutakuwa na kizazi dhaifu kisichohimili maradhi n.k. Hii ni kama ndugu wa nasaba moja wakizaliana wenyewe kwa wenyewe. Unaweza kuwa na kizazi cha watu wenye taahira.

Bila shaka Rais alilenga kule Selous ambako kuna madini ya urani. Kama ndivyo, asihangaike. Ajielekeze pale Makanya wilayani Same ambako kuna madini ya urani mengi mno. Profesa Posi anajua hili jambo.

Kama ni kuchimba dhahabu, kuanzia Seronera hadi Fort Ikoma ni dhahabu tu! Leo kukichimbwa dhahabu pale ikolojia itakufa na wanyamapori watatoweka. Kwa kuwa madini ya huku nje hatujamaliza kuyachimba, Rais Mama yetu asiwahi kuingia hifadhini.

Tuyamalize haya ya nje ya hifadhi kwanza. Tusiwe na haraka. Kizazi chetu bado kipo na bado kinakuja. Ukiacha hilo, nampongeza kwa kutambua kuwa bila juhudi za makusudi, Ngorongoro inakufa. Tusikubali ife. Tuilinde maana ni fahari ya ulimwengu mzima.

Manyerere
Dar es Salaam
 
Tufukue tu madini yetu tuangalie tu yatatuingizia bei gani tukilingamisha na pesa za utalii kama zinapita utalii kwa mbali tuchimbe na wanyama waliomo humo mbugani tuchinje nyama yake tuuze buchani tule tufaidi nyama na madini
 
Tule tu mapema vya kwetu, maana umri wenyewe haueleweki, Jamaa kaishia 61 sisi wengine hatujui hata kama tutafika hiyo 61.
 
Hata mimi nilishangaa,ukishaingiza mabulludozer kwenye hifadhi hiyo hifadhi inakuwa imekosa sifa. Nazani awekeze nguvu kwenye usimamizi wa machimbo yaliyopo sasa bado madini ni mengi!
 
Watanzania na walimwengu wamemsikiliza vema Rais Mama Samia hii leo. Amezungumza mengi yenye tija kwa nchi na wananchi wa Tanzania. Mwanzo wake ni mzuri. Hatuna budi kumuunga mkono.

Pamoja na utamu wote wa hotuba, naomba kwa taadhima kubwa nimpe hadhari kwenye msimamo wake wa kuchimba madini katika Hifadhi za Taifa. Hili hatuna budi kuwa makini nalo. Kumega maeneo ya hifadhi ( za wanyamapori) ili kuchimba madini kutaua ikolojia na hivyo kutaathiri wanyamapori. Suala hapa si ukubwa wa eneo, bali ikolojia. Ukubwa wa maeneo ya hifadhi unatokana na ikolojia.

Mfano, leo Masai Mara ikiuawa kama ilivyokuwa kwenye ujenzi wa hoteli, Serenmgeti nayo itakufa tu! Wanyama huhama kufuata malisho. na ukiwalazimisha wabaki sehemu moja watakosa chakula, na watakufa. Mfano, ukimega eneo la Tarangire, ujue kuna wanyamapori hawatakuvuka kwenda Ziwa Manyara.

Madhara yake ni makubwa. Watazaliana wenyewe kwa wenyewe na mwishowe tutakuwa na kizazi dhaifu kisichohimili maradhi n.k. Hii ni kama ndugu wa nasaba moja wakizaliana wenyewe kwa wenyewe. Unaweza kuwa na kizazi cha watu wenye taahira.

Bila shaka Rais alilenga kule Selous ambako kuna madini ya urani. Kama ndivyo, asihangaike. Ajielekeze pale Makanya wilayani Same ambako kuna madini ya urani mengi mno. Profesa Posi anajua hili jambo.

Kama ni kuchimba dhahabu, kuanzia Seronera hadi Fort Ikoma ni dhahabu tu! Leo kukichimbwa dhahabu pale ikolojia itakufa na wanyamapori watatoweka. Kwa kuwa madini ya huku nje hatujamaliza kuyachimba, Rais Mama yetu asiwahi kuingia hifadhini.

Tuyamalize haya ya nje ya hifadhi kwanza. Tusiwe na haraka. Kizazi chetu bado kipo na bado kinakuja. Ukiacha hilo, nampongeza kwa kutambua kuwa bila juhudi za makusudi, Ngorongoro inakufa. Tusikubali ife. Tuilinde maana ni fahari ya ulimwengu mzima.

Manyerere
Dar es Salaam
Kwani tembo wanayala?
 
Hapa mwanangu una hoja kubwa. Maana inavyoonekana tunaweza kujikuta kwenye ruxa bila kujua halafu tunaanza kulaumiana.
 
Hapo kachemka.

NA SOON HUYU MAMA ATA LETA MADHARA KWA TAIFA.

naona kama ana dalili za Mzee Mwinyi wa awamu ya pili, TUNA RUDI KE KWENYE
"RUKSA".
 
Ni vema tujikite kutengeneza vision ya nchi katika kila sekta kwa walau miaka 30 ijayo.
Jpm ni mkemia kuna siku alisema jambo muhimu sana kuwa kama kuna madini yachimbwe sasa kwasababu teknolojia inabadilika sana na haya madini yaliyopo huwenda yasiwe na thamani tena mbeleni
 
Back
Top Bottom