Rais wa Zanzibar Dr Shein ashiriki MAZISHI YA ALIYEKUWA MWANASHERIA MKUU Wolfgang Dourado | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa Zanzibar Dr Shein ashiriki MAZISHI YA ALIYEKUWA MWANASHERIA MKUU Wolfgang Dourado

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tuesday, March 20, 2012

  Rais wa zanzibar dr shein ashiriki MAZISHI YA ALIYEKUWA MWANASHERIA MKUU WA KWANZA WA ZANZIBAR Wolfgang Dourado.  [​IMG]
  Marehemu Jaji Dourado
  [​IMG]
  [​IMG]


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiweka shada la Mauwa katika kaburi la marehemu Wolfango Dourado,aliyekuwa Jaji Mkuu na mwanasheria mkuu Mstaafu wa Zanzibar,huko mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo. Picha na Ramadhan Othman IKULU.
  ===== ====== ======  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein leo ameshiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 Wolfgang Dourado ambaye alifariki dunia jana katika hospitali ya Zanzibar Medical Group Vuga mjini Zanzibar.
  Katika mazishi hayo ambayo yaliwashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd yalitanguliwa na Sala maalum ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa la Minara Miwili Shangani Mjini Zanzibar.
  Akitoa Salamu za Rambi Rambi kwa niaba ya Serikali kufuatia kifo hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais amesema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwa kumpoteza mtu ambaye alikuwa muhimu katika kutoa michango yake katika utayarishaji wa sheria na maamuzi ya kimahkama jambo ambalo halitasahaulika milele.
  Amesema kifo hicho si cha wanafamilia pekeyao bali ni kwa taifa zima la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa ambao alikuwa akiutoa hata kabla ya awamu ya kwanza ya utawala hadi kilipomfika kifo chake.
  Aidha Waziri Aboud ameiomba familia ya Marehemu Dourado kuwa na subra katika kipindi hiki cha msiba na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo bega kwa bega na wanafamilia hao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
  Marehemu Wolfgang Dourado alizaliwa Zanzibar Septembar 20 mwaka 1929 na kupata Elimu yake katika Skuli iitwayo St. Joseph Convert ya Zanzibar katika mwaka 1939-1946
  Mnamo Mwaka 1947-1950 Marehemu Dourado alianza kazi Serikalini kama Karani wa Ardhi ambapo mwaka 1952 alihamishiwa Afisi ya Mrajisi Mkuu wa Serikali na mwaka 1954 alipewa Cheo cha Msaidizi Mrajisi Mkuu.  Mwaka 1954-1957 alipelekwa Uengereza kwa masomo ya juu na aliporejea masomoni alishika nafasi mbalimbali za uongozi kama vile Permanent Hospital Home Affairs,External Affair and Trade na hatimaye kuwa Mwanasheria Mkuu na Mrajisi Mkuu wa Zanzibar.

  Nyadhifa nyengine alizowahi kuzishika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uhamiaji,Bodi ya Kodi na Bodi ya Bima Zanzibar na lakini pia katika Shirika la Bima Zanzibar Marehemu alikuwa Meneja Mkuu.


  Mnamo mwaka 1983 Marehemu Dourado aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria na Mwaka 1996 akiwa tayari amestaafu katika Utumishi aliteuliwa pia na Rais kuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar na hatimaye kuwa Naibu Jaji Mkuu.


  Aidha Marehemu aliwahi kukabiliana na kesi nzito nzito zikiwemo zile zilizohusu mapambano ya Juni 1961, kuuwawa kwa Marehemu Mzee Abeid Aman Karume 1972 na kushiriki kama Mjumbe wa Tume ya Rais inayoshughulikia mambo ya Siasa 1991


  Marehemu Wolfgang Dourado ameacha Mjane.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Walisema Mengi kuhusu Wolfgang Dourado; kumbe alibaki Zanzibar Mpaka Mauti yake...
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bwana Dourado, amefariki dunia leo: Dourado atakumbukwa sana kwa msimamo wake mzito sana kuhusu Muungano hasa enzi za Awamu ya Kwanza.

  - MUNGU AMREHEMU NA KUMSITIRI!

  fmEs!
   
 4. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake
  lihimdiwe
   
 5. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,285
  Likes Received: 3,015
  Trophy Points: 280
  Sisi sote ni wa Allah na kwake tutarejea.
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  R.I.P tukisubiri hukumu yetu mbele ya HAKI
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  R.I.P mwanamapinduzi na mzalendo Daurado.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2015
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kumbe? sasa mbona wansema alifukuzwa!
   
 9. G

  George Anthony Member

  #9
  Apr 8, 2015
  Joined: Mar 21, 2015
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Marehemu alale mahali pema peponi
   
Loading...