Rais wa zamani Afrika Kusini Kgalema Motlanthe asema ni vyema ANC kishindwe mwaka 2019

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
"Chama hicho kimehusishwa na ufisadi na ni lazima kipoteze ili tatizo hilo kumazika," aliambia BBC.

Bwana Motlanthe ni mwanachama wa cheo cha juu wa ANC ambaye matamshi yake yanaonyesha kuwepo tofauti kubwa chamani.

Chama hicho kimeshinda kila uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 60 tangua utawala wa wachache ufikie kikomo mwaka 1994.

Hata hivyo kilishindwa katika miii mikuu nchini Afrika Kusini ukiwemo mji wa Johannesburg wakati wa uchaguzi wa manispaa mwaka 2014.

Wapiga kura walionekana kukiadhibu ANC kutokana na ufisadi ufisadi unaozidi kukiandama.

Kiongozi wake Rais Jacob Zuma, ameponea kura ya kutokuwa na imani nae mara 8 katika bunge.

Amelaumiwa na upinzani na wakosoaji wengine wa ANC kwa kuwa kati kati ya mtandao wa ufisadi ndani ya serikali, madai ambayo anayakanusha.

Chanzo: BBC Swahili
 
Huyu jamaa alikuwa makamu wa Thabo Mbeki baadaye akawa Rais baada ya Mbeki kujiuzulu.
Alikuwa rais kwa kipindi kifupi sana kutoka 25 September 2008 and 9 May 2009.
 
Back
Top Bottom