Rais wa Zanzibar aagiza Meli zote za Serikali ziuzwe kwa vile hazileti faida

Kuna haja ya kubadili mifumo ya nishati ya meli za serikali. Serikali iangalie uwezekano wa meli zote mpya zinazojengwa ziwa Victoria, Tanganyika na bahari ya Hindi kutumia nishati ya gesi ambayo ni nafuu sana ili meli hizi zianze kuendeshwa kwa faida.
Mwinyi pia angefanya 'last attempt' kwa kutenga fedha na kununua gas fired engines na kufunga kwenye baadhi ya meli, hasa zile ambazo ni mpya-mpya aone kama ufanisi utaongezeka kwa kupugua kwa gharama ya nishati.
Gas is our future...
Meli karibu zote za kisasa duniani zinatumia heavy diesel oil.
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?
Hiyo ndiyo faida ya ushindani wa kibiashara. Kama hutoi huduma nzuri unawekwa pembeni automatically. Hata kwa serikali ya JMT hizo ndege za ATCL zilitakiwa ziwe na competitors ili tuchague kilicho bora, lakini walianza kuwakaba shingo private investors ili wabaki wao. TBC yenyewe haiwezi kujiendesha, watu hawana interest na programs zake. Rais Hussein Mwinyi yuko sahihi kabisa.
 
Tatizo kuwa viongozi wa mashirika huchaguliwa na raisi hakuna kuangalia kama wana weledi wakazi au laa.
Hata kama shirika linakula hasara hakuna kupunguza watu kazi hakuna kufukuzwa mtu.
Ukiwa na weredi sio rahisi ufanye kazi kwa mshahsra wa 15 million labda uwe na mpango wa kwenda kuiba.

Top management staffs in top private sector companies mshahara ni zaidi ya 20,000 + US dollars.
 
Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Kitu ninachojiuliza ni kwamba tuliaminishwa ATCL ilikuwa inaingiza faida kwa maana mpaka inatoa gawio kwa serikali, lakini kinachoshangaza papo hapo tunaambiwa ATCL imeingiza hasara ya mabilioni kwa serikali!
Alichokiamua Rais Hussein Mwinyi ni bora mara 50. Ndio ziuzwe ikiwezekana zinunuliwe boti ndogo za biashara.
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?

Nasikia aibu; sasa shirika la ndege ndo kituko, wanadaiwa zaidi ya asset zao that means shirika doesn’t exist
 
Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Nipate pesa, nijiandae kununua ndege za serikali, maana najua bado ni mpya na zitauzwa kwa bei che.
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?
Ndio, kwasababu huwezi kuniambia nisipande Azam au Zanzibar One eti nipande MV Mapinduzi 2! Then angalia jinsi Azam alivyodorminate hiyo biashara, usafiri wa uhakika unaokwenda na muda pia sasa hiyo MV Mapinduzi ya Serikali umeiona ilivyo?!
 
Hata ningekuwa mimi ndio Rais wa Muungano ndege zote ningekodisha kwa mashirika binafsi au serikali yanayojitahidi afu nasubilia changu.

Soon sgr itakuwa hivyo hivyo hasara ,wataleta mwekezaji atasema sipati faida yaani tuendako itakuwa maumivu Sana.

Kama sgr ya Mombasa Nairobi ambayo iko kwenye main transport corridor inaleta faida ndogo au hasara sembuse sgr ya kwenda Mwanza ambako hata mizigo ya kubeba ya maana hakuna
Je,Kuna umuhimu wa serikali kuendelea na mradi wa bandari ya Bagamoyo ili kufanya mradi wa SGR kuwa wenye tija?
 
Serikali kufanya biashara siku zote ni maumivu
Labda washirikiane na mtu binafsi
Ila wakiwa wenyewe ni hasara tupu,upigaji nk

Ova

Ila wao wanapapara ya kuwabambika wenzao makodi wanapowaona wanafanya biashra vizuri
 
Hiyo ndiyo faida ya ushindani wa kibiashara. Kama hutoi huduma nzuri unawekwa pembeni automatically. Hata kwa serikali ya JMT hizo ndege za ATCL zilitakiwa ziwe na competitors ili tuchague kilicho bora, lakini walianza kuwakaba shingo private investors ili wabaki wao. TBC yenyewe haiwezi kujiendesha, watu hawana interest na programs zake. Rais Hussein Mwinyi yuko sahihi kabisa.
Tunataka ubepari lakini tunaendesha nchi kijamaa wakati huo huo tunataka kuendesha mashirika kibepari.

Full of contradictions, we should make a choice either we sell all public assets or we retain them.

It's a failure which most of the former socialist countries are in that catch. We invariably retake the companies which we unloaded off yesteryears.
 
Hata ile meli 'mpya' ya MV Mapinduzi II ya mwaka 2015 tayari ni chakavu bila kusahau meli ya MT Mkombozi II maalum kama tanker ya mafuta muda mwingi imetia nanga bandarini Malindi Zanzibar bila kupiga kazi!.

8 August 2019
MT Ukombozi II meli mpya yatinga Zanzibar

MV MAPINDUZI II , meli mpya inayoendelea kukumbwa na changamoto zisizoisha

Source : Hilmi Hilal
https://www.balticshipping.com › imo
MAPINDUZI II, Passenger vessel, IMO 9708485 - BalticShipping.com
MAPINDUZI II is a Passenger vessel built in 2015. Currently sailing under the flag of Tanzania. Formerly also known as POSCO PLANTEC 13SV01

Mimi wananimaliza hayo majina ya hayo meli zao, MAPINDUZI, MKOMBOZI Hopeless kabisa hawa jamaa
 
Ila wao wanapapara ya kuwabambika wenzao makodi wanapowaona wanafanya biashra vizuri
Si wanajua hata wakitumia pesa ovyo
Wao watazirudisha kwa style nyingine

Wakati umefika na wao serikali na vyombo
Vyao wasimamie vizuri,pesa na matumizi za pesa wanazozikusanya

Ova
 
Baada ya kuuza meli,wafumue pia na mfumo mzima wa usimamizi wa meli.Kama hakuna tija maana yake ni kwamba utendaji ni hovyo.
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?
Kwanza ni meli za nini? Mizigo tanker abiria uvuvi? Hasara inatoka wapi? Mikopo madeni uendeshaji au meli nzee? South Korea uchumi umeshikwa na meli, Sweden shirika la maersk ni roho ya uchumi wao, sie tatizo nini hasa?
 
Back
Top Bottom