Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi anatangaza Baraza jipya la Mawaziri. Hakuna Manaibu Waziri

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,283
2,000
Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi yupo mubashara Channel ten anatangaza baraza jipya la mawaziri.

Baraza la mawaziri limetangazwa lakini Wizara mbili zimebaki wazi na uteuzi utafanywa baadae nazo ni Wizara ya afya na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Rais Mwinyi amesema kwa sasa hakutakuwa na Manaibu Waziri na endapo siku za mbele itajitokeza wizara itakayoonyesha umuhimu wa kuwepo naibu waziri basi atateuliwa.

Kuhusu wizara mbili kuwa wazi ni kwamba ACT wazalendo hawajapeleka majina kwa mujibu wa katiba na wala wawakilishi wake hawajala viapo hivyo wanasubiriwa.

========


BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ZANZIBAR:

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji - Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora - Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi - Dokta Khalid Mohammed Salum.

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo - Soud Nahoda Hassan.

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni - Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri.

10. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi - Riziki Pembe Juma.

11. Wizara ya Maji na Nishati - Suleiman Masoud Makame.

12. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

13. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale - Lela Mohammed Mussa.

14. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi - Abdallah Hussein Kombo.

15. Wizara ya Ujenzi - Rahma Kassim Ali.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,894
2,000
Kama Seif na watu wake wakikubali kujiunga kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa naona bora safari hii wachukue na kadi za CCM kabisa, ili next time wasiwasumbue wananchi kwenda kupiga kura na kuwasababishia makovu na vilema.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,283
2,000
Kama Seif na watu wake wakikubali kujiunga kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa naona bora safari hii wachukue na kadi za CCM kabisa, ili next time wasiwasumbue wananchi kwenda kupiga kura na kuwasababishia makovu na vilema.
Waache wazanzibar wajiamlie mambo yao bwashee!
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,223
2,000
Hahahaaaa......serikali inabana matumizi bwashee.

Sisi tutaendelea kukitumikia chama.
Ila kweli,zanzibar naibu waziri wa nini.

Hata hao wawakilishi ni wengi sana aisee.

Ilikuwa zanzibar wawakilishi wachache wanatosha, sehemu ndogo sana hii.

Yani nchi ambayo ukubwa wake ujirrudirle mara kadhaa ndo ufikie ukubwa wa mkoa wa lindi ati ina wawakilishi kibaoo.

Nchi ambayo watu wake idadi ni ndogo kuliko idadi ya watu wa daresalam ati ina wawakilishi kibaoooo
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,453
2,000
Mungu ndiye mpaji!
Amina Bwashee. Wengine wooote wanajivunia Oksijen anayotoa bure japo inawapa kiburi na kuona wenzao hawana haja ya kuivuta hiyo Oksijen anayotoa mpaji. Ila kwake kila goti litapigwa na kila Ulimi utakiri yeye ni Bwana. Ukiua kwa Upanga utakufa kwa upanga.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,128
2,000
Kama Seif na watu wake wakikubali kujiunga kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa naona bora safari hii wachukue na kadi za CCM kabisa..
It is just a matter of time na watajiunga tu hawa. Jusa kishalidokeza hilo.

CUF ya Maalim Seif walisusa kipindi cha 2015-2020 na surely watakuwa wameshaonja radha ya zote mbili: kuwa nje ya ulingo wa siasa kwa miaka mitano na kuoperate ndani ya SUK.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom