Rais wa Tanzania sio rais wa Tanganyika (Wazanzibar hamjui hili?)

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Nimesikitishwa na kauli za wazanzibari (kupitia kwa wabunge wao) na wengine humu JF wanaolazimisha kuwa rais wa Zanzibar na rais wa Tanzania wawe na mamlaka sawa katika suala la katiba na mustakabali wa nchi yetu.

Urais wa Tanzania sio Jakaya Kikwete. Leo hii JK akifa, ni wazi kuwa Mohamed Gharib Bilal atapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kwa hiyo, itawezekanaje Bilal na Shein wakae kuzungumzia mustabali wa Kigoma, Mwanza, Mbeya, Bukoba, Mtwara, Tanga, nk? Kauli za wabunge hawa zinamfanya JK kuonekana kuwa ni rais wa Tanganyika na si rais wa Muungano.

Ni ‘ujuha' kwa rais wa Tanzania kutembelea Zanzibar kama mgeni wa kitaifa wakati yupo katika nchi anayoitawala! Rais huyo huyo anapokwenda Dodoma haendi kama mgeni bali mkuu wan chi yake. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA. Kwa kuongezea tu, sasa ifikie wakati kwa wabunge kukaa kama ‘bunge la Tanganyika' na kuwatoa nje wabunge wa Zanzibar pale yanapojadiliwa mambo yasiyowahusu wa-zenji.

Kama watawaonea aibu wabunge wa Zanzibar pale Dodoma, basi wafufue bunge la Tanganyika pale Karimjee (kwa masaburi) ili Tanganyika iweze kuongea kama Tanganyika bila mwangwi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Mungu ibariki Tanganyika
 
Kwani kuna Serikali ya Tanganyika.?

Nani rais wake?

Umeuliza vema, japo jibu walijua. Kwahiyo si sahihi kwa mtu na bosi wake kuwekwa level moja inapokuja katika suala la katiba. Mwinyi na Salmin wasingeweza kukaa kujadili mambo yanayohusu Biharamulo. Kwa hiyo JK hawezi kukaa na Shein wakiwa ktk level moja, huyu ni rais wa Tz na mwingine ni rais wa znz (iliyomo ndani ya tz).
 
Huu muungano bwana! Wazanzibar wandadeka, Watanganyika wanawabembeleza weee! Ipo siku mtapata rais kutoka Tanganyika ambaye haogopi mzimu wa Mwalimu, atafanya maamuzi kama yanavyotakiwa ndio mtajua tuliungana tukawa nchi mmoja itwaayo TANZANIA na sio Tanzania na Zanzibar kama ilivyo sasa.
Nawashauri wale wa visiwani waache kujiita Wanzanizibar, tufanye kama hapo zamani mwalimu alipokuwa anasimamia, tulijiita Mtanzania bara na visiwani.
 
hapo nilipo bold, hadi sasa najiuliza nani anawabembeleza hawa watu? mbona mie mtanganyika na ninauchukia huu muungano kama ninavyomchukia mzee wa kasi zaidi na ari zaidi.
 
Nadhani imefika wakati wa Tanganyika (wadanganyika) kudai taifa letu, uhuru wetu wa mawazo kwa kuwa wenzetu wana sauti kweli tena ya uakli wanapozungumzia ZNZ yao sisi tukizungumzia Danganyika yetu tunaambiwa ni uhaini
 
Mimi nadhani ni sahihi kabisa kwamba Rais wa Tanzania ni Rais wa Tanganyika tu. Nasema hivyo kwa sababu huyo raisi tunayemwita wa Tanzania hana mamlaka ya uteuzi zanzibar. Hawezi kuteua wakuu wa wilaya, wa mikoa na watendaji wengine wa serikali. Kwa ujumla Zanzibar hana power yoyote ile, zaidi ni mambo ya kudanganyana kisiasa tu.
 
Serikali tatu hapana! Kama tumeungana lazima kiwe kitu kimoja,kama mke na mume wanakuwa kitu kimoja kwanin isiwe Tanganyika na Zanzibar? Kama ni muungano iwe Tanzania moja Zanzibar iwe kanda kama ilivyo kanda ya ziwa na mikoa yake.!
 
Na ndio maana imefika wakati eti wanadai rais wa Tanzania awe na hadhi sawa na yule wa Zanzibar, kwa maana hiyo akichaguliwa rais mzanzibari kuongoza Tanzania ndio kusema watanganyika tutakuwa 'koloni' la Zanzibar. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA
 
Haya ndo matokeo ya kuwabeba watu then wanageuka wababe!Kichefuchefu pu!Sitaki kusikia upopompo mm,but time will tell kwani migongo inauma jamani tembeeni sasa!
 
Mwaka huu tunasherekea miaka hamsini ya Uhuru wa nchi gani?
Tanganyika huru (1961-1964) age 2yrs 4months
Tanzania (URT) (1964- to date) age 47 years
sasa hii miaka hamsini ya kitu gani? I stand to be corrected!

Utata huu usingekuwepo tukiweka haya mambo sawa
 
Tungekuwa na serikali tatu, utata wote huu usingekuwepo.
Nimeshauliza lakini sijapata jibu. Hivi kiongozi wa serikali ya tatu atakuwa na kazi gani katika mfumo wa serikali tatu? Hivi sasa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye rais wa Tanganyika. Ni amiri jeshi mkuu na ana executive power on issues za Tanganyika. Huyu wa serikali ya tatu atapachikwa wapi na mamlaka yake yataishia wapi? Nijibuni jamani. Sijauliza gharama za kuendesha serikali tatu bado.
 
Serikali tatu hapana! Kama tumeungana lazima kiwe kitu kimoja,kama mke na mume wanakuwa kitu kimoja kwanin isiwe Tanganyika na Zanzibar? Kama ni muungano iwe Tanzania moja Zanzibar iwe kanda kama ilivyo kanda ya ziwa na mikoa yake.!
wewe koma kabisa kufananisha muungano wa nnchi hizi kama vile ndoa hii sio ndoa na wala haiwezi kuwa ndoa milele kwa huwezi kusema ni nani kaolewa sasa hapo au nani ni mume wa mwenzake
 
Na ndio maana imefika wakati eti wanadai rais wa Tanzania awe na hadhi sawa na yule wa Zanzibar, kwa maana hiyo akichaguliwa rais mzanzibari kuongoza Tanzania ndio kusema watanganyika tutakuwa 'koloni' la Zanzibar. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA
Cricifix, chance ya mwisho kwa Mzanzobari kuwa rais wa JMT ni ile ya Dr. Salim. Hakuna tena nafasi kwa Mzazibari kuchaguliwa hivyo kamwe haitatokea tukawa koloni lao!.
 
Mwaka huu tunasherekea miaka hamsini ya Uhuru wa nchi gani?
Tanganyika huru (1961-1964) age 2yrs 4months
Tanzania (URT) (1964- to date) age 47 years
sasa hii miaka hamsini ya kitu gani? I stand to be corrected!

Utata huu usingekuwepo tukiweka haya mambo sawa

mambo madimu!!
 
Nimesikitishwa na kauli za wazanzibari (kupitia kwa wabunge wao) na wengine humu JF wanaolazimisha kuwa rais wa Zanzibar na rais wa Tanzania wawe na mamlaka sawa katika suala la katiba na mustakabali wa nchi yetu.

Urais wa Tanzania sio Jakaya Kikwete. Leo hii JK akifa, ni wazi kuwa Mohamed Gharib Bilal atapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kwa hiyo, itawezekanaje Bilal na Shein wakae kuzungumzia mustabali wa Kigoma, Mwanza, Mbeya, Bukoba, Mtwara, Tanga, nk? Kauli za wabunge hawa zinamfanya JK kuonekana kuwa ni rais wa Tanganyika na si rais wa Muungano.

Ni ‘ujuha' kwa rais wa Tanzania kutembelea Zanzibar kama mgeni wa kitaifa wakati yupo katika nchi anayoitawala! Rais huyo huyo anapokwenda Dodoma haendi kama mgeni bali mkuu wan chi yake. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA. Kwa kuongezea tu, sasa ifikie wakati kwa wabunge kukaa kama ‘bunge la Tanganyika' na kuwatoa nje wabunge wa Zanzibar pale yanapojadiliwa mambo yasiyowahusu wa-zenji.

Kama watawaonea aibu wabunge wa Zanzibar pale Dodoma, basi wafufue bunge la Tanganyika pale Karimjee (kwa masaburi) ili Tanganyika iweze kuongea kama Tanganyika bila mwangwi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Mungu ibariki Tanganyika
mkuu umenena jambo la mbolea ,tunahitaji watanganyika wazalendo wa kuikomboa TANGANYIKA YETU
 
Hiv nin maana ya muungano?.
Unaunganisha vitu viwili au zaid unapata kitu kimoja kikubwa zaid ya vile vya mwanzo vikiwa kimoja kimoja.
Vitu viwili au zaid vinaamua kushirikiano vnabak kkt idad yao kwa yale mambo yasiyo ya ushirikiano.
Hapa kwetu hatujaunga bali tumeshirikiana, ndio maana kuna serikal mbil. Labda katiba mpya iruhusu muungano, ila hii ni ya ushrkiano. Wananch waelimishe, Kikwete analitambua, wananch hatulijui tunapga kelele.
 
Cricifix, chance ya mwisho kwa Mzanzobari kuwa rais wa JMT ni ile ya Dr. Salim. Hakuna tena nafasi kwa Mzazibari kuchaguliwa hivyo kamwe haitatokea tukawa koloni lao!.

Pasco siafikiani na wewe. Ninaangazia 'angles' zote mkuu. Ni kwa kujiamini huko ndio maana tumejiachia bila tahadhari kwa kudhani kuwa siku zote rais wa muungano hatatoka znz kupitia uchaguzi na eti bara tutatawala siku zote kwa uwingi wetu. Vipi rais akifa akiwa madarakani na katiba inatamka makamu ndiye anachua urais? Bado utasema tena kuwa chance ya mwisho ilikuwa kwa Dr Salim? Au kuna mkakati wa rais na makamu wote kutoka Tanganyika?
 
Back
Top Bottom