BM Pesambili
Senior Member
- Jul 10, 2016
- 102
- 624
Ni aibu tena ni aibu sana kujishusha na kujidumaza kimataifa kwa kiwango juu cha kugeuka maskini na ombaomba, kwamba tunaweza kuendelea kwa misaada kutoka kwa wahisani huku Tanzania ikiwa na rasilimali lukuki? Heshima na utu wa Mtanzania kiuchumi umebaki unahabika na kudhalilika kimataifa.
Rais wangu ni lini au ni wapi uliposikia mtu ombaomba akapata heshima? Siku zote ni mtu wa kudharauliwa na watu wote na haitatokea kupata heshima popote pale. Uko upuuzi mwingi na masharti ya ajabu ya hawa tunaowaita wahisani, ndio maana tunamashoga na wasagaji na taasisi za siri zinazowasaidia ndani ya nchi yetu. Ukijaribu kupinga tunatishiwa kusitishiwa misaada yao hati kisa haki za binadamu!!! Upuuzi sana yaani tuendelee kufuga mashoga na wasagaji eti kisa misaada.
Rais wangu nakuunga mkono kuthubutu hata kutamka hadharani kwamba imefika wakati tujitegemee. Japo kuna watu wanabeza mi nasema tuwapuuze wameubwa hivyo hakuna jema kwao hata ukifanya nini ni asili yao. Tumechoka kuwa ombaomba, ombaomba hana heshima popote duniani.
Rais wangu Magufuli ebu tujikumbushe kidogo Busara za baba wa Taifa
"Hutumheshimu Athumani bin Maganga kwa sababu anakula chakula cha kuomba; anavaa kilemba cha kuomba, kiatu chake cha kuomba, kitanda cha kuomba. Athumani bin Maganga mahari aliyoolea Binti Musa ni mahari ya kuomba. Binti Musa yuko nyumbani na kajaliwa kuzaa. Lakini kila siku yuko barabarani anatoka nyumba hata nyumba, hodi, karibu! Hapa kaja kuomba nini? Kaja kuomba vitumbua. Anaombaomba, Mara anatoka hapo, akishapata vitumbua hapo anakwenda nyumba ya tatu; huko anakwenda kuomba nini? Anakwenda kuomba kibiriti, nyumbani hakuna moto.
Ni dhairi kwamba mtu huyu hawezi akaheshimiwa. Tena watu hawatamwita Athumani bin Maganga, watamwita Athumani bin Ombaomba, jina lake ni " ombaomba" na wakimwona watu wanaanza kufunga milango wanasema " Huyo tena anakuja" Wanafunga milango. Hawamkaribishi, hawampokei, hana heshima; majirani zake wote wanamsema mtu wa namna hii, mtu balaa, mtu yule. Mtu mzima, si kilema, si mgonjwa lakini ombaomba hafanyi kazi, hataki kujitegemea. Anakula vya wengine; kupe mkubwa! Hawezi akaheshimiwa na mtu."
Kadhalika taifa haliwezi likaheshimiwa kama taifa la Bin ombaomba, waombaji wakubwa. Iwe Taifa la Tanzania mambo yetu ya kulijenga taifa letu liheshimike sana duniani ni kuomba. Kila siku kuomba, chakula cha kuomba, kila kitu chetu sisi ni cha kuomba. Tukichagua viongozi ni viongozi wetu wa kuomba. Rais Nyerere anasifiwa na wananchi wa Tanzania, wanasema " Tuna president hodari sana" Uhodari wake nini? Ni mwombaji sana Rais wetu. Mara yuko Marekani, Mara yuko China, Mara yuko India, Mara yuko wapi, anakwenda kuomba. Na akirudi ana mahindi mfukoni. Rais wetu mtu mkubwa sana. Na asipokwenda mwenyewe, huwapeleka mawaziri; wala hawachelewi. Mara waziri mmoja yuko huku kusini, Mara mwingine kaskazini; hawakai mawaziri, hawatulii hata kidogo. Wamo katika safari za kuomba omba" Hii ni hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyeitoa februari 5, 1967 jijini Dar es salaam.
Rais wangu Magufuli tumechoka kuitwa Maganga bin Ombaomba, pambana kulijenga taifa letu lijitegemee najua ni safari ni ndefu lakini inawezakana.
Boniphace M. Pesambili.