Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,299
- 3,055
Kufuatilia zaidi gonga hapa Uruguay's Jose Mujica - "The poorest president in the world" - YouTube
Inamana rizone anaweza mzidi kwa cash? vp yeye hana malori? jakaya kashamtembelea au rais wetu ataki maskini.
Mimi binafsi nampongeza!!Pato lake halali ni zuri kiasi kwamba hahitaji kulimbikiza mimali, na amesema, akisha maliza muda wake wa uongozi anarudi kuchunga ng`ombe shambani kwake. Tatizo la wanadamu ni kwamba wengi hawajui wanataka nini. Kuku ngendu alikuwa na jumba kando ya ziwa Geneva la vyumba kibao, lakini aliishia kupigwa chepe Morocco kienyeji. Furaha ya kweli na uhuru wa kweli, na amani ya kweli ni bidhaa muhimu sana kwa maisha ya mtu mwenye akili timamu, huyu jamaa kafanikiwa sana kufikia hivi vitu vitatu.
Umesahau vitu vingi ktk hadithi yako hii, moja hujasema mkewe anafanya nini? Mkewe ni senetor ktk bunge/uongozi wa nchi hiyo, pili, huyu jamaa ana shamba kubwa la ng`ombe wa maziwa. Nchi hiyo ina-export bidhaa za maziwa nje. Tatu nchi ile ina wahamiaji wengi sana toka nje ya bara la America kusini. Na mwisho ni nchi yenye idadi ndogo sana ya watu, na wengi wanazalisha kwa njia ya kilimo kwa scale kubwa akiwemo Rais mwenyewe.
Kwa hiyo utaona kwamba hawa wahamiaji ( most Wadachi, japanese) wamekuwa na mchango mkubwa sana ktk mafanikio ya nchi ile. Na jioni wote wanaburudika na soka la vijana wao. Wenyewe wanasema ile ni Switzerland ya America Kusini.
hata rais wetu ni masikini sana zaidi ya huyo unayemsifia
Umeambiwa Huyu Mujica anatoa 90% ya mshahara wake kwenda kusaidia wenye dhiki. Huwezi kuishi maisha haya ukaupata huo utajiri wa kutupwa wa huyo warren. Kwa upande mwingine, hakuna makuu kuliko kuwa na huo utajiri wa kutupwa wakati umezungukwa na watu wasiomudu hata mlo mmoja kutwa. Kwa lugha rahisi, ni ushetani.
Yericko rais wetu anasingiziwa tu wala sio tajiri coz anavijumba vya kawaida pale Msoga vimejengwa kwa msaada wa S.Patel (kama Nyerere alivyojengewa na JW). Kile kighorofa cha Regent any civil servant can build.
Rais JK sio mfanyabiashara, ni mkulima wa mahindi na mananasi.
Vibiashara vingi mnavyovisema ni vya mwanae ambaye nasikia ni mzuri sana wa kuandika proposal ndio maana anapata tender nyingi za serikali.
Hata ile kampuni yake ya uwakili RGK (share na binti wa Karume) inapata kazi serikalini kwa vile kampuni nyingi zimekuwa haziisaidii ipasavyo serikali yetu.
Nasikia wasaidizi wake ndio wanapenda pomps, ila yeye hana makuu. Ukiona kavaa suti ya gharama sana basi kuna uwezekano mkubwa kapewa tu hajanunua yeye..
Rais wetu sio tajiri...
Rubuye123 tukana tu ila ukikutana na BAN usinilaumu.uko serious!!!?????...............najizuia sana kukutukana hapa,kama kweliuko serious!!!
Rais Jose akishuka kwenye gari lake, kwenye nyumba yake ya kawaida. Wanaoonekana pembeni ni wasaidizi wake wa idara ya ulinzi (Picha kutoka Mtandao) |
Tupe chanzo cha hii taarifa tafadhari...Mwaka wa mwisho wa jk atafanya hivyo pia