Rais wa Zambia awataka viongozi wa umma kutangaza mali zao

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
[h=2]Rais wa Zambia awataka viongozi wa umma kutangaza mali zao[/h] Rais mpya wa Zambia awataka viongozi wa umma kutangaza mali zao hadharani na aahidi kupambana na rushwa na umasikini.






PNN_Michael-Sata_480X300.jpg
Picha AP
Rais mpya wa Zambia Michael Sata


Rais wa Zambia Michael Sata amerudia wito wake wa kupambana na rushwa. Akizungumza bungeni Ijumaa rais huyo mpya aliahidi kuchukua hatua za kupambana na rushwa wa kuwataka viongozi wa umma kutangaza mali zao hadharani.
Bw. Sata aliahidi pia kuchunguza tuhuma za rushwa za uongozi uliopita. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 alipata ushindi mkubwa dhidi ya kiongozi wa zamani Rupiah Banda katika uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita, akiwaambia wapiga kura kuwa atawasaidia masikini wan chi hiyo na kupambana na rushwa.
Awali mwezi huu Bw.Sata alimbadilisha Afisa wa juu wa kupambana na rushwa katika mlolongo wa hatua za kuisafisha serikali yake kutokuwa na mahusiano yeyote na mtangulizi wake.
Bw.Sata amerudia mara kadhaa shutuma kwamba Bw.Banda kwa kuvumilia rushwa na hakufanya vya kutosha kuhakikisha raia wengi zaidi wa Zambia wanapata kiasi cha utajiri wa shaba wa nchi hiyo
 
na wakwetu wangefanya ivo ingekua poa sana na pengine na cc tungeondokana na tanzagiza milele
 
na wakwetu wangefanya ivo ingekua poa sana na pengine na cc tungeondokana na tanzagiza milele

hapa kwetu unakuta kiongozi kwenye file ana gari moja na kijumba kimoja lakini kwenye ukweli ni tajiri wa kutupwa..
 
wakwetu ukimuuliza sana anasema yeye sio Mungu, mara hajui tena hajui... ukizidi kumbaba anaanguka!!!
Na kukanusha kwa kumtumia Salva kuna siku watajichanganya, atamkanusha mpaka Riz1 sio wake.
 
Na kukanusha kwa kumtumia Salva kuna siku watajichanganya, atamkanusha mpaka Riz1 sio wake.
au kusafiri kabisaaaaaaaaaaaa, anawaachia mtajiju wenyewe

naona Pinda nae kaamua kurithi safari
 
wakwetu ukimuuliza sana anasema yeye sio Mungu, mara hajui tena hajui... ukizidi kumbaba anaanguka!!!

Halafu hakawii kuzua safari ili kukimbia matatizo nchini na huku akiwa na bakuli lake la ombaomba na wakati mwingine hujifanya kwenda kushughulikia matatizo ya nchi nyingine za Afrika wakati ya nchini yamemshinda kuyatatua.
 
jamaa wa zambia anawafundisha viongozi walio madarakani kwamba wajiandae tu kwani anayofanya ni appetizer kwa wapinzani kwa nchi za sadc

but in our country kama cdm wanataka nchi, basi they need to bolster their squad, hasa kwenye timu ya kuwasaidia waliopo, kwani ni wachache sana na wanabeba mizigo mikubwa sana
 
Kuna kipindi huwa nawaza baadhi ya viongozi wetu sio raia maana hawana uchungu na nchi!
 
Back
Top Bottom