Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaj | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaj

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Jan 19, 2011.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav.

  Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji.

  Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav amepatikana leo na hatia ya makosa mawili ya ubakaji, ikiwa ni kilele cha kashfa iliyojitokeza miaka minne iliyopita ambayo ililishangaza taifa hilo la Kiyahudi. Rais huyo wa zamani anakabiliwa sasa na hukumu ya kwenda jela miaka minane.

  Wakati mahakama hiyo mjini Tel Aviv ikitoa hukumu hiyo, ambapo pia imemhukumu Katsav kwa madai ya bughdha za kingono, vitendo vinavyovuka mipaka na kuzuwia sheria kuchukua mkondo wake, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 65 ambaye alionekana dhahiri kufadhaika, alikuwa akinong'ona tu, "hapana , hapana".

  Hukumu hiyo inakuja baada ya kuendeshwa kesi hiyo ambayo imechukua mwaka mmoja na nusu na kujumuisha madai ambayo ni ya kuhuzunisha, yakimuonesha Katsav kuwa ni mbakaji ambaye mara kwa mara huwasumbua wafanyakazi wanawake katika ofisi yake.

  Kiongozi huyo wa zamani wa nchi anashutumiwa kwa kumbaka mara mbili mwanamke mmoja ambaye ametambuliwa kwa jina la "Aleph" wakati akiwa waziri wa utalii, na kuwafanyia usumbufu kingono na kuwabughudhi wanawake wengine wawili wakati akiwa rais. Katsav amesema kuwa hana hatia wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo ya ubakaji na usumbufu wa kingono.

  Awali alikubali makubaliano ya kutoa maelezo yake mahakamani ambayo yangemfanya kukubali madai madogo madogo na kulipa faini ili waendesha mashtaka watupilie mbali madai ya ubakaji, lakini baadaye alibadili msimamo wake, na kufanya makubaliano hayo kuwa batili na kusema anataka kusafisha jina lake mahakamani.

  Alilazimika kujiuzulu kama rais , akakabidhi ofisi kwa hasimu wake Shimon Peres. Katsav amewashutumu wahanga wake kwamba wanajaribu kumwendea kinyume na kudai kuwa alikuwa mhanga wa juhudi za kumchafulia jina zinazofanywa na kundi la waendesha mashtaka na vyombo vya habari bila ya yeye kuweza kujitetea. Mwanawe wa kiume Boaz Katsav, baada ya kutolewa hukumu hiyo amesema kuwa baba yake hana hatia.

  Tunataka kukata rifaa. Na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, kila mmoja atatambua kuwa baba yangu , rais wa nane wa taifa la Israel hana hatia.

  Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa ni siku ya masikitiko kwa taifa la Israel na raia wake, lakini ameisifu kesi hiyo kuwa ni ishara ya nguvu za mfumo wa sheria wa nchi hiyo.

  Mwandishi : Sekione Kitojo / AFPE

  Mhariri : Josephat Charo

  Source: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,14744419,00.html?maca=kis-rss-kis-all-1488-rdf
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Not in africa pls
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Alikulia Iran huyo kwa hiyo aliadhiriwa na mazingira ya eneo alilokulia Hata hivyo hii imeonyesha kuwa kwa wa-Israel hakuna aliye juu ya sheria. Inabidi tuige mfano huu
   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Sheria za ubakaji kwenye nchi nyingine, zikiletwa hapa kwetu, kila mtu anaweza kupatikana na hatia ya ubakaji.

  Hebu fikiria, mpo kati kati ya shughuli, halafu mwanamke anaamua kubadilisha uamuzi, mwanaume aking'ang'ania, mwanamke anaweza kushtaki kuwa kabakwa. Sasa hatujui sheria za huko zina ugumu gani.
   
Loading...