Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi punguza sana Cheap Publicity ambayo naona inaanza kukuzoea sasa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kuna Mtu wako Mmoja wa karibu mno hasa kutoka Wizara uliyokuwa ukiiongoza huku Tanzania Bara kwa muda mrefu kanidokeza ya kwamba Role Models wako wakubwa Kiuongozi na ambao unawakubali sana ni aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama na Rais Mstaafu wa Tanzania kwa Awamu ya Nne Mzee Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Sikatai Mtu kuwa na Role Model au Role Models wake duniani kwani hata Mimi pia nilitamani kweli kweli kuwa kama Mchezaji wa Kifaransa japo ana Uraia wa nchi uliyowahi Kusoma pia ya Algeria Zinedine Zidane 'Zizzou' lakini nikajikuta sijafikia Malengo ya Kumuiga na kuwa kama Yeye hadi sasa nipo zangu tu hapa Kisiwani Pemba na Kazi yangu hii ya Kupara Samaki na Uvuvi pekee.

Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa takribani Mwezi sasa tokea uwe Rais huko nimeanza Kukuona ni Mtu unayependa sana Makamera na Kutupia Vitu vyako/ Mambo yako Mitandaoni. Na leo tena nimeona umetupia Picha uko ndani ya Ndege angani ukisoma Faili moja hivi kama vile alivyowahi kufanya Mzee Mwinyi na hata Rais Mstaafu wa Marekani Obama.

Ushauri wangu Kwako Mheshimiwa hebu punguza sana hizi mambo na fanya Kazi ngumu Kwanza ya Kuijenga vyema Zanzibar Isles, waunganishe vyema Wazanzibari na kazania mno masuala mazima ya Uchumi na Elimu zao na huko baadae Zanzibar yako ikikaa sawa sasa unaweza hata kuwa unatutupia Picha zako zingine ukiwa Dinning Room na Mkeo Bi. Mariam mnakula Kuku.

Na kuna Mtu Mmoja hivi wa juu yako Yeye mambo hizi huwa hapendi kwakuwa anataka awe Maarufu Yeye tu nchi nzima. Kuwa makini nae kabisa!
 
Ndugu yangu acha roho mbaya kumbuka nae ni binadamu anahaki ya kufanya kile ambacho kinafaa kufanywa na wengine acha usitulete tabia zako km mapaka ya bar
Nimemshauri na hakuna mahala ambapo nimemlazimisha.
 
Kuna Mtu wako Mmoja wa karibu mno hasa kutoka Wizara uliyokuwa ukiiongoza huku Tanzania Bara kwa muda mrefu kanidokeza ya kwamba Role Models wako wakubwa Kiuongozi na ambao unawakubali sana ni aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama na Rais Mstaafu wa Tanzania kwa Awamu ya Nne Mzee Dk. Jakaya Mrisho Kikwete....
Wivu unakusumbua ndugu.
 
Ukishakuwa Rais mambo kama hayo huwa hayakwepeki.

Picha kama hizo huwa zina nafasi yake mkuu.
 
Kuna Mtu wako Mmoja wa karibu mno hasa kutoka Wizara uliyokuwa ukiiongoza huku Tanzania Bara kwa muda mrefu kanidokeza ya kwamba Role Models wako wakubwa Kiuongozi na ambao unawakubali sana ni aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama na Rais Mstaafu wa Tanzania kwa Awamu ya Nne Mzee Dk. Jakaya Mrisho Kikwete..
ko wee una force au unataka Mwinyi afanane na magu?

Kila mmoja kazaliwa, kalelewa na kukulia mazingira ya namna yake, hii huchangia kila mtu kuwa na tabia yake binafsi.

Ko Mr. usiforce watu wafanane wakati ni kitu ambayo haiwezekani kamwe.
 
Kuna Mtu wako Mmoja wa karibu mno hasa kutoka Wizara uliyokuwa ukiiongoza huku Tanzania Bara kwa muda mrefu kanidokeza ya kwamba Role Models wako wakubwa Kiuongozi na ambao unawakubali sana ni aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama na Rais Mstaafu wa Tanzania kwa Awamu ya Nne Mzee Dk. Jakaya Mrisho Kikwete....
Bado anajifunza urais
 
Kuna Mtu wako Mmoja wa karibu mno hasa kutoka Wizara uliyokuwa ukiiongoza huku Tanzania Bara kwa muda mrefu kanidokeza ya kwamba Role Models wako wakubwa Kiuongozi na ambao unawakubali sana ni aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama na Rais Mstaafu wa Tanzania kwa Awamu ya Nne Mzee Dk. Jakaya Mrisho Kikwete...
Mie sijakuelewa hata kidogo. Ulitaka kumaanisha nini katika andiko lako?
 
Unajua ukitupia kapicha fb istagramu au mtandao wowote ule halafu wezako wakalike unafurahi na ukifurahi unaondoa msongo wa mawazo , unaondoa uchovu, mwilini, unapata nguvu mpya ya kufanya kazi hata maraisi ni binadamu pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom