figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,481
Rais wa TLS Mhe Tundu Lissu alitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na siyo siasa.
Rais wa Chama cha wanasheria Tanzania (TLS) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikungi na kuwataka polisi kuacha kutekeleza maagizo ya baadhi ya viongozi wa siasa kutoa amri ya maneno ya kuwa kamata watu bila ya kuwa na kibali halisi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kati Bi.Aisha Luja amemuomba Mheshimiwa Tundu Lisu kundelea kusimamia mikataba ya madini ambayo imekuwa ikitekelezwa kisiasa na kunyimwa kwa uhuru wa vyombo vya habari,huku Mbunge wa Kilombero Mheshimiwa Peter Ambrosi Jualikali akiwataka wananchi wa Jimbo la Singida Mshariki kumtumia vizuri mbunge wao Tundu Lisu.
Mheshimia Tundu Lisu baada ya kufika katika mkutano huo akiwa na badhi ya wabunge wa CHADEMA,uliohudhuriwa na wananchi wengi kutoka katika vitongoji vya Jimbo la Singida mashariki alivishwa mavazi ya asili ikiwa ni ishara ya shujaa
Chanzo: ITV