Rais wa Uruguay José Mujica, ndiye Rais anayeishi maisha duni kuliko wote duniani

[h=2] Rais masikini zaidi duniani[/h]Imechapishwa Jumapili, 14 Oktoba 2012 14:37
Imeandikwa na MONTEVIDEO, Uruguay
Imesomwa mara: 8298





NCHI ya Uruguay yenye raia takribani milioni 4, inatajwa kuwa na bahati ya kuwa na Rais asiye na chembe ya tamaa. Hana makuu, kiasi kwamba anatajwa kuwa ndiye Rais masikini zaidi kuwahi kutokea duniani. Huyu si mwingine, bali ni Jose Mujica, Rais wa sasa wa Uruguay ambaye pia ni Rais wa 40 wa nchi hiyo. Tangu aingie madarakani Machi mosi mwaka 2010, amekuwa akionekana kuwa kiongozi wa tofauti kabisa, tofauti na waliomtangulia. Mathalan, baada ya kufanikiwa kuishika nchini, hakuwa na tamaa ya kukimbilia Ikulu, yeye alichokifanya ni kuamua kuishi katika makazi yake yaleyale, katika nyumba ya mkewe iliyoko shambani, nje ya Jiji la Montevideo. Kwa ujumla, anapenda maisha ya kawaida, maisha ya kuwahurumia wengine na kujitahidi kuonesha kwa vitendo. Ni vigumu kuamini, licha ya kuwa ni Rais wa nchi, amejishusha mno kiasi cha mara kadhaa kuonekana akijichanganya na raia wake katika shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwamo ujenzi wa barabara, kulima mashamba ya mfano. Na wakati mwingine, anapougua huwahi kupanga mstari ili kuonana na daktari, akichelewa anapanga mstari kusubiri zamu yake. Ni Rais pekee ambaye ameamua kutoa mshahara wake kwa zaidi ya asilima 90 kugawana na watu masikini wa nchi yake, kwamba fedha hizo huingizwa katika vikundi mbalimbali vya maendeleo.
Akiwa amepangiwa na Bunge kupokea dola za Kimarekani 11,000 (sh milioni 17.6 kwa fedha za Tanzania) kwa mwezi, hajawahi kupokea fedha hizo na ameiamuru Hazina kuzipeleka fedha hizo kwa wananchi masikini.
Yeye hupokea shilingi milioni 3 tu, tena hizi akizitumia kwa ajili ya mafuta ya gari lake alilonunua na mkewe aina ya Volkswagon Beetle maarufu kama `Mgongo wa Chura’. Gari hilo lenye umri wa miaka 23, ndio utajiri pekee anaojivunia.
Hana kingine anachokimiliki. Hana akaunti benki, hana nyumba yake binafsi, wala mali nyingine ya aina yoyote aliyojilimbikizia. Kuhusiana na gari lake lenye thamani ya dola za Kimarekani 1,900 (Sh milioni 3), ambalo analiendesha mwenyewe, anasema: “Niko mimi na mke wangu, wawili tu, gari kubwa la nini, sina haja nalo, sitaki kuwaibia wananchi, kunichagua tu kuwaongoza ni sifa pekee, tena kubwa inayokaribia utukufu wa kawaida, sasa zaidi ya hapo nini…
“Nahitaji sana kuwatumikia wananchi wa Uruguay, sio kuwanyonya wala kuwaibia au kuwa mwanya wa kuchuma na kujifurahisha mimi, mke wangu, watoto wangu na ndugu zangu, sioni haja hiyo na sitaki kuwa mnyonyaji kamwe,” anasema Rais Mujica. Anasisitiza anayafurahia maisha ya kawaida, hivyo haoni shida kuishi na watu wa kawaida mtaani kwake, kupiga nao porojo na hata kushirikiana katika shughuli za kijamii pale inapolazimu.
“Nikiwa na akaunti benki, nikiwa na magari makubwa, nitakuwa nakaribisha ushawishi wa kuwa mwizi, kuwaibia wananchi wangu, sitaki chochote,” anaongeza Rais huyo ambaye hata anapoamua kunyoa nywele zake, hahitaji kinyozi maalumu, bali yeyote anayejua kunyoa anamwita nyumbani kwake aweze kumnyoa.
Staili ya maisha ya Rais huyo inaonekana pia kumwingia mkewe ambaye pia tofauti na wake wengine wa marais, yeye hajipambi kwa dhahabu, almasi wala aina nyingine ya vito vya thamani.
Anashirikiana na mumewe katika shamba lao la maua katika makazi yao, huku Rais Mujica wakati mwingine akifanya usafi wa nyumba na hata kumwagilia maua. Hayo ndiyo maisha ya Jose Mujica, Rais wa 40 wa Uruguay ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 77, lakini licha ya kupigania mno kuingia Ikulu, ameonesha kutokuwa na kiu ya utajiri, hataki kujikweza na wala kuonekana ni tofauti na watu wengine. Ndiyo maana ameonekana kuwa Rais wa ajabu, akitajwa pengine kuwa ndiye asiye na makuu na masikini kuliko wote duniani. Hata vaa yake ni ya kawaida, mara nyingi akiingia ofisini na mavazi ya kawaida, lakini mara moja moja tu, akivalia suti na tai hasa anapokuwa na ugeni mzito. Angalau Makamu wake, Danilo Astori anaonekana na `ufisadi’ kidogo, kwani ana nyumba yenye thamani ya dola 250,000 (Sh milioni 400) na gari kama la milioni 30 hivi. Je, kuna wengine wenye staili ya maisha ya Rais Mujica? Yawezekana, lakini kwa sasa imeonekana hakuna kama Mujica.


Source Habari leo 19.01.2013

Nionavyo:
Kwa kasi ya kutumia pesa ili waingie madarakani, je tuna rais kati ya marais tulionao anayeweza kuishi maisha angalau nusu ya rais huyu? Sie tulionao wanatamani kuendelea kufisadi hata baada ya kuondoka madarakani.
Naomba Mungu tumpate mmoja tu kama huyu.
 
Hata Babu anatakiwa agawe milioni 140 alizochukua kwa wananchi maskini
 
http://m.bbc.co.uk/news/magazine-20243493


Jose Mujica: The world's 'poorest'
president
By Vladimir Hernandez
BBC Mundo, Montevideo
15 November 2012 Last updated at 00:29
It's a common grumble that politicians'
lifestyles are far removed from those of
their electorate. Not so in Uruguay. Meet
the president - who lives on a ramshackle
farm and gives away most of his pay.
Laundry is strung outside the house. The water
comes from a well in a yard, overgrown with
weeds. Only two police officers and Manuela, a
three-legged dog, keep watch outside.
This is the residence of the president of
Uruguay, Jose Mujica, whose lifestyle clearly
differs sharply from that of most other world
leaders.
President Mujica has shunned the luxurious
house that the Uruguayan state provides for
its leaders and opted to stay at his wife's
farmhouse, off a dirt road outside the capital,
Montevideo.
The president and his wife work the land
themselves, growing flowers.
This austere lifestyle - and the fact that Mujica
donates about 90% of his monthly salary,
equivalent to $12,000 (£7,500), to charity -
has led him to be labelled the poorest
president in the world.
"I've lived like this most of my life," he says,
sitting on an old chair in his garden, using a
cushion favoured by Manuela the dog.
"I can live well with what I have."
His charitable donations - which benefit poor
people and small entrepreneurs - mean his
salary is roughly in line with the average
Uruguayan income of $775 (£485) a month.
All the president's wealth - a 1987 VW Beetle
In 2010, his annual personal wealth
declaration - mandatory for officials in
Uruguay - was $1,800 (£1,100), the value of
his 1987 Volkswagen Beetle.
This year, he added half of his wife's assets -
land, tractors and a house - reaching
$215,000 (£135,000).
That's still only about two-thirds of Vice-
President Danilo Astori's declared wealth, and
a third of the figure declared by Mujica's
predecessor as president, Tabare Vasquez.
Elected in 2009, Mujica spent the 1960s and
1970s as part of the Uruguayan guerrilla
Tupamaros, a leftist armed group inspired by
the Cuban revolution.
He was shot six times and spent 14 years in
jail. Most of his detention was spent in harsh
conditions and isolation, until he was freed in
1985 when Uruguay returned to democracy.
Those years in jail, Mujica says, helped shape
his outlook on life.
"I'm called 'the poorest president', but I don't
feel poor. Poor people are those who only
work to try to keep an expensive lifestyle, and
always want more and more," he says.
"This is a matter of freedom. If you don't have
many possessions then you don't need to work
all your life like a slave to sustain them, and
therefore you have more time for yourself," he
says.
"I may appear to be an eccentric old man...
But this is a free choice."
The Uruguayan leader made a similar point
when he addressed the Rio+20 summit in June
this year: "We've been talking all afternoon
about sustainable development. To get the
masses out of poverty.
"But what are we thinking? Do we want the
model of development and consumption of the
rich countries? I ask you now: what would
happen to this planet if Indians would have the
same proportion of cars per household than
Germans? How much oxygen would we have
left?
"Does this planet have enough resources so
seven or eight billion can have the same level
of consumption and waste that today is seen in
rich societies? It is this level of hyper-
consumption that is harming our planet."
Mujica accuses most world leaders of having a
"blind obsession to achieve growth with
consumption, as if the contrary would mean
the end of the world".
Mujica could have followed his predecessors
into a grand official residence
But however large the gulf between the
vegetarian Mujica and these other leaders, he
is no more immune than they are to the ups
and downs of political life.
"Many sympathise with President Mujica
because of how he lives. But this does not stop
him for being criticised for how the
government is doing," says Ignacio Zuasnabar,
a Uruguayan pollster.
The Uruguayan opposition says the country's
recent economic prosperity has not resulted in
better public services in health and education,
and for the first time since Mujica's election in
2009 his popularity has fallen below 50%.
This year he has also been under fire because
of two controversial moves. Uruguay's
Congress recently passed a bill which legalised
abortions for pregnancies up to 12 weeks.
Unlike his predecessor, Mujica did not veto it.
Instead, he chose to stay on his wife's farm
He is also supporting a debate on the
legalisation of the consumption of cannabis, in
a bill that would also give the state the
monopoly over its trade.
"Consumption of cannabis is not the most
worrying thing, drug-dealing is the real
problem," he says.
However, he doesn't have to worry too much
about his popularity rating - Uruguayan law
means he is not allowed to seek re-election in
2014. Also, at 77, he is likely to retire from
politics altogether before long.
When he does, he will be eligible for a state
pension - and unlike some other former
presidents, he may not find the drop in
income too hard to get used
 
Kama kiongozi yuko tayari kuongwa suti tatu ili kuuza nchi ni vipi akubali pay cut kusaidia masikini?!
 
Mtu mzima Josee huyu hapa!!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1367148544.019494.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1367148544.019494.jpg
    24.2 KB · Views: 128
  • ImageUploadedByJamiiForums1367148571.742493.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1367148571.742493.jpg
    49.6 KB · Views: 119
  • ImageUploadedByJamiiForums1367148634.925479.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1367148634.925479.jpg
    33.3 KB · Views: 112
  • ImageUploadedByJamiiForums1367148666.860843.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1367148666.860843.jpg
    28.1 KB · Views: 111
Captain Thomas Sankara was Burkina Faso aliishi maisha hayo na wakamwuua. Hata Warren Buffet ni tajiri wa kutupwa lakini hana makuu sana Ningependa viongozi wetu hasa wabunge waishi kwa mtindo huo
Fomu zingeoza kwenye ofisi za chama...I mean nani angechukua fomu za kuomba kugombea ubunge???
 
Kwa jina Kamili anaitwa José Alberto "Pepe" Mujica Cordano ni raisi wa Uruguay Tokea mwaka 2010..Alizaliwa 20 May 1935. Raisi huyu kwa mwezi anapokea mshahara wa dola $12,000 (Tshs 19,320,000) kwa mwezi lakini cha ajabu kabisa raisi huyu hutoa asilimia 90% ya mshahara wake kama sehemu ya msaada kwa wananchi wake wasiojiweza na hivyo kupokea mshara wa dola $775 (Tshs 1,247,750) hivyokumpelekeakuwa moja ya maraisi masikini zaidi ulimwenguni. Baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa Uruguay alikata kuishi ikulu na kwenda kuishi nje ya kidogoya mji mahalipalipo shamba la mke wake.. Kitu cha thamani anachomiliki Raisi huyu ni gari aina ya Volkswagen Beetle, yenye Thamani ya dola $1,945 (Tshs 3,131,450). Je marais na wanasiasa wa Afrika wanaweza kujishusha kiasi hiki??

941143_460780244013547_499541479_n.jpg
 
Back
Top Bottom