TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
360E476B-3000-49D0-9834-08E0719A1902.png

Hayati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alizaliwa Masasi, Mtwara 12/11/1938 alisoma Shule ya Msingi Ndanda kisha shule ya Sekondari Pugu, Dar

1962 alipata shahada ya kwanza katika Lugha ya Kiingereza kutoka ktk Chuo Kikuu cha Makerere Uganda
1963 alipata shahada ya uzamili katika masuala ya kimataifa kutoka katika Chuo Kikuu cha Colombia nchini Marekani

Alianza kama Afisa Tawala serikalini
Mwaka 1966-1976 alikuwa Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje
Mwaka 1982-83 alikuwa Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, Mtwara

Kati ya mwaka 1977 hadi 1995 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Habari na Utangazaji, Waziri Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu
Aliongoza Serikali ya awamu ya tatu tangu Novemba 1995 – Novemba 2005
Alikuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa chini ya mfumo wa vyama vingi, ulioasisiwa 1992

Mafanikio
Alifanikisha kuunda, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Wakala wa barabara Tanzania, TANROADS
Taasisi na mifuko ya kuinua wananchi, Mkukuta na mkurabita
Amefariki akiwa na miaka 81
Rais Magufuli kwa masikitiko amesema mzee Mkapa amefariki katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa amelazwa.
===



Mkapa alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia 1995 hadi 2005.

Rais Mkapa alikuwa mtoto wa William Matwani na Stephannia Nambanga.

Muda wa Utawala : 23 November 1995 – 21 December 2005

Makamu wa Rais wakati wa Utawala wake: Omar Ali Juma (1995–2001), Ali Mohamed Shein (2001-05)

Mtangulizi: Ali Hassan Mwinyi

Aliyemfuata: Jakaya Kikwete

Alishawahi kuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kuanzia 1992 – 1995, Waziri wa Habari na Utangazaji, 1990 – 1992

Mkapa alizaliwa 12 Novemba 1938 (umri 81) Ndanda, Masasi, Tanganyika

Ameaga dunia tarehe 24 Julai 2020 Dar es Salaam

Ameacha Mjane Anna Mkapa na watoto wawili.

Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere, Chuo Kikuu cha Columbia.

Fani yake ni mwandishi wa habari, mwanadiplomasia

91459F10-CE5F-4614-B931-81707FF94825.jpeg


PIA SOMA:

= >
Je, Benjamini Willium mkapa ni nani hasa?

===MAZISHI===
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mwili wa Mzee Mkapa utazikwa kijijini kwao Lupaso,Masasi Mkoani Mtwara Jumatano ya wiki ijayo July 29,2020 saa nane mchana, mwili utasafirishwa kwa Ndege Jumanne July 28 mchana baada ya kuagwa DSM, utatua Uwanja wa Nachingwea,Lindi kisha kuelekea Masasi.

Historia|Wasifu: Je, Benjamin William Mkapa ni nani hasa?
 
Status
Not open for further replies.
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom