Rais wa watanzaniau ni mfujaji wa kodi zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa watanzaniau ni mfujaji wa kodi zetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, Jul 23, 2011.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa siku kadhaa nimekuwa nikifuatilia nyendo za rais watanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mwezi huu huu alikuwa katika mji wa Bukoba kwa ajili ya kufunga maonyesho ya ushirika yaliyofanyika Bukoba kitaifa. Nilishangaa jinsi alivyokuwa na msafara mkubwa sana. Lakini nilisikitishwa na kitendo cha magari anayotumia kuja toka Dar es salaam ili tu aweze kutembelea hapo Bukoba na kisha yarudi tena Dar. Gharama zote hizo za nini? kuna mtu aliniambia hata mbwa wa polisi waliletwa toka Dar ingawa sina hakika na hilo.

  Leo tena alikuwa Muleba kuhudhuria mazishi ya mbunge wa zamani wa Muleba anayejulikana kama Zimbihile. Kwa mara nyingine tena imeshuhudiwa msafara mrefu wa magari ya serikali na polisi wamekuwa barabarani tangu asubuhi wakizuia magari na watu kutumia barabara iendayao uelekeo wa njia ya Muleba. Ilikuwa ni usumbufu mkubwa sana usio na sababu kwa wananchi. Lakini lililoniumiza ni kule kuleta tena yale magari anayotumia Dar kuja kufanya shughuli ya kumtembeza Kagera. Jamani gharama zote hizo nani analipa katika hali ngumu yetu tuliyonayo?

  Siwezi kulaumu kuja kwake kwenye msiba huo maana inasemekana wazi kwamba mmoja kati ya mabinti wa marehemu ni kidosho wake na amezaa naye na kwa hiyo alikuwa anakuja kwenye msiba wa baba mkwe wake! lakini kwa nini kwa gharama kubwa zote hizo? si angeweza kutumia gari ya mkuu wa mkoa wa Kagera na akawa na msafara mdogo? nchi imejaa simanzi ya giza na bado tunatumia pesa ovyo, huku ilitolewa hoja na serikali yenyewe kwamba itapunguza safari na misafara ya viongozi?

  chini ya utawala wa Kikwete hakika hatuwezi kupata maendeleo mie nawambia ukweli. Nyie kaeni mkao wa vilio visivyokwisha maana huyu jamaa hana mpango wa kutuendeleza bali starehe zake na kutafuta umaarufu tupu. Endeleeni kuusikiliza porojo zake mtabaki umia buree!
   
Loading...