John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Picha: Rais wa Ujerumani Frank -Walter Steimeier
Rais huyo maarufu amechaguliwa kwenye mkutano maalum wa wabunge 736 na wawakilishi wa majimbo 16 ya Ujerumani uliofanyika jana Jumapili mjini Berlin.
Mwanasiasa huyo mahiri mwenye umri wa miaka 66 wa Chama cha Social Democratic (SPD) aliungwa mkono na vyama vyote vitatu vinavyounda serikali ya mseto pamoja na chama cha upinzani cha wahafidhina cha Christian Democratic Union (CDU).
Steinmeier katika hotuba kwenye Bunge Maalum baada ya kukubali kuchaguliwa kwake, amesema wajibu wake ni kuwatumikia watu wote wa Ujerumani na amesisitiza kuwa haegemei upande wowote na linapokuja suala la demokrasia yeye wakati wote atasimama na wanaotetea demokrasia.
Wadhifa wa Rais nchini Ujerumani ni wa heshima tu. Wagombea wengine watatu waligombea ofisi hiyo ya juu zaidi nchini Ujerumani ingawa hawakuwa na nafasi kubwa ya kushinda.
PIA SOMA:
- Ujerumani kumchagua Rais wake kupitia Baraza la Wabunge