Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi amemteua Nassor Mazrui na Omar Said Shaaban kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Mwendo wa wasaliti kula vyeo huku wafuasi na wanachama wao wakiendelea kuuguza majeraha , maumivu ,vipigo , majonzi , vifo , vifugo ,kesi , nk.
 
Watanganyika mambo Wazanzibar waachieni wenyewe.

Yakwetu yanatushinda, sasa hivi hakuna Polisi anaweza kumkamata Maalim Seif, kwahiyo wana nafasi ya kufanya harakati zao wakiwa serikalini bila kubughuziwa na mpaka IGP Sirro sasa hivi atalazimika kumpigia saluti Maalim Seif.

Mimi naamini wamejitafakari kwa kina sana kabla ya kufikia maamuzi, Wazanzibar wako tofauti sana na Watanganyika, kama kuna anayefikiria hawa wanafuata pesa serikalini anajidanganya na mtashangaa kuona ccm na ACT wanaungana kudai Zanzibar yenye mamlaka.

Kwenye ajenda ya Uzanzibar hawa jamaa ni wamoja, na hasa baraza la mawaziri la Magufuli kutoteuwa waziri kamili hata mmoja nalo ni bomu linasubiri kulipuka tu.
Umetafakari na umetoa ubashiri ambao naamini utakuwa kweli tupu

Huyu Mwinyi hata CCM bara wataanza mstukia hivi sasa, kwa kuwa amewachukua vigogo wote wa ACT Wazalendo na kuwapa nyadhifa serikalini!

Tofauti na huku Bara ambako Magu amehakikisha hakuna kigogo yeyote wa Chadema aliyepenya kwenye ubunge na wala hafikirii kuwapa nafasi zozote za uteuzi serikalini
 
Watanganyika tulijisahau na kudhani ili uwe ushike Dola ni lazima upange safu yako kuanzia Urais hadi mawaziri kumbe sivyo.
Kumbe kuwemo ndani ya Dola ndio njia sahihi ya kuizoesha Dola kukuamini ili uishike siku zijazo.
Vyama vya siasa vya Tanganyika viombe hili libadilishwe ili navyo viwe miongoni mwa wenye kushika Dola.
Bado havijachelewa muda dio huu..
 
Inawezekana wazanzibari wamekaa kama wazanzibari na wameamua kuachana na mambo ya hao machogo watanganyika. Tusiwabeze sana, nchi yao ikitulia basi ni afueni kwetu. Tuwaombee tu wafanikiwe.

Amandla...
 
Unaweza kukuta lawama zote wametupiwa machogo. Utasikia waliopiga, waliowafunga n.k. ni machogo. Kwa hiyo tuachane nao sisi tuendelee na safari yetu ya mamlaka kamili ambayo ki ukweli ni kujitenga na Tanganyika. Waliokula hasara hapo ni machogo wa ACT-WAZALENDO.

Amandla...
 
Hii ni taarifa kutoka Zanzibar iliyotufikia hivi punde , kwamba Dr Hussein Mwinyi ameteua Ndugu Nassoro Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo pamoja na Mwanasheria wa Chama hicho Omary Shaaban kuwa wajumbe wa baraza la Wawakilishi .

Huu ni muendelezo wa mambo ya SUK .

Tunawatakia kila la heri

====

Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amemteua Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Nassor Ahmed Mazrui na mwanasheria mkuu wa chama hicho, Omar Said Shaaban kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
View attachment 1644003
Hizi sasa ndio siasa za ukweli. Sio zile siasa za kususa susa.
Hongera sana ACT Wazalendo kwa kujitambua, hongera sana rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi kwa kuwa muungwana kama baba yako.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania..
P
 
2025 idadi ya wapiga kura sidhani kama itafika 50% ya hawa wa 2020, mwana yanayotokea ni matokeo ya yajayo.

•Note this comment.
 
Hizi sasa ndio siasa za ukweli. Sio zile siasa za kususa susa.
Hongera sana ACT Wazalendo kwa kujitambua, hongera sana rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi kwa kuwa muungwana kama baba yako.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania..
P
Kweli raisi wa zanzibar ni muungwana Kama baba yake
 
2025 idadi ya wapiga kura sidhani kama itafika 50% ya hawa wa 2020, mwana yanayotokea ni matokeo ya yajayo.

•Note this comment.
Ikiwa Rais Mwinyi atatawala kama alivyoahidi kwenye hotuba yake ya kufungua Baraza la Wawakilishi, bila ubaguzi wa aina yeyote, idadi itaongezeka na yeye na chama chake watashinda bila figisu figisu zozote. ACT wataendelea kuwa washika shela kama Fatma Karume alivyo tabiri. Ila asipotimiza ahadi zake, utabiri wako utatimia na wengi ambao hawatapiga kura watakuwa waliokuwa wafuasi wa ACT-Wazalendo. Itakula pia kwa ACT-Wazalendo. CHADEMA na CUF vitabakia kuwa vyama vya bara. CUF itarudisha wafuasi wake wa bara lakini sio Zanzibar.

Amandla.
 
Back
Top Bottom