Rais wangu, hata kama sisi masikini huoni sifa ya misaada ni aibu? Ukoloni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wangu, hata kama sisi masikini huoni sifa ya misaada ni aibu? Ukoloni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jun 2, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  hakuna msaada wa Bure! Hii ni ishara dhahiri ya kuukubali ukoloni mambo leo na utumwa wa fikra. Kial hotuba unayotulete Mheshimiwa unatueleza sifa zako za jinsi unavyojua kuomba na kiasi ulichopata. ninajiskia kudhalilikia kabisa na fedheha. Je washauri wako hawakudokezei hali ilivyo huku mtaani? Hawakwambii mambo tunayotaka kusikia?

  Je ni kwa kiasi gani serikali imeweza kukushanya mapato, na ina mikakati gani ya kuwa na mapato ya kukidhi haja bila kuwa na pengo katika bajeti? Na je ni mkakati gani serikali yako inao utakaotupunguzia kero ya misaada. na je kweli hiyo misaada mfano zile fedha ulikuwa unatueleza zianatoka bank ya Afirka ni bure tu au ndo unatuachia madeni?

  Kila siku tunasikia unatuambia tumevuka malengo ya kukusanya kodi hii inamaanisha nini? Inaweaje kwenda sambamba na kuongezeka kwa misaada badala ya kupungua? Hii ni aibu kweli kweli mheshimiwa dah, unaonaje hata kama umepata fedha hizo kwa kuomba ukatafuta namna ya kuizzungumzia, mfano ukaeleza mipango ya serikali iliyonayo an inavyoitekeleza. Na mwisho bila kutaja moja kwa moja ukawashukuru wahisani wanaochangia maendeleo badala ya kuweka picha ya serikali kuwa ombaomba dah!

  Hotuba yako haijatulia, kwa sasa ni kipindi cha kubadilisha mwandishi wa hotuba zako na kuhakikisha zina mvuto na zinakuwa sensitive enough kwa maswala yalivyo sasa. Sifurahiwi na jinsi unavyowasilisha zimepoa sana saaana na mambo mengine kama hayo ya misaada yanawasilishwa vibaya hayailetei serikali yako sifa huo ndio ukweli.
   
 2. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutopokea au Kutoomba Misaada kwa sasa halina Mjadala. Asipofanya hivyo atakuwa hana Serekali ya Kuendesha. Na Bunge litakuwa halina Bajeti ya Kujadili wala kupitisha.
  Najaribu kukisia itakuwaje...........! Sipati jibu.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
   
 4. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kweli Tz inaweza kujiendesha bila kuomba misaada, na kweli misaada ni ukoloni. Swali, je wewe kama raia wakawaida uko tayari kuvumilia mtikisiko japo kwa miaka michache pale tutakapoanza kusimama wenyewe? Tunaweza kosa sukari kwa wakati, dawa kwa wakati, mavazi kwa wakati, kutopata chakula kwa wakati, vifo vinaweza kuwepo, nk. HIYO YOTE NI KATIKA KUJIJENGEA UWEZO, KABLA HATUJAANZA KUJITOSHELEZA LATIKA KUJITEGEMEA! Uko tayari? Au unataka tujitegemee katika bajeti tu kama Kenya, huku teknolojia, projects, policies, siasa, nk. ni misaada toka nje? Je, misaada ni fedha tu?
  Tunaweza ila tukiwa wamoja na kuthubutu.
  Mungu wetu anaita!
   
 5. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kwani kipato chako kinawezaje kutosheleza mahitaji yako yote? Siunapanga matumizi yako kutokana na kipato. Sifa mojawapo ya serikali ilojaa rushwa ni mishahara minono kwa viongozi wa juu pamoja na wabunge ili kuwanyamazisha. Pia inakimbilia misaada. Ushawahi sikia pesa za misaada zimechunguzwa?
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Well said profesa kuna kitu ambacho hata mimi kinanipa shida kukielewa hivi bank ya afrika wanatupa misaada(grants) au mikopo(loan)?na Je kuna uhusiano wowote wa mkutano kufanyika tz na huu mkopo/msaada?
  Ifike mahali tuwe na mipango endelevu ya kujenga uchumi wetu kwa rasilimali zetu ambazo tumepewa na mungu coz kwasasa serikali mda mwingi mipango na hata kauli zao ni za kuomba misaada.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Unachofikiri mkuu si ambacho serikali yetu inafikiri, serikali yetu inafikiri kuomba misaada na kupewa misaada. lakini ukiangalia hata kwenye majimbo yetu, unaweza kuona wanajimbo huwa tunataka kupewa msaada na mbunge, tatizo ni kubwa sana.
   
 8. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nipo kijiweni mie, nasubiri maisha bora niliohaidiwa na chama Tawala.
   
 9. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Nitajie nchi 1, unayoifahamu isiyokuwa na madeni.

  Hakuna kitu so called "MISAADA", yote hayo ni mamikopo na tunalipa direct or indirect.
   
 10. b

  bohha Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mwezi nalipia kodi ya sh 50000 kutokana na mshahara wangu mdogo,Rais hasemi namna ya kuboresha mapato ya ndani ya nchi watumishi hasemi kodi yetu inttumika vipi? anajisifia kuomba misaada, Mikusanyo ya TRA wanayodai ni zaidi ya 50% yanaenda wapi tujiulize. Maoni yangu misaada siyo dili tujipange wenyewe sijawahi sikia nchi iliyoendelea kwa misaada.
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hotuba nzima kujisifia kuomba tangu G8..ADB zoote kuomba kuomba tuu aibu gani hii!!!!!
   
 12. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Ni aibu hata wewe kuyatamka haya tena.nilipoyasikia jana nilikaribia kutapika tafadhali usiendelee kuyajadili tena.kwa nchi yenye rasilimali kama yetu ni wehu mkubwa kuzungumzia misaada tena kwa passion kama huyo jamaa alivyofanya
   
 13. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Chukua Marekani ambayo ina deni inalosumbuka kulipa zaidi ya dola 14,000 billion. Kwanini hizo pesa za misaada wasitumie kulipa madeni yao? Hizi pesa tunazopewa siyo misaada. Ni mikopo. Tutauza asilimali na kulipa madeni daima kwa mtaji huu wa serikali ya CCM
   
 14. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Sasa kama alipata kura kwa wizi na rushwa unategemea nini?
   
 15. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Next time atajisifia kwa kuomba kenya,uganda,rwanda,msumbiji,south africa,egypt, nigeria na angola kwa sasa libya wameblock misaada yao kwa jk kwa kutowatambua waasi
   
 16. U

  UNO Senior Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i had the same thought. Inakuwaje??? Hivi hana washauri? Ina maana tunatamba kupata msaada nje?? Hakuna msaada wa bure. Tutalipa mpaka na vitukuu. Hesabu hela zote zilizoliwa kila kona; ni asilimia ngapi ya hiyo misaada? Mungu ibariki tanganyika
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu hili swala linahitaji ufafanuzi wa kutosha kuhusu misaada ambayo tunaambiwa na mwisho wa siku inaongeza deni. Hivi kama unaomba mkopo kuna haja ya kumshobokea Credit Officer?Kuna haja ya wananchi kuelimishwa tofauti kati ya Msaada na Mkopo.
   
 18. T

  Tata JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wangetumia askili zao mwaka 1992 wasingelitupilia mbali Azimio la Arusha bila kuelewa mantiki nzima ya azimio lile. Wangejipa muda kulielewa na kutafakari kwa kina wangetupa siasa ya UJAMAA ila wasingeachana na KUJITEGEMEA kwani kujitegemea hakuna siasa. Kingine ambacho walikitupa bila tafakuri ya kina ni suala la Maadili ya uongozi ambayo kutokuwepo kwake kumeliingiza taifa kwenye kansa ya rushwa na ufisadi. Bahati mbaya kwa taifa hili watu waliacha kutumia vichwa kufikiri siku nyingi zilizopita. Kuna haja kama taifa kulirudia Azimio la Arusha na kuona ni mambo gani ya msingi kwa taifa yaliyomo kwenye azumio yanatakiwa kuwepo kwenye katiba mpya.
   
 19. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Unajua Tata, kuna kitu huwa kinaitwa sindicate au wengine wanaita wana mtandao, kukiingia utamaduni mbovu ndani ya kundi na wakakubaliana nao, basi kila kitu watakachofanya ni kulinda huo utamaduni.

  Lengo la kuua Azimio la Arusha ni moja tu, kujinufaisha binafsi bila kujali wanyonge waliowengi katika nchi ambayo bado inaendlea. na hii ni pamoja na kuwaka mianya ya wizi, Ubwanyenye, Ubwana na Utumwa, na Kuahkikisha watu wanajitajirisha na kujilimbikizia mali hata isivyo halali na kuondoa uwezekano wa kuulizwa na mtu yeyote yule, ikiwemo kuzipotosha sera na taratibu, na kutakatisha ubadhilifu.

  Na mwanya huu ni rahisi kuupata pale ambapo, walioelimika ni wachache na wachache haop wanashawishika na wana dhamana kubwa na wana uwezo wa kufanya hivyo bila kuhojiwa. Kwa sasa hali ya mambo ni tofauti, nadhani baadhi ya misingi mizuri inayofaa kutumika inaweza kurudishwa, kama si na kiongozi mwenye nia njema na ncho hii kituoka CCM basi ni upinzani.

  China, Venezuela na nchi nyingine ambazo zianfanya vizuri kwenye ubora wa maisha wa watu wake kwa usawa na wingi wao, wametumia misingi kama hii. Ukiona Magharibi wanahangaika na wewe, ujue wewe ni tishio unadalili za kuwapita kwa ubora, na ni jambo wasingelipenda kwakuwa linahatarisha nafasi yao ya kuendelea kukunyonya.
   
Loading...