Rais wa Vietnam aanza ziara ya siku tatu nchini

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Truong Tan Sang, ameanza ziara ya siku tatu nchini, ambapo pamoja na masuala mengine, atasaini mkataba wa masuala ya Kodi na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Mkataba huo unalenga kuchochea biashara kati ya Vietnam na Tanzania kwa kuwa utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote kutotozwa kodi mara mbili katika biashara na uwekezaji watakaoufanya.

Rais huyo anatarajiwa kupigiwa mizinga 21 leo, ikiwa ni pamoja na kukagua gwaride rasmi, ambapo baadaye atatambulishwa kwa viogozi mbalimbali wa Serikali, kabla ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu ujio wa Rais huyo wa Vietnam, baada ya viongozi hao kutia saini mkataba huo, mgeni huyo na ujumbe wake atakwenda kwenye ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Mtaa wa Lumumba jijini humo kukutana na Mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Rais huyo wa Vietnam ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo chenye uhusiano wa muda mrefu na CCM, atakwenda kwenye Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Ubungo, Dar es Salaam kutembelea viwanda na kupata taarifa za fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.

Aidha, ratiba hiyo imeeleza kuwa atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, kabla ya kukutana na Spika wa Bunge, Job Ndungai na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika wakati tofauti.

Pamoja na ujumbe wake atatembelea hifadhi ya wanyama ya Saadan iliyoko Bagamoyo na kuondona nchini Machi 11 kuelekea Msumbiji kuendelea na ziara yake.
 
Afadhali waje watusaidie kuwaelekeza viongozi wetu jinsi ya kuimarisha uchumi wetu
 
Ujio wake natumaini utakuwa na mafanikio kwetu kwani wana bidhaa nyingi sana ambazo tunaweza kununua kama tutadumisha uhusiano na kujikita katika masuala ya kibiashara na viwanda well and Good
 
nakumbuka picha za kivita wakati wadogo , wavietinamu wanamiminiwa risasi lakini wanamiminika kama siafu , hawaishi!!
 
Napenda kujifunza labda protokali imebadilika. Raisi huyu amepokelewa uwanja wa ndege na Mhe. Waziri Mkuu, labda haya ni mabadiliko mapya. Nimeona pia kuwa mgeni wetu atakutana na mwenyekiti wa CCM kwenye ofisi zake zilizopo Lumumba ili kufanya naye mazungumzo.
 
Napenda waje wawekeze kwenye viwanda vya nguo maana Vietnam inasifika kwa utengenezaji wa nguo.
 
Sijaelewa vitu vingi hapo, nisaidieni wakuu huu ugeni kama sijauelewa
  • Hivi huyu si ndio rais ambaye unatoka ule mtandao wa halotel? Na imewahi kutajwa kwamba bwana mkubwa mstaafu anaumuliki ule mtandao, na ndio mana ttcl wameshindwa kupewa tender ya kusambaza internet kwenye halmashauri na mashuleni wakapewa hao halotel.Je kiongozi wa chama ana maamuzi gani kitaifa mana ziara ya huyu raisi ni ya kitaifa?
  • Kama nimeanza kuhisi huenda JPM hajaenda kumpokea kutokana na kujua jamaa anakuja kideal na sio kikazi kama inavotangazwa.
  • Anakuja kisign kuondolewa kwa kodi, Hivi kuna watanzania walio invest huko vietnam? Kama hakuna basi pasipo na shaka hapa tunapigwa peupe.
 
Napenda waje wawekeze kwenye viwanda vya nguo maana Vietnam inasifika kwa utengenezaji wa nguo.
Kikwete alimshauri wawekeze kwenye kampuni ya simu wamekuja na Halotel biashara ambayo ni sawa na mtoto aliyefia tumboni.
 
Back
Top Bottom