Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amsimamisha kazi Mkurugenzi wa ZSSF

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Sabra Issa Machano na watendaji wengine kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya serikali.

Dk Mwinyi alitoa kauli ya kuwasimamisha watendaji hao wakati alipozungumza na viongozi na watendaji wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Victoria Garden, Vuga Jijini hapa.

Watendaji wengine waliohusika na hatua hiyo ni pamoja na Ramadhani Abdalla Ali pamoja na watendaji wa Kamati nzima ya Uratibu wa mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) kutoka Wizara ya Fedha.

Alisema amechukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF, Sabra Issa Machano pamoja Ramadhani Abdalla Ali kwa makosa ya kiutendaji katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Jumba la Treni liliopo Darajani.

Alisema ni dhahiri kuwa katika utekelezaji wa mradi huo taratibu zilikiukwa na hivyo akabinisha ulazima wa kufanyika uchunguzi, wakati ambapo watendaji hao wakiwa nje ya kazi.

Aidha, alisema hafurahishwi na utekelezaji wa mradi wa ZUSP uliogharimu dola za Marekani milioni 93, ambao ulikusudiwa kuondoa changamoto katika Manispaa.

Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuwepo makosa makubwa katika manunuzi pamoja na kufanyika udanganyifu juu ya kazi zilizoelezwa kufanyika, il-hali hazikufanyika.

Alisema amelazimika kuisimamisha Kamati nzima ya Uratibu wa Mradi huo ili uchunguzi uweze kufanyika, wakati wafanyakazi hao wakiwa nje ya kazi zao.

Pia, Dk Mwinyi aliagiza ZAECA kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Haidar Mussa Maisara anayetuhumiwa kushusha kiwango cha kodi katika tukio la kuingizwa Bandarini kichwa cha Scania, sambamba na Kampuni ya KEVIS aliyoagiza ifanyiwe uchunguzi.

Alisema mfanyakazi huyo alijenga dhamira ya kujihusisha na rushwa, ambapo kwa nyakati tofauti aliteremsha kiwango cha kodi hiyo hadi kufikia Sh milioni tano, fedha ambazo haziendani na thamani halisi ya kodi iliyopaswa kulipwa, ambapo hatimaye gari hilo lilitolewa usiku bila fedha hizo kulipwa.

Alisema anasikitishwa na miradi mikubwa jinsi ilivyogubikwa na matatizo makubwa kiasi ambacho haionyeshi thamani ya fedha zilizotumika.

Katika hatua nyingine Rais Mwinyi alisema tangu Serikali ya Awamu ya nane iingie madarakani imebaini kuwepo matatizo makubwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa, na hivyo akasisitiza dhamira ya serikali ya kuchukua hatua madhubuti.

Aidha, alisema kuna miradi mingine inayoonesha dalili za kuwepo mianya ya rushwa na hivyo akaahidi kuifuatilia pamoja na kuhakikishia ZAECA kuwa serikali imefungua ukurasa mpya wa mapambano dhidi ya rushwa.

Mapema Waziri wa Nchi (OR) Katiba, sheria, utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisema kuna ushirikiano mkubwa wa kiutendaji kati ya ZAECA na wenzao wa Tanzania Bara (Takukuru) kutokana na vikao vilivyofanyika, na hivyo akaahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa lengo la kudumisha Muungano.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Mussa Haji Ali alisema pamoja na taasisi hiyo kuasisiwa katika kipindi kifupi kilichopita, imepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake makuu matatu.

Chanzo: Habari Leo
 
Inatosha sasa. Ajikite kusimamisha maviwanda makubwa na sio kusimamisha wakurugenzi na watumishi wengine. Tatizo umeme wanategemea huku
 
Uandishi wa Tz! Sasa hayo majukumu huyo mkuu wa taasisi ya kuzuia rushwa hakuyataja?
 
Zanzibar haina Rais.Ukweli mchungu ni kwamba Mwinyi ni mkono wa bara!
87659087.jpg
 
Kumbe zanzibar kuna treni?,,wajitahidi basi hiyo nyumba ya treni ikamilike na ikibidi iwepo tren ya tube kutoka dar hadi zenji,ndani ya miaka hii mitano
 
Na Yeye nae yale Mauzauza ambayo ameyafanya kwa Kipindi kirefu katika Wizara Nyeti aliyoiongoza tena mengi sana nani atamshtakia kwa sasa?
 
Kumbe zanzibar kuna treni?,,wajitahidi basi hiyo nyumba ya treni ikamilike na ikibidi iwepo tren ya tube kutoka dar hadi zenji,ndani ya miaka hii mitano
Jumba la treni wanamaanisha zile nyumba zao ndefu (ni ndefu na nyembamba kama treni.)

Wazanzibar hebu nisaidieni kumuelewesha huyu ndugu juu ya jumba la treni.
 
Hussein Mwinyi anaibadilisha Znz kuacha kujifanya Busy na U Ccm ns ACT wakati kuna watu wanaogele kwny fedha z walipa kodi
 
Back
Top Bottom