konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,582
Wakati nipo sekondari nilikuwa natamani niwe sehemu ya watunga sera za nchi au kuwa kiongozi serikalini, na hii ilisababishwa na jinsi nilivyokuwa naona mambo yanavyoendeshwa nchini. Niliona bila kuingia ndani ya siasa siwezi kubadirisha chochote, nitabaki kuwa mtazamaji tu, kama kuna mambo hayapo sawa na ninahitaji kuyabadirisha sina budi kuingia jikoni na hii ndoto nahisi siku moja itakuja kutimia. Mniombee.
Kwa sasa kila nikiiangalia nchi yangu naona inahitaji viongozi wenye maono na mikakati isiyoyumba ili kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kwanza. Nchi za Ulaya na Amerika ya kaskazini hazijaamuka tu siku moja zikawa pale zilipo. Viongozi wake walikuwa na maono na mikakati isiyoyumba, na kila rais au kiongozi aliyekuwa anapata dhamana ya kuongoza alikuwa anatembea mle mle kwenye yale maono na mikakati iliyowekwa na watangulizi wake. Kama wao waliweza kuwa ulimwengu wa kwanza kwa nini sisi watanzania tushindwe ukizingatia sisi tuna rasimali za asili nyingi kuwazidi wao, tuna hali ya hewa nzuri, tuna ardhi inayomea kila aina ya mmea.
Natamani Tanzania iwe nchi ya kwanza Africa kufikia uchumi wa kwanza. Hili lipo ndani ya uwezo wetu watanzania, ni swala la kuamua tu na kujifunga mkanda.
Naomba tujadili kidogo nini kifanyike, hii ni nchi yetu, hatuna nchi nyingine zaidi yahii.
Binafsi vifuatavyo ni baadhi ya mambo ambayo yakifanyika Tanzania inakuwa ni miongoni mwa nchi za ulimwengu wa kwanza.
i. Elimu,
Hakuna nchi yeyote katika ulimwengu wa kwanza iliyoendelea kiuchumi bila kuweka mifumo mizuri ya elimu, na zaidi ya yote bila kuwekeza kwenye masomo ya sayansi na hesabu. Elimu bora ndio kila kitu kwenye maendeleo. Sasa hivi dunia ipo kwenye ulimwengu wa sayansi na tekinologia, bila elimu tutabaki kuwa wachuuzi tu, hatuwezi kumiliki na kuendesha viwanda vyetu. Kuna rafiki yangu ni raia wa Canada ila ana asili ya kieritrea, ana ndugu zake wa damu Ujerumani na nchi za Scandinavia. Nchi zote hizo amefika na kukaa kidogo. Aliniambia “Africa bila kuwekeza kwenye elimu tutabaki kuwa nyuma siku zote, Africa itapiga maendeleo makubwa ya kiuchumi kama itawekeza kwenye elimu hasa masomo ya sayansi na hesabu”. Alinitolea mfano nchi ya Sweden kama sikosei au the Netherlands ilikuwa masikini sana lakini serikali ilitunga sera na sheria kuhakikisha masomo ya sayansi na hesabu yanakuwa ya lazima, na kuhakikisha wanafunzi kutokea elementary school hadi chuo wanafundishwa vyema, wanapikika na kuiva kwenye hesabu na sayansi. Yalikuwa ni malengo ya muda mrefu lakini baada ya muda matunda yalionekana, na sasa kama mnavyoona hiyo nchi ipo ulimwengu wa kwanza. Anasema hiyo nchi walimu wanaongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa. Kwa hiyo sisi watanzania kama tunataka kufika huko lazima tuwekeze kwenye elimu, hakuna short cut ya maendeleo, lazima tuwe na mipango ya muda mrefu ambayo tutakuwa na uhakika kuwa baada ya muda fulani tutakuwa level nyingine. Natambua tunaweza kuwa na changamoto ya kupata walimu wa hesabu na sayansi kukidhi mahitaji ya shule zetu lakini tukiamua hii changamoto tunaishinda. Kuishinda hii changamoto serikali inaweza kutangaza nafasi za kazi za ualimu wa hayo masomo duniani. Mtu yeyote kutoka nchi yeyote anayeyamudu hayo masomo aruhusiwe aje apate kazi, na viza yake isiwe na urasimu kuipata. Kuwe tu na screening ya uhakika ili isitumike kama uchochoro wa raia wa nchi zingine kuja kufanya yao Tanzania.
Nchi ya Korea ya kusini ina utaratibu wa watu kutoka mataifa ambayo English ni lugha ya nyumbani kuruhusiwa kwenda kufundisha kiingeeza huko. Ukiwa na passport ya hizo nchi unapata viza ya kwenda kufundisha kiingereza. Kwa nini Tanzania tusifanye hivyo.
Malengo ya nchi, rais akiingia madarakani lazima ayafuate.

- Lazima tupate katiba nzuri inayokwenda na wakati tulionao
- Kuhakikisha serikali inakuja na sera za kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.
- Lengo jingine la muda mfupi linaweza kuwa hili; Hizi nafasi za uteuzi zenye mishahara mikubwa kama ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya, ukatibu mkuu, ukatibu tawala na zingine zote zinazoshabihiana na hizi zitumikiwe kwa miaka miwili tu ili kuwapisha wengine.
- Lengo jingine la muda mfupi ni hili, au linaweza kuwa la muda mrefu inategemea litadumu kwa muda gani;
- Malengo ya muda mrefu
i. Elimu,
Hakuna nchi yeyote katika ulimwengu wa kwanza iliyoendelea kiuchumi bila kuweka mifumo mizuri ya elimu, na zaidi ya yote bila kuwekeza kwenye masomo ya sayansi na hesabu. Elimu bora ndio kila kitu kwenye maendeleo. Sasa hivi dunia ipo kwenye ulimwengu wa sayansi na tekinologia, bila elimu tutabaki kuwa wachuuzi tu, hatuwezi kumiliki na kuendesha viwanda vyetu. Kuna rafiki yangu ni raia wa Canada ila ana asili ya kieritrea, ana ndugu zake wa damu Ujerumani na nchi za Scandinavia. Nchi zote hizo amefika na kukaa kidogo. Aliniambia “Africa bila kuwekeza kwenye elimu tutabaki kuwa nyuma siku zote, Africa itapiga maendeleo makubwa ya kiuchumi kama itawekeza kwenye elimu hasa masomo ya sayansi na hesabu”. Alinitolea mfano nchi ya Sweden kama sikosei au the Netherlands ilikuwa masikini sana lakini serikali ilitunga sera na sheria kuhakikisha masomo ya sayansi na hesabu yanakuwa ya lazima, na kuhakikisha wanafunzi kutokea elementary school hadi chuo wanafundishwa vyema, wanapikika na kuiva kwenye hesabu na sayansi. Yalikuwa ni malengo ya muda mrefu lakini baada ya muda matunda yalionekana, na sasa kama mnavyoona hiyo nchi ipo ulimwengu wa kwanza. Anasema hiyo nchi walimu wanaongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa. Kwa hiyo sisi watanzania kama tunataka kufika huko lazima tuwekeze kwenye elimu, hakuna short cut ya maendeleo, lazima tuwe na mipango ya muda mrefu ambayo tutakuwa na uhakika kuwa baada ya muda fulani tutakuwa level nyingine. Natambua tunaweza kuwa na changamoto ya kupata walimu wa hesabu na sayansi kukidhi mahitaji ya shule zetu lakini tukiamua hii changamoto tunaishinda. Kuishinda hii changamoto serikali inaweza kutangaza nafasi za kazi za ualimu wa hayo masomo duniani. Mtu yeyote kutoka nchi yeyote anayeyamudu hayo masomo aruhusiwe aje apate kazi, na viza yake isiwe na urasimu kuipata. Kuwe tu na screening ya uhakika ili isitumike kama uchochoro wa raia wa nchi zingine kuja kufanya yao Tanzania.
Nchi ya Korea ya kusini ina utaratibu wa watu kutoka mataifa ambayo English ni lugha ya nyumbani kuruhusiwa kwenda kufundisha kiingeeza huko. Ukiwa na passport ya hizo nchi unapata viza ya kwenda kufundisha kiingereza. Kwa nini Tanzania tusifanye hivyo.
Malengo ya nchi, rais akiingia madarakani lazima ayafuate.
- Kwa sababu tumeamua kama nchi kufikia uchumi wa juu, itungwe sheria ya kumtaka kila rais anayeingia madarakani ayatekeleze malengo ya nchi. Rais hatakuwa na uwezo wa kuiendesha nchi anavyotaka yeye. Awe na job description kabisa kwamba watanzania wamejiwekea malengo haya hivyo ukiingia madarakani lazima uyatekeleze, ukienda kinyume na hayo malengo bunge linakutoa kwenye hicho kiti cha urais na makamu wa rais anachukua usukani au uchaguzi mwingine unafanyika. Katiba itaweka wazi kipi ni bora zaidi kati ya kufanya uchaguzi au makamu wa rais kushika madaraka.
- Ili kuhakikisha hili linafanyika, inaweza kuundwa taasisi huru ambayo itakuwa inahakikisha rais anafuata katiba. Unajua sisi watanzania ni wapole sana. Tunaweza kuwa na katiba bora kabisa ambayo imeainisha mambo yote yanayotakiwa kutekelezwa na rais, na tukawa na taasisi amabayo jukumu lake ni kuhakikisha katiba haivunjwi. Lakini pamoja na kuwa na hivi vyote unaweza kukuta rais bado anavunja katiba na hiyo taasisi iliyoundwa kumuwajibisha rais haimfanyi chochote, na raia nao washatishwa kupigwa kipigo cha mbwa koko wamefyata hata kuandamana kushinikiza katiba ifuatwe hawawezi. Sasa nini kifanyike, labda inaweza kutungwa sheria inayotambua huu woga na udhaifu wa watanzania ikasema kwamba “Pale rais au kiongozi yeyote wa juu serikalini anapovunja sheria au anapoenda kinyume na mipango iliyaoanishwa kwenye katiba, raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kufungua kesi katika mahakama za kimataifa ili kushikikiza katiba ifuatwe na kumwajibisha rais au kiongozi aliyevunja katiba au aliyeenda kinyume cha malengo yaliyoainishwa kwenye katiba”
- Kwa muktadha huu mahakama za kimataifa zitakuwa zimearifiwa kuhusu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo zitakuwa na mamlaka yaku-prosecute kesi ya namna hii itakapoletwa mbele yake. Kuna watu wataanza kusema Konda msafi wewe sio mzalendo, rais wetu ashitakiwe nje tena? hapana mimi ni mzalendo, najaribu tu kuwa realistic. Haya ni mawazo tu ambayo yanaweza kufikiriwa kuingizwa kwenye katiba na sio lazima yaingizwe, huenda kukawa na mawazo bora zaidi ya haya ambayo yatasaidia kuhakikisha katiba inalindwa na malengo tuliyojiwekea kama nchi hayatelekezwi.
- Rais kuachana na mambo ya uchama akiwa madarakani
Kwa sababu tumeamua kupiga kazi kwa ajili ya nchi yetu. Uchaguzi ukiisha na rais akatangazwa katiba imzuie rais kushabikia hadharani mambo ya chama chake badala yake awatumikie wananchi. Mambo ya mipasho kuwananga wapinzani yasiwepo, kauli za kuwagawa wananchi kwa misingi ya chama zisiruhusiwe. Rais ni rais wa raia wote na sio rais wa chama kilichompa ticketi ya kuwania urais. Mambo ya chama atayaongea akiwa kwenye vikao vya chama chao lakini anapokuwa nje au kwenye ziara za kikazi hataruhusiwa kuongea mambo ya kichama. Atatakiwa awe na kazi ya kuhamasisha umoja, ushirikiano na uzalendo na kutekeleza malengo yaliyoainishwa kwenye katiba.
- Sheria kandamizi
Ili tufike tunakotaka, sheria kandamizi zote zifutwe. Sheria zina nafasi kubwa sana kwenye kuleta maendeleo. Sheria zote zinazokwamisha maendeleo zifutwe. Sheria zote kandamizi zifutwe. Mojawapo ya sheria kandamizi ambazo binafsi ningependa zifutwe ni hizi: sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PSSSF. Kumpangia mtu namna ya kutumia hela yake, hii sheria ni kandamizi. Fao la kujitoa lirudishwe. Mfanyakazi akiachishwa kazi au akiacha kwa hiari yake apewe hela yake ikamsaidie mambo yake. Haya mambo ya kumzuia kuchukua hela yake mpaka uzeeni hayafai. Apewe hela yake ili kama anataka kufanya biashara akafanye akatengeneze ajira. Sheria nyingine kandamizi ni hii ya kufungwa miaka 30 jela ukimpa ujauzito mwanafunzi. Hii sheria ukiachilia kuwa ni kandamizi pia inamnyima haki mtoto atakayezaliwa haki ya kulelewa na wazazi wake wote wawili. Unapomfunga baba wa mtoto huoni kama unakitesa kiumbe kisichokuwa na hatia? Baba ake mmemfunga, huyo mtoto atahudumiwa na nani? Mama mjamzito atahudumiwa na nani? Zaidi ya yote unapomfunga baba wa mtoto unapata faida gani? Sheria kandamizi zipo nyingi, hizi mbili ni mifano tu.
Karibuni tujadiliane, ushauri na mapendekezo. Tanzania ni yetu sote. Kazi ieendelee.