Rais wangu Jakaya Kikwete Unakumbuka ahadi yako Ari Mpya, Nguvu mpya na Kasi Mpya?


Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
376
Likes
5
Points
35
Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
376 5 35
WENGI walimwona ni tumaini lililorejea. Tukaanza kuona nuru ikimulika gizani. Matumaini yaliyofifia yakafufuka. Kumtazama tu ikawa kama ni tiba. Wengine wakatuambia huyu ni chaguo la Mungu. Wengi wakasema sasa Nyerere mwingine amepatikana. Watu wakatoa tabasamu pana na kukenua meno wakisuburi faraja. Ahadi yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania ikaleta hamu ya mapambazuko mapya. Lakini sasa imefika wakati watu wanalazimika kuamini kwamba walichokiamini ndicho, sicho. Kama walidhani wameona nyota, basi kilikuwa kimondo. Mwanga uliobashiriwa hauonekani tena na pambazuko tarajiwa limetoweka.
Huu ni mwaka wa mwisho sasa tangu uwe katika madaraka ya juu zaidi hapa nchini. Tuna haki kuhoji kasi, nguvu na ari zimetupeleka wapi? Tunatarajia kufika wapi? Mwelekeo wetu ni chanya au hasi? Maisha bora yametufikia? Au kaulimbiu imebadilika? Maisha bora uliyoahidi kwa Kila Mtanzania, ina maana hiyo hiyo kama yanavyotamkika maneno hayo? Tujadili ukweli hata kama ni mchungu.
 

Forum statistics

Threads 1,250,863
Members 481,494
Posts 29,748,417