Rais wa Zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo azuiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amezuiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wa tume ya uchaguzi.

Wakili wake Claude Mentenon amelimbia shirika la habari la AFP amesema kuwa kuna matatizo menginezaidi ya kisheria ndani ya Ivory coast dhidi yake.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilimuondoa katika orodha ya wagombea kwasababu alipatikana na hatia ya uhalifu.

Rais wa tume ya uchaguzi , Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, alisema mwezi Agosti kwamba yeyote anayepatikana na hatia ya uhalifu ataondolewa kwenye orodha ya wagombea.

Alitoa tangazo hilo wakati alipokua akitangaza orodha mpya ya wagombea.

Wagombea wanne akiwemo kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro waliondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais.

Bwana Gbagbo aliondolewa mashitaka mwezi Januari 2019 baada ya kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu uliohusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
 
Duh waafrika acha wazungu watudharau tu.. wachache wanafanya ujinga unaofanya kila mwafrika kuonekana mpumbavu popote duniani ... Yaani gbabo kakaa madarakani zaidi ya miaka 5 lakini anataka arudii .
Hayo mashtaka yametolewa lakini hili halizuii waliouliwa ndugu zao kutomwita muuaji
 
Wafuasi wa  Laurent Gbagbo walikuwa wamewasilisha nyaraka zake za  kugombea urais

Mahakama ya katiba nchini Ivory Coast aimemzuwia Rais wa Zamani wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo, na Waziri Mkuu wa Zamani, Guillaume Soro, kugombea Urais katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwezi ujao.

Tume ya uchaguzi ilikuia tayari imekwishasema kuwa yeyote mwenye rekodi ya uhalifu atazuiwa kugombea.
Kwa pamoja Laurent Gbagbo na Guillaume Soro walipatikana na hatia.

Awali, maandamano yaliibuka katika miji kadhaa kupinga uamuzi wa Rais Alassane Ouattara wa kugombea muhula wa tatu, kitu ambacho katiba ya Ivory Coast inazuwia.

Watu kumi na watano walikufa katika ghasia tangu mwezi uliopita alipotangaza kwamba atagombea tena urais.

Alichukua uamuzi huo baada ya mrithi wake aliyemchagua kufa ghafla mwezi Julai.
 
Huyo mrithi wake utakuta raisi Ouattara aliamua kumchomolea battery kwa makusudi ili aachie ngazi ya wenyewe. Africa is not yet free
 
Africa ni bara la giza kweli. Yaani mgombea kufa ghafla ndio inakuwa ticket ya Ouattara kutaka kuvunja katiba ili agombee muhura wa tatu?

Atleast dictators wengie (Mu7, Kagame..) walibadili Katiba kwanza...
 
Lile jinamizi letu limetung'ang'ania kweli kweli na hana kabisa mpango wa kutuachia.

Huyo Ouattara ameshasahau alivyoingia madarakani baada ya umwagaji mkubwa wa damu ya wananchi wasio na hatia. Mambo kama haya ndio yanafanya Afrika idharauliwe duniani.
 
Back
Top Bottom