Rais wangu Kikwete wasilisha maombi haya kwa Rais Obama utakapokutana naye

Mipangomingi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,713
2,058
Japokuwa mimi si muumini wa kutembeza bakuli nje ya nchi, lakini kwa kuwa Rais wetu amesema asipofanya hivyo, watoto wake tutakufa njaa, sina budi kuchukua nafasi hii walau kumsaidia kuomba masuala ambayo huko baadaye tutamkumbuka sana. Rais Obama anakuja Tanzania akiwa Rais wa tatu wa marekani kutembelea Tanzania katika kipindi cha chini ya miongo miwili. Hakuna ubishi kwa mujibu wa Sera ya Marekani inayojali maslahi kuliko chochote, sababu kubwa ya Ziara ya Obama ni maslahi ya kiuchumi. Hata hivyo naweza kusema, Marekani ni miongoni mwa nchi chache ambazo ukiweza ku-negotiate vizuri na kukubaliana,basi harudi nyuma kwenye makubaliano na mambo yako yatakuwa ila ukienda kinyume, jua jina baya linakufuata.
Kwa mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu na ukanda wa Afrika Mashariki, mambo mawili nayaona yatatawala sana uchumi wa nchi hizi ikiwa pamoja na kuchukua sehemu kubwa ya utoaji wa ajira na hata kufanya "Eastern Africa energy and Mineral Hub" 1. Mafuta na gesi pamoja na madini mengineyo; 2. Ukuaji wa Viwanda na matumizi makubwa ya Nishati ya Umeme yatakayolazimu uwepo wa matumizi ya umeme wa Nuclear. Hata hivyo, kwa vile nijuavyo, nchi za Afrika Mashariki na Kati hazina wataalamu wala Chuo Kikuu kinachospecialize kutoa wataalam wa Mafuta, gesi na Nuklia kama ilivyo katika nchi za Kiarabu na zile zinazotumia nishati ya nuklia. Kwa muktadha huu, Nakumba Rais wangu tumia Diplomasia yako iliyofuzu kuwasilisha maombi mawili zaidi kwa Obama
1. Msaada wa Kuanzisha na kujenga Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi Mtwara (Mtwara University of Gas and Oil "MUGO"); Chuo hiki kiwe kikubwa kuliko ikibidi hata UDOM na uwezo wa kuchukua wanafunzi kimataifa na wa kutosha kikihusisha Fani zote zihusuzo mafuta na gesi ili kuweza ku-backup ile kauli yako kuwa Nchi inajiandaa na uchumi wa gesi. Unajua kitakachofuata iwapo chuo hiki kitaanzishwa; hata watani zangu akina Chinga kidogo watapoa japo beneficiries wakubwa watakuwa watani wangu wa kulee 'kilelen mwa Afrika'.

2. Msaada wa Kuanzisha Idara ya Nuklia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Dodoma (Nuclear Department). Uanzishwaji wa Idara hii(Kama ipo nitaomba mnisamehe) utatoa wataalamu watakaoweza kushirikiana na hao hao akina Obama katika madini ya Urani yanayoendelea. Idara hii ianze mapema kabla ya mtalaamu wa Nuclear Physics nimjuae hajachoka (Dr. Mohamed Gharib Bilal/Makamu wa Rais).

Kwa kuzingatia historia nzuri ya Rais katiak elimu, naamni haya Wamarekani watakuwa tayari kutusaidia na kutimizi ndoto zetu. Vinginevyo, pasipo kuwa na Chuo chetu wenyewe cha kutoa wataalam wa mafuta na gesi, tusahau ndoto za kuwa nchi yenye uchumi wa gesi. Chondechonde Rais wangu, ushauri huu pokea. Nimalizie kwa nahau isemayo: Kama mtu ukiwa ni hodari wa kuomba, basi omba mtaji usiombe matumizi.
 
Mawazo mazuri lakini njia mbovu! Kwanini tuombe kila kitu?
Uko sawa mkuu, nadhani nimeanza kwa kubainisha kuwa sifurahishwi na kuomba lakini ndio utaratibu ambao kama mtoto ndani ya nyumba naouona, hivyo nilichofanya ni kumshauri mwenye nyumba mambo ya kuomba amabyo si watotowe tunayataka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom