Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi awasili Chato kwa ziara ya siku mbili

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,422
2,000
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi leo asubuhi Alhamisi Januari 14, 2021 amewasili Chato kwa ziara ya siku mbili.

Akiwa Chato Dk Mwinyi na ujumbe wake watakuwa na mazungumzo na mwenyeji wao, Rais John Magufuli.

Baada ya mazungumzo hayo Dk Mwinyi atatembelea soko la kimataifa la dagaa la Kasenda na kuzungumza na wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo.

Dk Mwinyi ametua katika uwanja wa ndege wa Geita-Chato na kupokelewa na waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani na Waziri wa Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad akiwa njiani kuelekea Chato ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigongo -Busisi mkoani Mwanza, ambalo limepewa jina la JPM na kuwataka wananchi kulinda miundombinu yake.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,509
2,000
Kweli kabisa hana, yaani Zito ndio anawahitaji hao wazenji kuliko kinyume chake.
Ndi hivyo.

Hata wangekuja CHADEMA, bado wasingekuwa na uwezo wa kuwaamulia chochote.

Wale wamejitosheleza
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
1,621
2,000
Tunasubiri pia mawaziri, wabunge na wakuu wa mikoa kutembelea kitovu cha utalii Tanzania.
Chato the chosen city!
Mwanzo wa hesabu ni moja! Na Magufuli si mtu wa maneno maneno tu, ni wa vitendo - ona sasa January hii tu, ni watu wangapi mashuhuri wamezuru Chato? Na wanakwenda huko wakiwa wamesheheni na watu wengine!

Huo ni mwanzo, na nyinyi mnaopinga kuendelezwa kwa Chato endeleeni kufanya hivyo, maana kupinga pinga ni njia mbadala ya kuitangaza Chato.

Na pia muendelee kusema uongo kwa wingi mnapo pinga! Mfano, mseme Magufuli amejenga jengo refu sana kuliko yote Africa au Duniani Chato!, muongeze kwamba tayari reli ya SGR kipande cha Chato imeisha anza kufanya kazi! Huu uongo utasaidia kuitangaza na utalii wa ndani na nje utainufaisha Chato.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom