Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu. Tumezoea kuona migomo kwa walimu, wauguzi, makonda na madereva na hata mawakili. Hili la Waziri kugoma ni tukio la pekee na halijawahi kutokea zaidi ya Tanzania. Kwanza nianze kwa kusema kuwa Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye na hata Januari Makamba ni viongozi vijana waliobahatika kuaminiwa lakini wameshindwa kuaminika. Uzoefu unaonesha kuwa Mawaziri vijana ufanisi wao ni mdogo na wamekuwa chanzo cha majungu na matatizo ndani ya Wizara walizoongoza. Wapo kama Ngoswe.
Mifano ipo mingi sana. Walikuwepo Mathayo David, Adam Malima ambaye aliporwa Bunduki akiwa Guest, Masele, Laurence Masha, Lazaro Nyalandu, Emmanuel Nchimbi nk. Hawa walikuwa ni Mawaziri vijana ambao wakati wanateuliwa, tuliwasifu na kuwapigia makofi. Lahaulaaaaaa! Utendaji wao uligeuka kuwa majipu na mwisho wa siku waliishia kutumbuliwa.
Mwigulu Nchemba ameangukia kwenye shimo hilo kama alivyoangukia mwenzake Nape Nnauye. Angalau Januari Makamba amejirekebisha baada ya kusoma alama za nyakati. Anachofanya Mwigulu kwa sasa ni kuwachonganisha Wabunge na Serikali. Yeye ndiye anayewalisha maneno akina Hussein Bashe na Zitto Kabwe ili wapige kelele bungeni ili Serikali yote ya Rais Magufuli ionekane haina maana. Ni mpango mkakati unaoratibiwa na kutekelezwa na wenye vinyongo dhidi ya Rais Magufuli.
Niwahakikishie tu kuwa mnayopanga gizani yanaonekana baada ya jua kuchomoka. Lazima tuheshimiane. Mwigulu yupo kwenye mgomo na sababu anazijua yeye. Hili si la kificho. Ila anachokitafuta atakipata. Utawala wa sasa si wa kubembelezana. Wabunge wenye sifa wapo wengi.
=======
Majibu ya Waziri wa Mambo ya ndani katika Mada hii

Nimesoma Ujumbe huu, NIMESIKITIKA SANA, Hii ndio SABABU KUBWA YA UMASIKINI HAPA AFRIKA NA TANZANIA
Halafu mtu mzima anaandika vitu vya ajabu ajabu sana kama hivi kwa kuficha ID. Mawazo kama haya ndio chanzo cha umasikini
1) Wizara ya Mambo ya ndani ni wizara ya vyombo vya dola, na inaongozwa na Idara zenye makamanda waliopitia mafunzo na wanaojua majukumu yao, SIO WIZARA YA WAZIRI KILUSEMA KILA DAKIKA, SIO KILA HABARI NI HABARI KWENYE WIZARA HII. UNATAKA WAZIRI AONGEE KABLA YA ASKARI KUFANYA KAZI YAO? Kuacha jambo lifanyiwe kazi kwa Weredi ndio mgomo?
2) Halafu mtu anasema kuna watu wana vinyongo then ananitaja na mimi uko timamu kweli? Yaani nimepewa Wizara ya Kilimo mara ya kwanza imani kubwa sana hiyo, Nimepewa Mambo ya Ndani hiyo ni Imani kubwa sana. Unaona kinyongo na unaona mgomo kwa kuendesha Wizara kwa weredi? Wewe sio na kinyongo unapiga majungu tulio na vinyongo tuna msadia mhe Rais.
3) Unasema mimi nimewapa Taarifa akina Bashe na Zitto. Yaani ndugu yangu UPEO WAKO MDOGO SANA, Unajua najua taarifa ngapi za nchi? Au hujui maana ya Home Affairs? Yaani Bashe kusema alikamatwa ni jambo la kuambiwa,? Ungekuwa Mbunge ningekuomba uwatake wasimame humu humu Bungeni waseme kama mimi nimewapa siri yeyote ya serikali iliyo kinyume na Kiapo changu. Wakisema hivyo nitawajibika. Kwanza ungejiuliza kwanza, nimewapa maneno gani? Pili kwa ajili ya nini na ili iweje? Ndio watu mnaodandia mnawaza kwa dot, niliyekulia CCM tangu chipkizi, sioni hata mtu gani mwenye akili TIMAMU ANAWEZA KUWA CABNET HALAFU AKAWA NA MGOMO.
4) Usipende kuchukulia kila kitu kwa majungu, kwa ushabiki na kwa unafiki, Wizara hii inashughulika na Maisha ya watanzania. Inahitaji utimamu na Sio ukurupukaji.
Mimi kama kijana inafaida kubwa sana kumsadia Rais kwani anavyofanikiwa manufaa makubwa ni kwetu vijana, asipofanikiwa Hasara ni kubwa sana kwetu vijana kuliko mtu mwingine. Kwa usiojitambua unaweza kuwaza mgomo. Tunaojua tunatambua kuwa URITHI HUWA SIO KWA WAZAZI BALI KWA WATOTO. Taifa Imara faida yake sio tu kwa Rais, sisi vijana ndio wanufaika.
Unaandika kwa uhakika kuwa yuko kwenye mgomo halafu sababu unasema anazijua mwenyewe.
Rudi kwa aliyekutuma kunichafua umwambie kuwa Cheo ni dhamana sio kitu cha kudumu ila Utu na Hatima ya Taifa letu ni vitu vya kudumu. Siwezi kufanya kazi za OCD,RPC, DCI, IGP na Msemaji wa Polisi, NITAFANYA ZA WIZARA.
MWIGULU