Rais wa wananchi atatokana na wananchi, na sio chaguo la mtu fulani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa wananchi atatokana na wananchi, na sio chaguo la mtu fulani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Jan 25, 2012.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hatutaki kuletewa raisi kwa kuzingatia jinsia

  Tunataka raisi mwenye uwezo.

  Tumeletewa SPika wa jinsia, sote tumeona udhaifu wake.

  Tunataka viongozi waadilifu, wenye uwezo na wenye dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi kama Nyerere na Sokoine.

  Kwanza tujiulize, huyo anaepigiwa debe, ametoa mchango gani kwa Tanzania wakati alipokuwa raisi, wakati alipokuwa nje?

  Pia tuwaogope wote wanaokimbilia Ikulu. Be Me, EL, SAM SIX, Mig ro, - tumikieni wananchi, acheni kupanga mikakati ya kuingia ikulu, hiyo ni NDOTO hamtapaona nG'0

  Hao wanaokimbilia ikulu wawasaidie wananchi sasa na sio wasubiri waingie Ikulu.

  Tunataka tuone michango yao wakiwa katika wadhifa wa uwaziri au ubunge au nafasi ingine, tukiridhika tuwape uraisi.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtindo wa WAJANJA wachache ndani ya CCM kuchagulia WaTanzania Rais wa nchi ulishapitwa na wakati tangu miaka mingi nyuma.

  Sasa hivi ni Rais chaguo la wananchi moja kwa moja bila udalali. Na huyo Migiro tunamsubiri na kashfa yake ya kufa mtu huko UN wakati utakapowadia achilia mbali minong'ono kibao ndani ya familia yake hadi hivi sasa.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Bila Katiba Mpya NEC wataendelea kutuchagulia Rais
   
Loading...