Rais wa Zanzibar Dr. Shein atuea makadhi watatu wa mahakama ya kadhi

Mtumbatu

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
362
170
Wakati Wanatanganyika wanasua sua na mahakama ya kadhi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa makadhi wa mahakama ya kadhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee uteuzi huo unaanza Julai 06 mwaka 2013.

Dkt. Shein amefanya Uteuzi wa Makadhi Watatu wa Wilaya kupitia uwezo wa Kisheria chini ya kifungu


Namba 5 cha Sheria ya Mahkama ya Kadhi Namba 3 ya mwaka 1985 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya mwaka 2003.

Makadhi hao ni Sheikh Othman Ame Chum, Shekh Abdulrahman Omar Bakar na Sheikh Khamis Kassim Haji.
Uteuzi wa Makadhi hao Umeanza Juni 06 mwaka huu.

Imetolewa na
Idara ya Habari Maelezo, Zanzibar
10/06/2013
 
Duh, kumbe ni serikali ndio inatakiwa kumteua Kadhi! Sasa kwa nini Bakwata inalalamikiwa? Je itakuwaje Raisi akiwa ni Kafir, ataweza kufanya teuzi hizo?
 
Haha haaaaa!ni zanzibar tu au na bara?je rais akiwa mkristo atamteuaje?du znz ni noma.
 
""Kadhi court is very impotant in Tanganyika thats why we need it""
Who is saying those courts are not important? What are saying is that the Government of Tanganyika shoukd back off as those courts are not government organs but have to do with religious issues. Tanganyika is not an Islamic state.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
ndo maana tunataka wajisimamie, hawa jamaa ndio sourc ya udin hapa tz!!! waende zao huko.... maana hata waislam wa bara wanatuita maqfir.!
 
Masuala ya dini yanapaswa kuachiwa wenye dini kuteuana..
Sasa endapo raisi atakuwa MKRISTO atawateuaje hao makadhi, ya KAISARI MPENI KAISARI NA YA MUNGU MPENI MUNGU..

Mambo ya dini tuwaachie wenye dini na mambo ya serikali tuwaachie serikali..

Kwa hiyo nataka kujuzwa SERIKALI YA ZANZIBAR INAWALIPA MISHAHARA HAO MAKADHI?

Kama inawalipa je hela hizo ni pamoja na ule mgao unaotoka bara kwenye kodi za bia,bangi,makahaba, nk!
 
Duh, kumbe ni serikali ndio inatakiwa kumteua Kadhi! Sasa kwa nini Bakwata inalalamikiwa? Je itakuwaje Raisi akiwa ni Kafir, ataweza kufanya teuzi hizo?
Hili swali lako limenifanya nifikirie mara mbili mbili
 
We muslims...Halafu bora utumie ID nyengine tu katika mijadala kama hii...Maana napata wasiwasi wewe ndio huwa unanipiga Ban katika hizi mada...Come on..yani hutakiwi kuchangia kwa style hii
Kaaaazi kwelikweli!
 
ndio nasema nchi kama haifati dini ni tatizo kubwa

lazima dini ziwaongoze wenye kufata kama sihivyo tutapendelea wapagan
na kujenga taifa la wanamuziki tena wajinga wasiomjua mungu na kufa kijinga kisha viongozi kwenda misibani kwao
waislam wapewe uongozi wao na mamlaka yao yenye mipaka na wakristo hivyo pia
serekali imonitor tu kushughulia taifa bora
 
Back
Top Bottom