Rais wa zamani wa Marekani Donald trump amtaka Netanyau amalize vita vya Gaza mapema kabla hajarejea Ikulu ya Marekani kuwa Rais kwa mara nyingine

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
3,426
7,805
Wadau hamjamboni nyote?

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani, amemwambia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwa anataka Israel imalize vita vya Gaza kabla ya yeye kurejea madarakani iwapo atashinda uchaguzi, vyanzo viwili vilivyo na taarifa juu ya suala hili vimeeleza kwa The Times of Israel wiki hii.

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa mara ya kwanza wakati mgombea wa urais kwa tiketi ya Republican alipomkaribisha waziri mkuu huyo wa Israeli katika makazi yake ya Mar-a-Lago, Florida, mwezi Julai, kwa mujibu wa afisa wa zamani wa utawala wa Trump na afisa mmoja wa Israeli.

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kimombo:
---

Trump told Netanyahu he wants Gaza war over by time he enters office — sources

Former US president Donald Trump has told Prime Minister Benjamin Netanyahu that he wants Israel to wrap up the war in Gaza by the time he returns to office if he wins the election, two sources familiar with the matter revealed to The Times of Israel this week.

The message was first conveyed when the Republican presidential nominee hosted the Israeli premier at his Florida Mar-a-Lago resort in July, according to a former Trump administration official and an Israeli official.

While Trump has publicly confirmed having told Netanyahu that he wants Israel to win the war quickly, the sources speaking to The Times of Israel are the first to reveal that a timeline was attached to that request.

The former US official stressed that Trump wasn’t specific in his appeal to Netanyahu and could well back “residual” IDF activity in Gaza, so long as Jerusalem has officially ended the war.
 
Nahisi kama hiyo ni kauli ya kujichotea kura za mwisho mwisho. Usikute Trump na Netanyahu wamezungumza kinyume kabisa.

Kwa nje kuna moyo wa huruma na ubinadamu, ila kwa ndani wanasema, ^wapigwe tu!^
 
Anamaanisha anataka kuwa na uraia wa Iran, Parestine na au Lebanoni?

Uwongo wa mchana kabisa huo
 
Hujaelewa alichomaanisha Trump soma tena upya km mara 3 utaelewa
Najua siasa za Trump, lakini kuhusu mkakati wake pale Mashariki ya Kati, anaonekana kupwaya sana. Kifupi, amezidiwa mbinu na kuingizwa kwenye mfumo bila kupenda.

Umesahau jaribio la kumuua, nani alisingiziwa? Unadhani kwa nini? Halafu Trump awaache kweli Wairani wanaosakaziwa njama za kumwondosha rais wa Marekani?

Sitaki niamini, lakini kuna muvi moja matata sana jamaa anaenda kuizindua akiingia madarakani Jumanne ijayo. Itakuwa tofauti kabisa na matarajio ya wengi.

Nadhani Trump kule kupitishwa kote kwenye hila na fila za wasiompenda ilikusudiwa aingiapo madarakani awatekelezee matakwa yao.
 
Subiri uone movie itakavyokua ila jua Israel na Trump ni watoto wa Baba na Mama mmoja kwa hio subiria kufurahia show, amemaanisha wamalize mapema maana akiingia yeye akikuta bado hawajamaliza ataenda kumalizia yeye walipoishia kwa hio ndugu zangu wa Alauakbaru wakae mguu sawa
 
Wadau hamjamboni nyote?

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani, amemwambia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwa anataka Israel imalize vita vya Gaza kabla ya yeye kurejea madarakani iwapo atashinda uchaguzi, vyanzo viwili vilivyo na taarifa juu ya suala hili vimeeleza kwa The Times of Israel wiki hii.

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa mara ya kwanza wakati mgombea wa urais kwa tiketi ya Republican alipomkaribisha waziri mkuu huyo wa Israeli katika makazi yake ya Mar-a-Lago, Florida, mwezi Julai, kwa mujibu wa afisa wa zamani wa utawala wa Trump na afisa mmoja wa Israeli.

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kimombo:
---

Trump told Netanyahu he wants Gaza war over by time he enters office — sources

Former US president Donald Trump has told Prime Minister Benjamin Netanyahu that he wants Israel to wrap up the war in Gaza by the time he returns to office if he wins the election, two sources familiar with the matter revealed to The Times of Israel this week.

The message was first conveyed when the Republican presidential nominee hosted the Israeli premier at his Florida Mar-a-Lago resort in July, according to a former Trump administration official and an Israeli official.

While Trump has publicly confirmed having told Netanyahu that he wants Israel to win the war quickly, the sources speaking to The Times of Israel are the first to reveal that a timeline was attached to that request.

The former US official stressed that Trump wasn’t specific in his appeal to Netanyahu and could well back “residual” IDF activity in Gaza, so long as Jerusalem has officially ended the war.
Muhuni sana huyu. Nakumbuka alipoingia kipindi kile kitu cha kwanza alitoa unalozi wa USA kutoka tel aviv na kuuhamishia jerusaleem
 
Kwa nini ?
Screenshot_2024-10-30-19-37-29-51.png
 
Vita ni mzozo mkubwa tena unakula rooo za watu pande zote kama rais unataka usafiri kwenda kule n kule kwa aman Tramp ataki mizozo na Iran baada kuambiwa na majenerali wake kipindi kile kuwa Iran inanguvu kubwa ktk eneo. Ataki atolewe kwenye reli na mavitavita. Afuu msisaau Netanyahu alimsaliti Tramp ktk ule mgogolo wa urais Tramp anaamin kashinda ila kaibiwa kura n Biden uyu Netanyahu akawa kiongozi wa kwanza dunian kumpa ongela Biden za ushindi w urais!!!! Tramp akasema Netanyahu umenichoma kisu moyoni mwangu mtu ninaekuamini kuwa mwenzangu,,!! Tukumbuke Tramp alijotoleabsana kwa Israel kuliko rais yoyote isemavyo! Kubwa zaid Tramp z aliamisha ubalozi wao kupeleka jerusalemu na akaimiza wengine waamishe balozi zao kubwa zaid WAARABU alifanya juhudi watambuane na Israel na kufungua balazi kila alipofanikiwa kuwaweka pamoja Warabu n Israel, lkn mfahamu pia ktk ili Netanyahu kafaida kibinafsi ktk chaguzi za ndani uko Israel Tramp anafanya yote anajua zaid aya yatamsaidia mshilika wake Netanyahu ktk chaguzi, na ndio alishinda ayo mambo yalimbeba vizuli. Sasa mwenzie Tramp kule kabanwa mbavu alitegemea msaada kutoka kwa Netanyahu lkn mjuba nyahu akaona msaada wake amtambue mpinzani wake kuwa ndio rais yani Biden🤣🤣🤣🤣 sijui kama kamsameee yawezekana ataki ivyo vita sababu iyo ukiacha usalama wake lkn iyo vita ndio inashikilia nafasi ya Netanyahu kama PM WAZIRI MKUU kutokuwepo vita Netanyahu ataingia matatizoni hoo akimbie Isreal kabisa. So Tramp anataka kumsukuma nayeye nje ya uongozi!!!!! kwasasa Pia tujue Isreal ktk uchaguzi huu w USA wazi lazima wamuunge mkono Tramp japo atamsukuma Netanyahu nnnje y uongozi wa Israel Pm mpya watashilikiana vizuli na Tramp kuliko ashinde mwanamama H.... tangia mwanzo kashaonesha uruma kubwa kwa wapalestina., niwatakie asubui njema.
 
Subiri uone movie itakavyokua ila jua Israel na Trump ni watoto wa Baba na Mama mmoja kwa hio subiria kufurahia show, amemaanisha wamalize mapema maana akiingia yeye akikuta bado hawajamaliza ataenda kumalizia yeye walipoishia kwa hio ndugu zangu wa Alauakbaru wakae mguu sawa
Trump alivyoingia madarakani alitoa hadi majeshi ya marekani sehemu nyingi middle east ikiwemo afghanistan, trump moja ya misimamo yake ni kutotaka vita, ushoga wala abortion na alisimamia hayo alivyokuwa raisi
Na trump akiingia vita ya ukraine itaisha, ndio maana hata viongozi wa ulaya hawataki ashinde, hata huo upuuzi unaoendelea gaza hutausikia tena
Wakati dunia ya mafharibi ikipambana ba putin ,yeye alikuwa mshkaji wake
 
Sijaisoma hiyo article kwasababu moja tu, naujua msimamo wa Trump kuhusu Israel, nafahamu jambo moja pia kuhusu USA na sera zao kwa mambo ya nje ya nchi, wao ni "maslahi ya Marekani kwanza" mengine ndio yatafuata; USA ina maslahi na Israel so hata aje rais wa aje, sera yao kuhusu Israel inaeleweka, haibadiriki na haitakuja kubadirika; halafu chanzo cha hu ugomvi wa Israel na Hamas Ft Hezbollah ni Iran, Iran ni hasimu wa USA since mwaka 1978/9 halafu Trum afanye tofauti? No, sijasoma hiyo article kwasababu hizo, majibu nayajua.
Kitu kimoja ambacho lazima wana body tukijue; Marekani haiongozwi kwa matakwa ya rais kama nchi zetu hizi masikini, wale jamaa hata rais hana uhuru huo wa kujiamulia chochote anacho kitaka, kuna vyombo vina monitor maamuzi yake mengi. Mnakumbuka kampeni zilizo muweka Obama madarakani? Alikua anahubiri hivi, "nikiingia madarakani, sitaki VITA, naondoa majeshi yetu nchini Afghanistan na Iraq, nalifunga gereza la Gwantamo" guess what? Hakufanya hata moja katika hayo na ndiye aliye ongoza majeshi ya NATO kuipiga Libya. Na mwishoni alikuja kujizolea umaarufu kwa kumuua Osama bila kupeleka nchi vitani BUT why? Cause gereza la Gwantamo na majeshi yao bado yalikuwepo Afghanistan na Iraq. Marekani sio Tanzania, USA sio Africa. Wale wana mila na tamaduni zao za kiongozi.
 
Back
Top Bottom