Rais wa zamani wa Cape verde kupata sh Bil 8; Ni tuzo ya Mo Ibrahim

Kizimkazimkuu

JF-Expert Member
Nov 8, 2007
337
220
Felix Mwagara na Mashirika
RAIS wa zamani wa Cape Verde, Pedro Verona Pires, ameshinda Tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora barani Afrika.Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim ni moja ya tuzo yenye thamani kubwa duniani ambayo inatolewa na bilionea wa Sudan kwa mtu binafsi barani Afrika anayefikia viwango vya uongozi bora.

Pires ambaye aliachia madaraka Agosti, ametunukiwa Dola 5milioni za Marekani (zaidi ya Sh8 bilioni) zilizotolewa na kamati ya Mo Ibrahim.Kamati hiyo ilitangaza uamuzi wake jana jijini London, Uingereza, na kuonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni kote barani Afrika.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, Pires aliisaidia nchi yake kuwa mfano mzuri wa kuigwa wa utawala wa kidemokrasia, uhuru wa kibinafsi, na kuwa na rekodi nzuri ya kuheshimu haki za binadamu, uthabiti wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi.

Tuzo ya Mo Ibrahim iliyoanzishwa mnamo mwaka 2006 na bilionea wa Sudan, Mo Ibrahim, haijatolewa katika miaka miwili iliyopita kutokana na kukosekana watu waliotimiza vigezo vya kuimarisha maendeleo na demokrasia ili watunukiwe tuzo hiyo.

Habari zinasema kuwa, tuzo hiyo inatakiwa kutolewa kila mwaka kwa kiongozi anayechaguliwa kidemokrasia na kuondoka madarakani kwa hiari.Tuzo ya Mo Ibrahim ina thamani ya Dola5 milioni za Marekani katika kipindi cha miaka 10 na Dola 200,000 za Marekani kila mwaka kwa maisha.
Viongozi waliowahi kupata tuzo hiyo ni aliyekuwa Rais wa Botswana, Festus Mogae na Rais wa zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano
 

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Rais wa zamani wa Cape Verde, Pedro Verona Pires, ameshinda Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim ya utawala bora barani Afrika.

Tuzo hiyo ni moja ya tuzo yenye thamani kubwa duniani ambayo inatolewa na bilionea wa Sudan kwa mtu binafsi barani Afrika anaeyefika viwango vya uogozi bora.

Pires ambaye aliachia madaraka Agosti, ametunikiwa Dola 5 milioni za Marekani kwa kipindi cha miaka 10 na Dola 200,000 za Marekani kila mwaka kwa maisha yake yote.

SOURCE; MWANANCHI OCT 11 2011
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom