Rais wangu J.M.Kikwete una tamko gani kuhusu Polisi kuua raia?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Matukio ya Jeshi la Polisi kuua raia hapa Tanzania sasa imekuwa kama kitu cha kawaida. Mifano mauaji yaliyomuusisha Zombe, maua ya raia kwenye mikutano ya kisiasa na matukio ya Jeshi la Polisi kutesa raia hadi kuwasababishia vilema. Je, kwa matukio haya bado Tanzania ni kisiwa cha amani?

Rais wangu umechaguliwa uilinde Katiba pamoja na roho za Watanzania, je unatekeleza wajibu huo?Binafsi sifurahishwi na hali hii katika nchi yetu.
 
Mulize Slaa ataacha lini kutumika kuvuruga Amani ya nchi yetu?
 
TAIFA LETU TULIPENDALO SAAANA LA TANZANIA HIVI SASA LIKO NJIANI KUANGAMIA SHAURI YA KUKOSA UONGOZI SIKIVU, ADILIFU NA WENYE HEKIMA

"Taifaa la Tanzania linaumwa tena linaugua ugonjwa wa hatari sana tangu uchaguzi wa Oktoba 2010, kufanyike juhudi za haraka kulitibu taifaa," alisikika miezi michahe akitoa hii kauli yenye hekima tele yule Mhe Mbuye wa Arusha alie likizoni Godless Lema.

Hata hivyo, ni wangapi ndani ya nchi hii walau waliweza kumuazima sikio na kutafakari ki-undani zaidi hii kauli?

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na maswahiba wake wanaoendelea kufilisi nchi hii kupitia Dowans, EPA na rundo la fedha za ki-shetani kwenye Benki Uswisi, wataendeleaa kuishi kwa matumaini ya ulinzi wa FFU mpaka lini?

Ama kweli Tanzania taifa langu linaangamia kwa kukosa uongozi wenye hekima na uadilifu.

Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine.

Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
 
we una maoni kuhusu chama chako kutwa kuvunja sheria kwa makusudi hali wanajua ni kinyume cha sheria. una maoni gani pia kuhusu
chama chako kumvalisha bomu mwandishi akijilipue kwenye vurugu za wanachama wenu! unafikiria kwa kutumia ubongo au gluteus(m...tko)
 
Nilishangaa kwa majibu nikagundua kuwa ni mpya JF, nani ametaja chama hapa, usitumiwe kama ZUZU/ROBOT.Tumia akili kuchangia mada badala ya kukurupuka.Maelezo yako yanaonyesha unafiri kwa kutumia Masaburi.
 
Mulize Slaa ataacha lini kutumika kuvuruga Amani ya nchi yetu?
<BR><BR>Kumbe Magamba wanaogopa wimbi la watanzania kujulishwa jinsi walivyowadanganya kwa miaka mingi.Dr.Slaa amesaidia kuwaamsha Watanzania kwenye lindi la uzingizi sasa mnahaha.Mkubali yaishe kwani hamwezi tena kuwadanganya watanzania kama mwanzo,mtaendelea kushindwa tuu.
 
Nilishangaa kwa majibu nikagundua kuwa ni mpya JF, nani ametaja chama hapa, usitumiwe kama ZUZU/ROBOT.Tumia akili kuchangia mada badala ya kukurupuka.Maelezo yako yanaonyesha unafiri kwa kutumia Masaburi.

mimi sio mpya ndani ya jamiiforums ila account hii ndo mpya! ungekuwa una uwezo mzuri wa kufikiria(IQ>100) usinge-draw conclusion eti mi mgeni kwa kuangalia account! two quite different thngs sucker!
upuuzi wako mwingne badala ya kujibu hoja unamuongelea mtu, toa hoja sio kukimbilia kuangalia account yangu haikusaidii kabisa! umri wa account na wewe kutoa jibu havitegemeani kabisa! shit!
 
Matukio ya Jeshi la Polisi kuua raia hapa Tanzania sasa imekuwa kama kitu cha kawaida.Mifano mauaji yaliyomuusisha Zombe, maua ya raia kwenye mikutano ya kisiasa na matukio ya Jeshi la Polisi kutesa raia hadi kuwasababishia vilema.Je kwa matukio haya bado Tanzania ni kisiwa cha amani?Rais wangu umechaguliwa uilinde Katiba pamoja na roho za Watanzania, je unatekeleza wajibu huo?Binafsi sifurahishwi na hali hii katika nchi yetu.

Atatoa tamko la kuwapongeza waislam kwa kuandamana bila ruhusa na kuwapongeza polisi kutoyavunja maandamano yao badala yake kubariki wavunja sheria waliogomea sensa kuachiliwa huru.Fikiria mrisho,said,suleiman,mohamed & co unatarajia nn
 
Mulize Slaa ataacha lini kutumika kuvuruga Amani ya nchi yetu?

Hebu jiulize ni nini leo hii waislamu wamefanya na ni hatua gani imechukuliwa.

Alafu utafakari nini kingetokea kama polisi wangetumia mabavu kuwatawanya.

Mwisho utapata jibu nani huwa ni chanzo cha vurugu kama ni polisi au wafuasi wa chadema.

Use your common sense.
 
Mulize Slaa ataacha lini kutumika kuvuruga Amani ya nchi yetu?

Duh, lakini sjamuona Slaa ameshika bastola au bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi !! Ooops, Hivi wale jamaa wa bastola kule Tabora hawajambo ??

Na bado sijamsikia Slaa akisema '...Liwalo na liwe...'.
Yule jamaa wa 'Liwalo na Liwe', mpaka sasa 'kauchuna' tu, hajatoa tamko lolote kulaani au kubariki mauaji ya Iringa !!!
 
mimi sio mpya ndani ya jamiiforums ila account hii ndo mpya! ungekuwa una uwezo mzuri wa kufikiria(IQ&amp;amp;gt;100) usinge-draw conclusion eti mi mgeni kwa kuangalia account! two quite different thngs sucker! &amp;lt;BR&amp;gt;upuuzi wako mwingne badala ya kujibu hoja unamuongelea mtu, toa hoja sio kukimbilia kuangalia account yangu haikusaidii kabisa! umri wa account na wewe kutoa jibu havitegemeani kabisa! shit!
Hayo unayoyaandika ndio yanaonye uu mpya JF.Haya sasa sema ni sheria gani iliyofunjwa na ambayo haijafunjwa leo na waislamu walioandamana na hakuna mtu aliyeuawa.Hapo una maoni gani?Ebu jibu acha jasba.
 
we una maoni kuhusu chama chako kutwa kuvunja sheria kwa makusudi hali wanajua ni kinyume cha sheria. una maoni gani pia kuhusu
chama chako kumvalisha bomu mwandishi akijilipue kwenye vurugu za wanachama wenu! unafikiria kwa kutumia ubongo au gluteus(m...tko)

Hapo kwenye rangi ya blue,
Angejilipua kwa bomu pale kwenye kundi la polisi, asingepona hata polisi mmoja pale.
Duh, mwandishi ajilipue mwenyewe, halafu polisi wamkamate polisi mwenzao kwa kumuua mwandishi !!!
Kwa naana nyingine, mwandish ajilipue mwenyewe, halafu Mafilili, Ritz na Zomba wa JF waende wakamkamate Mngony wa JF kwa kumuua mwandishi !!!
'Ajira' hizi hapa JF naona ziko zaidi ki-china china !!!
Hapo vipi ?? (huu msemo wa 'hapo vipi' ni kwa hisani ya Edward Lowassa)
 
mimi sio mpya ndani ya jamiiforums ila account hii ndo mpya! ungekuwa una uwezo mzuri wa kufikiria(IQ>100) usinge-draw conclusion eti mi mgeni kwa kuangalia account! two quite different thngs sucker!
upuuzi wako mwingne badala ya kujibu hoja unamuongelea mtu, toa hoja sio kukimbilia kuangalia account yangu haikusaidii kabisa! umri wa account na wewe kutoa jibu havitegemeani kabisa! shit!

Sijaona hoja ya kujibiwa pale. Halafu wewe nape ni au kibaraka wake. Ukitaka kumjua nape ni vile aking'ang'nia eti jibu hoja. Kuna hoja hapa!!?
 
hivi kabisa unadhani JK atatoa tamko lolote.....kwani mangapi yametokea katika nchi hii na rais hajatoa tamko lolote.
 
mimi sio mpya ndani ya jamiiforums ila account hii ndo mpya! ungekuwa una uwezo mzuri wa kufikiria(IQ>100) usinge-draw conclusion eti mi mgeni kwa kuangalia account! two quite different thngs sucker!
upuuzi wako mwingne badala ya kujibu hoja unamuongelea mtu, toa hoja sio kukimbilia kuangalia account yangu haikusaidii kabisa! umri wa account na wewe kutoa jibu havitegemeani kabisa! shit!

Wewe bangusilo sikiliza ITV live sasa hivi kwenye KIPIMAJOTO ujue idadi ya watu waliouawa na Polisi na wengine wala si kwenye vyama vya siasa.
 
nchi bila polisi haiendi... Subiri majibu ya jk hayatokuwa na tofauti na ya nchimbi... Hamtompata raisi mzuri kama yeye
 
Mh.raisi ni ushauri wangu mimi kama mtanzania kuwa unapaswa kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi wafuatao wakati uchunguzi unaendelea:-
1.Waziri wa mambo ya ndani
2.Mkuu wa jeshi la polisi nchini
3.RPC Iringa
4.Askari walioshiriki mauaji

Mh.raisi tafakari kilio cha watanzania wengi kutaka wahusika wachukuliwe hatua.Mh.raisi nafikia hatu ya kujiuliza hivi una moyo na roho ya aina gani kama kweli hutaonyesha kuguswa na jambo hili.Mh raisi wewe si mtanzani kama sisi tena unaonyesha kuguswa na misiba pale inapotokea kwani una rekodi nzuri sana ya kuhudhuria misiba.Mh rasisi kama unaguswa na misaiba ni kwanini basi usiguswe au uone uchungu kuona wauaji wanatamba mitaani?

Mh.raisi japo kamati ya uchunguzi imeundwa bado si sahhi kuona watu hawa wakiendelea na nyadhifa zao.Watu hawa wanapaswa kuwajibika kwa sasa kupisha uchunguzi.Mh.raisi kuchukua hatua kwa watu hawa kwa kiasi fulani itapunguza machungu miongoni mwa watanzania kuona serikali inaonyesha kujali.

Mh.raisi kama uliweza kuridhia waziri mkuu wako ajiuzulu inakuwaje kwa maofisa hawa inakuwa vigumu!

Mwisho, washauri wa raisi, mnaolipwa kwa kodi zetu, msaidieni bosi wenu kwa kutimiza wajibu wenu.

Hata wana ccm mnatakiwa kumshauri raisi kwa faida ya chama chenu.Msitake kuendelea kubaki madarakani wakati matendo yenu ni kinyume na dhamira yenu.

Umma wa watanzania haturidhiki na namna nchi inavyoendeshwa.
 
ushauli wako ni mzuri sana...je unamjua unayemshauli!binafsi naamini amiri jeshi mkuu anapenda zaidi propaganda hawezi kupokea ushauli wa maana,ukitaka kumfulahisha mwambie huu ni upepo tu utapita.
 
Back
Top Bottom