Rais wa watu, mtu wa watu lini atabadilisha maisha haya ya watu?

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
8E9U8225.jpg

8E9U8320.jpg

8E9U8216.jpg

Source: Issamichuzi blog
 
Sidhani kama ana hata kauchungu kadogo maana Rais hajali watu amabao hawajijali wao wenyewe na Raisi ni miongoni mwa hao watu
 
Huku ni kukosa mipango inayotekelezeka ama kukosa watendaji wenye moyo na nia njema kwa nchi yao. Nafikiri JK akitaka kupata viongozi na watendaji wenye moyo na nia njema kwa Tanzania anatakiwa hivi sasa kuangalia nje ya mipaka ya CCM. Kuna watu wanaweza fanya vizuri sana kama watapewa nafasi za uongozi bila kujali party affiliation.

Umefika wakati sasa tujiangalia kama Tanzania na siyo nani ni mwenzetu. Huu uwenzetu ndiyo unamkwamisha JK, ni bora uchukue mtu wa mbali akileta upuuzi unamfanyizia on spot kuliko mwenzako akileta upuuzi unaona aibu kumwambia.
 
Nitaomba muniwie radhi pale nitaposema mengine sio lazima ya kuhitaji fedha ila ni ubunifu wa ile familia tu. Mfano hiyo picha ya juu fito za nyumba zinaonekana kabisa, jee udongo unauzwa? Na kama kazi ni nyingi basi hata baada ya mavuno haiwezekani angalau kukandika kwa udongo na kuunyoshea (plaster) hata kwa udongo wenyewe lakini nyumba ikaonekana nadhifu?

Na hiyo picha inayoonyesha uwepo wa takataka tunasubiri Manispaa waje kuzoa wakati anaeishi hapo ndiye anayeugua malaria na maradhi mengine yanayotokana na kuwepo kwa nzi?

Sio kwamba namdharau mtu na namwomba Mwenyezi Mungu anisamehe kama nimekufuru!
 
Ni kweli kabisa Binti Mkongwe kuwa jamii inahitaji kutekeleza yale ambayo yanawapatia maendeleo. Hata hivyo kwa upande mkubwa yapo maeneo ambayo Serikali inawajibika kusukuma maendeleo. Kwa mfano hawa watu wanaoishi katika mitaa ambayo mazingira yanaonekana ni machafu, shida ilianzania katika mipango miji ambapo Serikali iliachia watu kujenga pasipo kufuata mipango na hata katika mabonde na kuzuia barabara na mitalo ya maji.

Katika hali kama hiyo, juhudi za mwananchi mmoja mmoja pasipo nguvu ya Serikali ya kulazimisha sheria kuchukua mkondo wake, huwezi kutegemea mabadiliko zaidi ya kuona hali inakuwa mbaya..Nini maana ya kuwa na Sheria za Mipango Miji au za Mazingira katika Nchi iwapo haki kama hizi zinashindwa kukabiliwa?
 
moyo unauma, hivi hapa na yeye anataka kuwalaghai wananchi ili waseme yeye ni mtu wa watu....mtu wa watu .....hivi haoni huruma hao watu jamani, angekaa tu ofisini, sasa hapo alienda kufanya nini? wakati wat uwenyewe hao si ajabu usiku wa leo hawatakula? Tz amkeni mtoeni huyu jamaa mwekeni mtu ambaye yuko serious.
 
Back
Top Bottom