TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Mkapa on presidential term-limits

Watanzania wakimsifia Mkapa kwa mengi, wakubali na maneno yake kuhusu viongozi kuheshinu term limits.
Tuliokuwepo enzi za Komandoo tunamkumbuka Mkapa kwenye hii ishu. Komandoo alikuwa na visa, mara aiunge Zenj kwenye jumuia ya nchi za kiarabu, mara atume wazee kumtishia kuvunja muungano kama hataruhusiwa kubadili katiba apate muhula wa 3, etc. Mkapa alisimama kidete, komandoo ikabidi akubali yaishe. Ingekuwa enzi ya JK, mmmmh 🙄.
 
Kuna Mabeyo wa Sasa na yule aliyestafu wa Mbeya
Yule aliyestaafu ni mstaafu. CDF ni mmoja tu. Ni sawa a leo hatusemi raisi, bali raisi mstaafu kafariki 😜.

Kuna yule kijana Nelson Mabeyo akiyeanguka na ndege aliyokuwa akiiendesha. In his early 20s. Miezi michache tu iliyopita.
 
“Mwili wa Rais Mstaafu Mkapa utazikwa kijijini kwao Lupaso, Masasi Mkoani Mtwara Jumatano ya wiki ijayo July 29,2020 saa nane mchana, mwili huo utasafirishwa kwa Ndege Jumanne July 28 mchana baada ya kumaliza shughuli za kuuaga Uwanja wa Taifa DSM, utatua Uwanja wa Nachingwea, Lindi kisha kuelekea Masasi”-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
#RIPMzeeMkapa
 
Kumbe unajua kwamba huko inabidi tuombeane ili tupumzike kwenye peace

Huu ni msiba wa mzee ninayemuheshimu na kujuana na familia yake si kama rais mstaafu wa Tanzania, bali kama watu tuliokua pamoja Upanga.

Sipendi uingize hashuo zako zenye shombo ya ushamba na kizabizabina cha kuparata.

Mzee Mkapa deserves better than that.
 
Tuliokuwepo enzi za Komandoo tunamkumbuka Mkapa kwenye hii ishu. Komandoo alikuwa na visa, mara aiunge Zenj kwenye jumuia ya nchi za kiarabu, mara atume wazee kumtishia kuvunja muungano kama hataruhusiwa kubadili katiba apate muhula wa 3, etc. Mkapa alisimama kidete, komandoo ikabidi akubali yaishe. Ingekuwa enzi ya JK, mmmmh 🙄.
Watu wanasema Nyerere haambiliki, lakini Mkapa kwenye msimamo akishaamua kitu alikuwa mbishi kuliko Nyerere, halafu anakubishia wakati kashasoma Bluebooks zote ana facts na figures na historia ya Tanzania tangu akiwa Editor wa Standard.

Utamwambia nini hakijui?
 
Kwanini tusimkumbuke pia na kwa mabaya yake ili ku balance?
Maisha ni kuendeleza mazuri na kuacha mabaya. Kama umesoma vizuri post yangu, niliandika kuwa "tutamkumbuka sana" kwa mazuri yake, sikusema kuwa "tutamkumbuka kwa mazuri yake tu". Sijui kama umenielewa
 
Hakika siku yako ikifika hakuna msalie Mtume, Apumzike kwa Amani Mzee Benjamin William Mkapa.
 
Mkubwa , huwezi kumtenga Mkapa na Siasa. Mshtuko ulioikumba jamii ni kutokana na haiba yake kisiasa. Leo kuna mamia ya watu wametangulia mbele ya haki, kwanini haiujulikani! si wanasiasa kama Mkapa.

2. Bendera zitapepea nusu mlingoti kwasababu mwanasiasa kafariki, si wananchi wengi waliofariki jana na leo.

3. Kwaviletumevunja utamaduni wa facts, zipi unataka watu wasubiri? Watu watasema kwavile tumevunja trust inayotoa facts. Watu hawaamini tena kinachosemwa!
Hayo uliyosema ni sahihi lakini siyo kutumia kifo chake kama uwanja wa kufanyia siasa za korona. Watu wote tumezaliwa siku moja na tutakufa siku moja; wengine hufa bila kuugua kabisa (Baba yangu alifariki ghafla bila kuugua chochote na wala hakukua na korona).

Wengine huugua mda mfupi tu (dada yangu aligua tumbo kuumwa, akalazwa hospitali siku moja na kufariki usiku huo huo akiwa na umri wa miaka 25 tu) na wengine huugua muda mrefu sana. Vyote ni vifo tu.

Ingekuwa ni kwa kushambuliwa na majambazi kama alivyoshambuliwa Lissu, ndipo hapo tungeweza kukabana na vyombo vya dola na kuingiza siasa.
 
Daaah . . . so sad.
Kwangu mimi nitamkumbuka kama mmoja wa wahariri bora wa habari za kiuchunguzi wakati ule akiwa pamoja na mwandishi mwenzie (Nsa Kaisi ambaye naye ni marehemu) kwenye gazeti la the nationalist (kama sijakosea). Alihariri story moja mpaka Nyerere akaukubali mzigo kwa jinsi ulivyosimama.

Nakumbuka siku moja tulikutana pale kwenye kijiwe chetu cha kahawa kabla hajaenda kugombea urais wa jamhuru ya muungano wakati huo akiwa waziri wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu tuliongea mambo mengi sana. Huyu mzee alikuwa critical kwelikweli. Na alipenda sana mijadala.

Chuo kikuu cha Columbia kilinoa mtu mahiri. Na sisi tuliokutana naye wakati tuko University of Washington tunajua dhahiri huyu jamaa alikuwa jembe japokuwa nilipishana naye sana kwenye suala la ubinafsishaji. Am happy kwa kiasi fulani alikubali makosa yake na kutuasa kuwa tayari kujisahihisha.

Taifa limepoteza mtu mahiri. Apumzike kwa amani.
 
Nimepokea kwa Masikitiko makubwa sana juu ya Kifo cha ' Kushtukiza ' cha Hayati Rais wa Awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na natoa pole zangu za dhati kabisa kwake Mjane Mama Anna, Watoto wake, wana Familia, wana CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa Ujumla.

Kwa Mema ya Kibinafsi kabisa niliyoyapata kupitia Uongozi / Utawala wake wa 1995 hadi 2005 sina cha Kumlipa sana sana nimwombe tu Mwenyezi Mungu amsamehe Dhambi zake zote na aiweke Roho yake mahala pema peponi.

Sitokwi na ' Machozi ' ya Nje, ila ndani ya Moyo wangu kuna ' Mafuriko ' makubwa ya ' Machozi ' ya Uchungu. Nenda Mzee Mkapa na ukapumzike kwa Amani kabisa, ila Asante kwa uliyonifanyia January 1996 hadi November 2001.

Nitakukumbuka daima hadi Pumzi yangu ya Mwisho nami hapa duniani.
 
Rais bora aliyekuwa akisoma taarifa yeyote kwa unyenyekevu mkubwa akitumia lugha ya kiswahili au kiingereza kwa ufanisi mkubwa, mpenda midahalo na ushindani wa hoja, RIP.
 
Buriani Mh. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, pole kwa Mama Anna na familia yote, pole watanzania, Mungu mpokee mwanao, mpe pumziko la milele eeh Bwana, hakika Ben tutakukumbuka daima, Amen 😭😭😭







 
Maisha ni kuendeleza mazuri na kuacha mabaya. Kama umesoma vizuri post yangu, niliandika kuwa "tutamkumbuka sana" kwa mazuri yake, sikusema kuwa "tutamkumbuka kwa mazuri yake tu". Sijui kama umenielewa
Tuyajue mazuri yake ili tuyaige, Na tuyajue mabaya yake ili tuyaepuke.
 
Tuyajue mazuri yake ili tuyaige, Na tuyajue mabaya yake ili tuyaepuke.
Sijui nini usichoelewa ndugu yangu; sijasema asikumbukwe kwa mabaya yake bali nimesema kuwa akumbukwe sana kwa mazuri yake ,ingawa mabaya yake yatakumbukwa pia. Historia haiwezi kufutika.
 
Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere alifariki baada ya miaka 15 toka kustaafu. Hayati Benjamin William Mkapa kafariki baada ya 15 toka Mustaafu. What a coincidence!!!!! wajameni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom