Rais wa Zambia atoa amri ya kufunga mpaka wa Tanzania na Zambia

Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,405
6,280
Leo tarehe 10/05/2020 Rais wa Zambia Edgar Chagwa lungu ametoa amri ya kufunga mpaka wa Zambia na Tanzania (Nakonde) na kupiga marufuku mtu yeyote pamoja na magari au treni kuingia na kutoka Mji wa nakonde.

Mji wa nakonde umepakana na mji wa tunduma ambapo ndo mpaka wa Tanzania na zambia ulipo.

Raisi Lungu amefikia maamuzi hayo baada upimaji wa Covid-19 uliofanyika juzi na kungundua watu 76 wana maambukizi ya virusi vya Corona katika mji wa Nakonde. Hiyo idadi imejumuisha wafanyakazi wa mpakani, afisa uhamiaji, wafanyakazi wa lodge na madereva wa kitanzania (18).

Kwa sasa Nakonde imetangazwa kua kitovu (epicenter) ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona. Hivyo basi Lungu kaona isiwe shida kama jirani anaona watu wake wafe freshi tu ila Corona mbaki nayo huko huko Tanzania.

Tunapoelekea Tanzania mtatengwa. Yani hamtoruhusiwa kuingia nchi yeyote ile Africa na Dunia nzima.

Swali la msingi la kujiuliza Je Lungu nae ni kibaraka wa Mabeberu?

InShot_20200510_150424055.jpg
InShot_20200510_150351273.jpg

========

Zambia shuts border with Tanzania over virus spread fears

May 10, 2020: Closure of border with Tanzania

The Zambian government has announced the closure of its common border with Tanzania. On Saturday (May 9) 76 new cases were reported in Nakonde, the border town in question.

The president directed that with effect from Monday 11th May, 2020; “the Nakonde border will be temporarily closed. There shall be no traffic in and out of Nakonde,” Health Minister Chitalu Chilufya announced at a COVID-19 press briefing on Sunday.

The measure is to facilitate the roll out of targeted interventions. During the time, immigration staff at the border will be trained and retrained on how to safely deal with entry of persons and goods.

Redeployments and reinforcements will also be undertaken, whiles Personal Protective Equipments and quarantine facilities and other key logistics will reinforced with the view to protect the lives of officials and the people of Nakonde.

Zambia’s case stats as of today stands at 267 confirmed cases with 117 discharges and 7 deaths. Tanzania on the other hand has 509 cases, 21 deaths and 183 recoveries, according to John Hopkins University tallies.

Tanzania’s overall response to the pandemic has been a mix of controversy. From president Magufuli casting doubts on the efficacy of test kits, refusal to implement measures such as curfew or lockdowns and reported cases of midnight burials.

Govt of Zambia orders temporary closure of border with Tanzania from tomorrow.

This after 76 Covid-19 cases were reported at Nakonde – the border town with Tanzania.

Total number of cases in the Country stands at 267.
 
Tuttyfruity,

Je, kwan kuna tatizo na Zambia kufunga mpaka wake? Mbona nchi nyingi tu duniani zimefunga mipaka na nyingine kuwafungia watu wao ndani (lockdown)!

Hamkosi la kulaumu ila mjue ukweli kwamba malengo yenu hayafatanikiwa kama hambadiliki kimawazo mkaungana na WaTz wengine kwa maendeleo bila kujali kabila, dini, jinsia, elimu, madaraka, kipato na siasa.

Kwa pamoja Tanzania bila COVID-19 yawezekana. Mimi, wewe, yeye, wao:-
JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO
 
Wazee wa buku7 mmekuja. Povu la nini hiyo ni taarifa tu. Mimi binafsi nnaunga Juhudi za Rais wetu mtukufu.
 
Je, kwan kuna tatizo na Zambia kufunga mpaka wake? Mbona nchi nyingi tu duniani zimefunga mipaka na nyingine kuwafungia watu wao ndani (lockdown)!

Hamkosi la kulaumu ila mjue ukweli kwamba malengo yenu hayafatanikiwa kama hambadiliki kimawazo mkaungana na WaTz wengine kwa maendeleo bila kujali kabila, dini, jinsia, elimu, madaraka, kipato na siasa.

Kwa pamoja Tanzania bila COVID-19 yawezekana. Mimi, wewe, yeye, wao:-
JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO

So far tumeshapima wananchi wangapi?

Tuwekee statistics hapa mkuu.
 
Zambia will never survive without Tanzania ni suala la muda tu watafungua wenyewe.
Tanzania ndo hamuwezi ku survive bila Zambia. Kwanza mnategemea border ya nakonde kuingia Congo. Mnategemea mpate mapato bandarini.

Ukisema kuhusu chakula kama mchele viazi etc vinavyotoka mbeya. Zambia karibu kila mji kuna maduka ya Shoprite na pick n pay. Hizo store ni za wa south afrika na wanaleta kila kitu mpaka ndizi sukari kutoka South vinauzwa hapo

Hicho kiburi alichokua nacho jiwe anawaambukiza Watanzania. Lakini Kaa ukijua Zambia anaweza kusurvive. Atatumia bandari ya beira/Durban kama ikibidi.

Sent From Galaxy S20 Ultra
 
Ni vizuri walivyofanya Zambia maana ni nchi inayojitawala kama ilivyo Tanzania so maamuzi yao ndiyo walichoamua, tusubili machine ipone ndipo tutajua mbichi na mbivu.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom